Kuna uwezekano gani wa AI kuleta madhara kwa binadamu?

Chanzo cha picha, GettyImages
Hatua zinazopigwa katika teknolojia ya ya akili mnemba (AI) yanazidi kuongeza hofu miongoni mwa watu kuhusu mustakabali wa dunia.
Kulingana na utafiti uliofanywa, zaidi ya nusu ya watu duniani wana hofu kuhusu AI.
Kulingana na wachambuzi, matumizi yasiyodhibitiwa ya akili mnemba yanaweza kuwa na madhara makubwa na ni miongoni mwa vitisho vinavyowatia wasiwasi wataalamu.
Kuhusiana na AI, mgogoro kati ya Anthropic na OpenAI umeibua zaidi suala la usalama wa teknolojia hiyo.
Kwa sasa, uwezekano wa AI kusababisha madhara makubwa unakadiriwa kuwa takriban asilimia 10. Hata hivyo, iwapo maendeleo ya AI yataendelea bila kuwepo kwa vizuizi au udhibiti wa kutosha, baadhi ya wataalamu wanakadiria uwezekano wa AI kupunguza ustaarabu wa binadamu kufikia takriban asilimia 20.
Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na wataalamu wa AI.
Utafiti huo ulifanywa na chuo cha Massachusetts Institute of Technology (MIT), mojawapo ya vyuo vikuu vinavyoongoza duniani katika masuala ya teknolojia.
Orodha ya hofu
Watafiti hao waliandaa orodha ya matukio 24 yanayoweza kutokea na kutathmini kiwango ambacho kila tukio linaweza kuwa "janga" ifikapo mwaka wa 2030.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Majanga hayo yanaweza kumaanisha, kwa mfano, vifo vya zaidi ya watu milioni moja au hasara za kiuchumi zinazozidi dola bilioni 100.
Pia kuna uwezekano wa kudhoofika au kuporomoka kwa misingi ya demokrasia, pamoja na kuharibiwa kwa haki ya watu binafsi.
Ukosefu mkubwa wa ajira, ambao ni miongoni mwa hofu kuu zinazohusishwa na AI, unashika nafasi ya nne katika orodha ya madhara yanayoweza kusababishwa na akili bandia.
Wataalamu wana hofu kwamba jambo hatari zaidi ni akili mnemba (AI) ambayo haiwezi kudhibitiwa.
Katika hali hiyo, AI inaweza kusababisha madhara makubwa kwa binadamu.
Inasemekana hali hiyo inaweza kutokea, kwa mfano, kutokana na matatizo ya kiufundi, vitendo vya watu wenye nia ovu, au pale ambapo malengo ya AI hayaendani na maslahi ya binadamu.
Madhara hayo yanaweza kujumuisha: ulaghai, utengenezaji wa silaha, udanganyifu na ushawishi wa watu, kuingilia siasa, mashambulizi ya kimtandao, au kuundwa kwa mfumo wa AI wenye uwezo wa hali ya juu.
Pia kuna hofu kwamba AI inaweza kufikia hatua ya kuelewa jinsi inavyofanya kazi na kujiboresha yenyewe na kuwa hatari zaidi kwa usalama.
Miongoni mwa hatari hizo ni utengenezaji wa silaha kwa kutumia AI, ikiwa ni pamoja na silaha zinazoweza kutumika katika mashambulizi ya kimtandao na zile zinazolenga kusababisha vifo vya watu kwa kiwango kikubwa.
Wakati huo huo, "utawala wa nguvu za AI" pia unaonekana kuwa tishio.
Hii inahusisha mkusanyiko wa rasilimali mikononi mwa idadi ndogo sana ya watu, ambao wanaweza kutumia teknolojia za hali ya juu zaidi, hali inayoweza kuongeza ukosefu wa usawa wa kijamii na kiuchumi.
Je, udhibiti wa AI uko mikononi mwa nani?

Chanzo cha picha, GettyImages
Kwa mfano, kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa kimataifa uliofanywa na Stanford AI Index, idadi ya watu wanaoiona AI kuwa "ya kutia wasiwasi" iliongezeka kutoka asilimia 39 mwaka 2022 hadi asilimia 52 mwaka wa 2025.
Wakati huohuo, idadi ya watu ambao hawaogopi maendeleo ya AI na badala yake wanayakaribisha, haikubadilika, ikiwa kati ya asilimia 53 na 54.
Hata hivyo, kulingana na watafiti, kuongezeka kwa wasiwasi miongoni mwa umma hakujasababisha kuanzishwa kwa vikwazo vya kutosha dhidi ya maendeleo ya AI.
Sababu moja ni kwamba watoa maamuzi wana maslahi katika maendeleo ya AI, huku wao pia wakiwa na ushawishi mkubwa wa kudhibiti mchakato huo.
Lakini watu ambao maisha yao yanaweza kuwa hatarini zaidi kutokana na teknolojia hii hawana uwezo mkubwa wa kushawishi au kubadilisha mchakato huo.
Wapi pa kufanya kazi?

Chanzo cha picha, EPA
Wataalamu walitathmini kiwango cha hatari katika sekta 14 za uchumi.
Matokeo mabaya zaidi yalirekodiwa katika sekta za teknolojia ya habari na usalama wa taifa.
Sekta ya habari inaweza kukabiliwa na vitisho kama vile taarifa potofu, udanganyifu wa maoni ya umma na uvamizi wa faragha.
Kwa upande wa usalama wa taifa, mifumo ya AI
inaweza kukabiliwa na mashambulizi ya kimtandao pamoja na aina mpya za silaha.
Sekta ya fedha nayo iko katika hatari
Kwa upande mmoja, AI inaweza kufanya iwe vigumu zaidi kupambana na ulaghai na udanganyifu katika masoko. Kwa upande mwingine, matumizi yake kwa kiwango kikubwa katika ngazi mbalimbali yanaweza kuongeza ukubwa wa madhara yanayoweza kutokea endapo mifumo hiyo itashindwa kufanya kazi.
Hata hivyo, AI haitishi sekta zote kwa kiwango sawa.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa hatari, kwa sasa AI bado haina uwezo wa kusababisha madhara makubwa katika maeneo ambayo teknolojia hiyo haitumiki sana.
Kwa mfano, sekta ya hoteli na migahawa, kilimo, uzalishaji viwandani, pamoja na utamaduni na burudani zinaonekana kuwa miongoni mwa sekta ambazo hazijaathirika pakubwa na AI.















