Moja kwa moja, Trump: Iran ichague, kutatua mzozo kwa njia ngumu au rahisi

“Nina uamuzi wa kufanya kuhusu Iran,” Trump aliwaambia waandishi wa habari alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya White House kuelekea kwenye mkutano wa hadhara huko Vandalia, Ohio.

Muhtasari

Trump: Iran ichague, mazungumzo au makabiliano

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Kiongozi wa Ujerumani atoa wito wa kuizuia Urusi mapema

    d

    Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, amewasili katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, akisema Rais Volodymyr Zelenskiy anaweza kutegemea uungwaji mkono wa Ujerumani, huku mashambulizi ya Urusi yakizidi.

    Merz, pamoja na wakuu wa kampuni kadhaa za ulinzi, amesema mashine ya vita ya Urusi itaelekeza nguvu zake kwa nchi nyingine iwapo haitazuiwa.

    Ujerumani inaipatia Ukraine msaada wa kijeshi wenye thamani ya hadi euro bilioni moja, ukiwemo mifumo ya ulinzi ya kukabiliana na ndege mpya zisizo na rubani zinazotumia injini za ndege, zinazotumiwa na Urusi.

    Rais Zelenskiy amesema Vladimir Putin anaidhinisha mashambulizi yanayolenga raia, baada ya kushindwa kupata ushindi wa kijeshi.

    Soma Pia:

  2. Australia yachunguza uhusiano wa rubani msaidizi wa Flydubai na nchi hiyo

    d

    Mamlaka za Australia zinafanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na rubani msaidizi wa shirika la ndege la Flydubai, ambaye anadaiwa kujaribu kutwaa udhibiti wa ndege iliyokuwa ikielekea Israel.

    Rubani huyo msaidizi anadaiwa kumshambulia rubani mkuu kwa kutumia shoka la dharura wakati wa safari ya ndege kutoka Dubai kuelekea Tel Aviv, kabla ya abiria kumzidi nguvu na kufanikiwa kurejesha udhibiti wa ndege hiyo.

    Mamlaka za Australia hazijamtaja rasmi rubani huyo msaidizi, ambaye ametajwa na vyombo kadhaa vya habari, vikiwemo Reuters, CNN na The New York Times, kuwa ni Hamam al-Hammami.

    Mwendesha mashtaka nchini Umoja wa Falme za Kiarabu amesema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo pamoja na sababu zinazoweza kuwa nyuma ya kitendo hicho.

    Katika taarifa yake kwa BBC, Polisi wa Shirikisho la Australia (AFP) wamethibitisha kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu “uhusiano wa mtu huyo na Australia.”

    AFP imesema uchunguzi huo unahusisha polisi wa majimbo pamoja na chombo cha usalama cha taifa, na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa “kwa wakati mwafaka.”

    Vyanzo vinavyofahamu suala hilo, vilivyozungumza na vyombo vya habari vya Australia, vimesema rubani huyo msaidizi alipewa viza ya mwanafunzi mwaka 2014 na kusoma nchini Australia kati ya mwaka 2015 na 2017, kabla ya kuondoka nchini humo.

    Shirika la Utangazaji la Australia (ABC) limeripoti kuwa visa yake ya mwanafunzi ilifutwa mwaka 2019 baada ya kutokuwa tena amejiandikisha katika kozi, hali iliyomfanya asistahili kuendelea kuwa na visa hiyo.

    Soma Zaidi Hapa:

  3. Meli ya kivita ya Marekani yatia nanga Thailand huku mvutano na Iran ukiendelea

    f

    Meli ya kubeba ndege za kivita ya Marekani, USS George H.W. Bush, imewasili Phuket, Thailand, siku ya Jumapili, huku takriban wanajeshi 4,800 wa kikosi chake wakipewa mapumziko.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, meli hiyo imekuwa ikishiriki katika operesheni za Marekani kwa miezi kadhaa, wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukizidi.

    Reuters, ikinukuu vyombo vya habari vya eneo hilo, imeripoti kuwa meli hiyo itatia nanga katika maji ya pwani, huku wanajeshi wake wakitarajiwa kushuka na kutumia siku tano katika kisiwa hicho.

    Ziara hiyo inakuja mwezi mmoja baada ya meli nyingine ya kubeba ndege za kivita ya Marekani, USS Abraham Lincoln, kutia nanga katika bandari ya Laem Chabang, ambako takriban wanajeshi 5,000 wa kikosi chake walipata muda wa mapumziko.

    Soma pia:

  4. Argentina yaitandika Burkina Faso 7-0 katika mechi ya kirafiki

    Argentina imeifunga Burkina Faso mabao 7-0 katika Uwanja wa Monumental usiku wa Jumamosi, katika mchezo wa kwanza kati ya miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Afrika.

    Hii ilikuwa mechi ya kwanza kabisa kwa ngazi ya timu za taifa za wakubwa kukutanisha Argentina na Burkina Faso, huku timu hizo zikitenganishwa na nafasi 60 katika viwango vya hivi karibuni vya FIFA.

    Argentina ilikuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza tangu Lionel Messi alipotangaza mwezi Agosti kuwa anaacha kuichezea timu ya taifa.

    Messi hakuitwa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Burkina Faso, lakini anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Argentina kwa mchezo wake wa kuaga dhidi ya timu nyingine ya Afrika, Benin, utakaochezwa Jumanne.

    Lautaro Martínez aliifungia Argentina bao la kwanza dakika ya nne, akianza safari ya ushindi mkubwa kwa wenyeji.

    Argentina ilifunga mabao matano katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza mengine mawili baada ya mapumziko na kukamilisha ushindi huo wa mabao saba.

    Mchezo huo ulichezwa mbele ya mashabiki wachache katika Uwanja wa Monumental kufuatia adhabu zilizowekwa na FIFA dhidi ya Argentina baada ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania.

    Burkina Faso ilipata nafasi tatu za kulenga lango, lakini ni moja pekee iliyolenga lango. Kipa Abdoul Guira alikuwa na kazi kubwa usiku huo mjini Buenos Aires, akifanya sevu 11.

    The Stallions waliwasili kwa kuchelewa katika mji mkuu wa Argentina baada ya kukumbwa na ucheleweshaji nchini Morocco, hali iliyovuruga maandalizi yao kwa mchezo huo.

    Kabla ya mchezo huo, Burkina Faso ilikuwa imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Benin na kuifunga Jamhuri ya Afrika ya Kati 1-0 katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

    Kikosi hicho kilikuwa pia kimefeli kufunga katika michezo sita kati ya saba iliyopita iliyopoteza, na matokeo ya Jumamosi yameendeleza mwenendo huo.

    Kwa upande wa Argentina, uhusiano wa soka la taifa hilo na Afrika una historia ndefu. Hivyo, ni jambo la kipekee kuona timu za Afrika zikipewa nafasi katika wiki ya kuaga kwa Messi.

    Messi amekutana na Nigeria katika baadhi ya nyakati muhimu za safari yake ya kimataifa, kuanzia fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la vijana chini ya miaka 20 mwaka 2005 hadi fainali ya soka ya Olimpiki mwaka 2008, michezo yote miwili ambayo Argentina ilishinda.

    Pia amekutana na Super Eagles katika Kombe la Dunia mara tatu na kufunga mabao matatu dhidi ya Nigeria katika michuano ya mwaka 2014 na 2018.

  5. Trump: Iran ichague, kutatua mzozo kwa njia ngumu au rahisi

    G

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema mzozo kati ya Iran na Marekani unaweza kutatuliwa kwa “njia ngumu au njia rahisi.”

    “Nina uamuzi wa kufanya kuhusu Iran,” Trump aliwaambia waandishi wa habari alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya White House kuelekea katika mkutano wa hadhara huko Vandalia, Ohio.

    Trump pia alisema Iran “imedhoofishwa kwa kiasi kikubwa” kutokana na hatua na operesheni za Marekani, na kwamba nchi hiyo “imekaribia kabisa kuachana na mipango yoyote ya kujipatia silaha za nyuklia.”

    Hata hivyo, Iran imeendelea kukanusha mara kwa mara madai kwamba inajaribu kujipatia silaha za nyuklia.

  6. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ya tarehe 04/10/2026.