Kisa cha mume kumlazimisha mkewe kushiriki ngono na wanaume 120

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Onyo: Taarifa hii huenda ikawakwaza baadhi ya wasomaji.

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 61 kutoka Uswidi, amehukumiwa kifunho cha miaka minne na miezi mitano jela, kwa kumlazimisha mkewe kushiriki ngono na zaidi ya wanaume 120.

Mahakama iiliskiza kesi hiyo iliyomshtumu mwanaume huyo kwa kutumia vitisho na nguvu kumlazimisha mwanamke huyo kushiriki ngono na wanaume hao, huku nyumba yao ikiwa na camera za kurekodi.

Baada ya kesi hiyo kumalizika eneo la Harnosandm Uswidi, mwanaume huyo alipatikana na makosa kadhaa ikiwemo ubakaji, kumlazimisha mtu kutoa huduma za ngono, mateso, kuzuiliwa kinyume cha sheria na vitisho.

Mahakama hiyo pia iliwapata na hatia wanaume wengine 28 kwa kujihusisha na Sakata hiyo ya kuwalazimisha watu kushiriki ngono.

Kesi hiyo ilipata umaarufu baada ya kufananishwa na ile ya Dominique Pellicot kutoka Ufaransa, ambaye alikuwa akimpa dawa za kulevya mkewe na kuruhusu wanaume tofauti kumbaka kwa kipindi cha miaka tisa.

Mwanaume huyo kutoka Uswidi amekanusha mashtaka dhidi yake na kusema alishiriki tu ngono ambayo aliruhusiwa kufanya.

Ila mahakama ilimpata na hatia ya mwanaume huyo 'kwa kumtumia mwanamke huyo vibaya'

Waendesha mashtaka wanasema mwanaume huyo alianza kumlazimisha mkewe kushiriki ngono na wanaume wengine mwaka wa 2022 kwa ajili ya pesa.

Watu kutoka maeneo tofauti walikuwa wakitembelea nyumbani kwao eneo la Karam Force kwa ajili ya kushiriki ngono hadi mwaka wa 2025 ambapo mwanamke huyo alimripoti kwa polisi.

Kulingana na waendesha mashtaka, mwanaume huyo alikuwa akimpea mkewe dawa za kulevya na kumdhibiti na kumzuia nyumbani kwao.

Kulingana na waendesha mashtaka, mshtakiwa alitishia kumuua mkewe, kumwagia mafuta na kumteketeza na moto.

Mahakama ilitoa hukumu kuwa mwanaume huyo alimtishia na kumuogofya mkewe, na kumlazimisha kujiweka mitandaoni kwa nia ya kuwavutia wateja wanaotaka kushiriki ngono.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kulingana na mahakama haya yote yalitekelezwa chini ya shinikizo kubwa na kumtukana mara kadhaa.

Kulingana na mahakama mwanaume huyo alifanya kushiriki ngono na mkewe kuwa biashara aliyosimamiwa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu, chini ya sheria za Uswidi, mashtaka ya ubakaji yanaweza kufunguliwa hata kwa unyanyasaji wa kingono ambao unachukuliwa kuwa wa kiwango sawa na ngono ya kulazimishwa au ubakaji.

Mahakama pia ilimpata mwanamume huyo na hatia ya jaribio moja la ubakaji, lakini ilitupilia mbali mashtaka mengine matatu dhidi yake.

Mbali na kifungo cha jela, mahakama pia iliamuru mshtakiwa kumlipa fidia ya takriban pauni 15,900 .

Ingawa mahakama iliwatambua wanaume 120 waliopokea huduma za kingono zilizotolewa na mshtakiwa huyo, ni 29 pekee waliofunguliwa mashtaka katika kesi hiyo.