Tetesi za soka Ulaya: Arsenal kulazimika kutoa ofa ya zaidi ya £60m ili kumsajili Osimhen

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Victor Osimhen
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal lazima watoe ofa ya zaidi ya pauni milioni 60 ili kuwa na nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Galatasaray msimu huu. (Football Insider)

Aston Villa wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kipa wa Japan, Zion Suzuki, kutoka Parma baada ya uhamisho uliopangwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwenda Paris St-Germain kufeli. (Talksport)

Nia ya Villa kwa Suzuki imeongeza matumaini ya Juventus kumsajili kipa wa Argentina, Emiliano Martinez, mwenye umri wa miaka 33, kutoka klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza. (Football Italia)

Barcelona wanaamini ofa yao ya tatu ya euro milioni 70 (pauni milioni 59.8) kwa ajili ya Rodri itatosha kuwashawishi Manchester City kumuuza kiungo huyo wa Uhispania, mwenye umri wa miaka 30. (AS - In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ayyoub Bouaddi

Manchester City wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Morocco, Ayyoub Bouaddi, kutoka Lille, ambao wanataka angalau pauni milioni 85 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Telegraph - Subscription Required)

Newcastle wamefufua mazungumzo ya kumsajili Joao Palhinha wa Bayern Munich, mwenye umri wa miaka 31, huku Aston Villa na Benfica pia wakionyesha nia kwa kiungo huyo wa Ureno. (Mail)

Inter Milan wana nia ya kumuuza winga wa Brazil, Luis Henrique, mwenye umri wa miaka 24, ili kupata fedha za kumsajili kiungo wa Uingereza na Liverpool, Curtis Jones, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anatarajiwa kugharimu takriban euro milioni 40 (pauni milioni 34). (Corriere dello Sport - In Itali)

Chelsea wanataka pauni milioni 60 kwa ajili ya Nicolas Jackson, huku Aston Villa, Tottenham na Atletico Madrid wakiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia mshambuliaji huyo wa Senegal, mwenye umri wa miaka 25. (RMC Sport - In French)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jackson

Mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 23, anataka kubaki Ligi Kuu ya Uingereza licha ya nia kutoka Como, huku Newcastle na Everton wakifuatilia hali yake. (Talksport)

Mshambuliaji wa Uholanzi, Cody Gakpo, mwenye umri wa miaka 27, ameweka wazi kwa Liverpool kuwa anataka kuondoka klabuni hapo na kujiunga na Tottenham. (Teamtalk)

Benfica wana nia ya kumsajili beki wa Uingereza, Tosin Adarabioyo, mwenye umri wa miaka 28, ambaye amepoteza nafasi yake ya kwanza katika safu ya ulinzi ya Chelsea. (Offside Trap)