Tetesi za Usajili Ulaya: Barca yaongeza dau la Rodri, Romero aitaka Arsenal

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Barcelona imeongeza ofa yake hadi £51.4m kwa ajili ya kiungo wa Manchester City na Hispania, Rodri, mwenye miaka 30. Mazungumzo kati ya klabu hizo yanaendelea. (Sport)

Beki wa kati wa Argentina, Cristian Romero, anataka kujiunga na Arsenal, lakini Tottenham haina mpango wa kumruhusu mchezaji huyo mwenye miaka 28 kuhamia kwa wapinzani wake wa London Kaskazini. (Sun)

Romero pia ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Barcelona, huku klabu hiyo ikitarajiwa kumruhusu beki wake wa Uruguay, Ronald Araujo, mwenye miaka 27, kujiunga na Liverpool kwa mkopo. (Mundo Deportivo)

Nottingham Forest iko karibu kumsajili beki wa kati wa Ivory Coast, Ousmane Diomande, mwenye miaka 22, kutoka Sporting kwa £34m. (The Athletic)

Mshambuliaji wa Hispania, Ferran Torres, mwenye miaka 26, ameiambia Barcelona kwamba anataka kujiunga na Paris St-Germain, baada ya kufikia makubaliano ya maslahi binafsi na mabingwa hao wa Ulaya. (ESPN)

Everton na Crystal Palace zimefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kubadilishana wachezaji, winga wa Everton Dwight McNeil kwenda Palace na winga wa Palace, Brennan Johnson kwenda upande wa pili. (Times)

Fenerbahce iko tayari kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, mwenye miaka 33, kutoka Napoli. Napoli italazimika kuilipa Chelsea sehemu ya ada ya mauzo ya mchezaji huyo. (Gazzetta dello Sport)

Tottenham iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Manchester City kuhusu kumsajili winga wa Brazil Savinho, huku ofa yenye thamani ya karibu £60m ikiaminika kuwa inaweza kukamilisha dili hilo. (Football Insider)

Aston Villa iko karibu kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Italia Matteo Ruggeri, mwenye miaka 24, kutoka Atletico Madrid. (The Athletic)

Leeds United bado inaweza kumsajili kiungo wa Southampton Shea Charles, lakini italazimika kutoa zaidi ya £30m, ambayo ndiyo ofa ya sasa ya Fulham kwa mchezaji huyo wa Ireland Kaskazini. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Füllkrug amekubaliana masharti binafsi na Venezia, lakini dili hilo limekwama kutokana na ada inayotakiwa na West Ham. (Bild)

West Ham imefikia makubaliano ya awali kumsajili winga wa Israel Manor Solomon, mwenye miaka 27, kutoka Tottenham. (The Athletic)