Wafcon 2026: Timu nne za Afrika zafuzu Kombe la Dunia la Wanawake

Hj

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Morocco wamefuzu Kombe la Dunia la Wanawake kwa mara ya pili baada ya kupoteza dhidi ya Ufaransa katika hatua ya 16 bora mwaka 2023.
    • Author, Michael Emons
    • Nafasi, BBC
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Algeria, Morocco, Cameron na Malawi zote zimefuzu kwenda kwenye Kombe la Dunia la Wanawake la 2027 nchini Brazil.

Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcon) nchini Morocco pia linafanya kazi kama mashindano ya kufuzu kwenda Kombe la Dunia la Wanawake msimu ujao wa joto, huku nchi yoyote inayofika nusu fainali ikipata nafasi ya kwenda Kombe la Dunia.

Algeria iliwashinda wachezaji 10 Ivory Coast 2-1, kwa mabao kutoka kwa Ines Khiri na Amira Ould Braham - baada ya N'Sira Oudraogo kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Ivory Coast walikuwa mbele kwa 1-0 - na hivyo Algeria kufika nusu fainali ya Wafcon na kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake kwa mara ya kwanza.

Mabao ya Sakina Ouzraoui Diki na Hanane Ait El Haj yaliisaidia Morocco kuishinda Afrika Kusini 2-1 na kufika nusu fainali.

Cameroon imefika nusu fainali baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Nigeria kutokana na mpira wa adhabu wa yadi 30 uliopigwa na Myriam Nyadjou mwenye umri wa miaka 19.

Timu ya nne kuingia nusu fainali ni Malawi, ya 153 katika orodha ya dunia, ambayo imeleta mshangao mkubwa kwa kuishinda Ghana 2-1, ikitoka nyuma kwa mabao ya Temwa Chawinga na Rose Kadzere.

Nusu fainali ya Wafcon itafanyika Jumatano ambapo Morocco itacheza na Cameroon na Algeria kukutana na Malawi.

18 zafuzu Kombe la Dunia

Jjj

Chanzo cha picha, CAF

Maelezo ya picha, Timu ya Malawi

Mataifa manne yaliyopoteza katika robo fainali ya Wafcon - Ghana, Ivory Coast, Nigeria na Afrika Kusini - bado yana nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Siku ya Alhamisi, Ivory Coast itacheza na Ghana na Nigeria itacheza na Afrika Kusini huku washindi wawili wakiingia katika mechi za mchujo za mataifa 10 kutoka mabara mengine mwezi Novemba na Desemba.

Kati ya nchi hizo 10 katika mechi za mchujo, tatu zitafuzu Kombe la Dunia la msimu ujao wa joto, litakaloanza Juni 24 na kumalizika Julai 25.

Uingereza, Jamhuri ya Ireland, Wales, Scotland na Ireland Kaskazini zote bado zina nafasi ya kufuzu kupitia mechi za mchujo za Ulaya, ambazo zitafanyika kuanzia Oktoba hadi Desemba.

Kutakuwa na mataifa 32 yatakayoshiriki Kombe la Dunia la Wanawake la 2027 nchini Brazil na mataifa 18 yalliyo fuzu tayari yanajulikana.

Nchi ambazo zimefuzu Kombe la Dunia la Wanawake la 2027 hadi sasa:

Afrika - Algeria, Cameron, Malawi, Morocco.

Asia - Australia, China, Japani, Korea Kaskazini, Ufilipino, Korea Kusini.

Ulaya - Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania.

Oceania - New Zealand

Amerika Kusini - Argentina, Brazili (wenyeji), Colombia.