Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Fernandez kuigharimu Man City zaidi ya pauni milioni 120

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City italazimika kuilipa Chelsea zaidi ya pauni milioni 120 ili kumsajili kiungo wa Argentina, Enzo Fernandez, endapo wataamua kukamilisha dili hilo katika wiki mbili za mwisho za la usajili wa wachezaji. (Telegraph - usajili unahitaji)
Chelsea inataka takribani pauni milioni 100 kumuachia winga wa Ureno, Pedro Neto (26), msimu huu wa joto, huku klabu ya Al-Hilal ya Ligi ya Saudi Pro ikihusishwa na mpango wa kumsajili. (Mail -usajili unahitaji)
Manchester City, Arsenal na Tottenham pia zote zinaonyesha nia ya kumsajili Neto, ambaye alijiunga na Chelsea akitokea Wolves kwa ada ya pauni milioni 54 mwaka 2024. (Metro)
Manchester United imepewa fursa ya kumsajili kiungo wa Uhispania, Marc Casado (22), ambaye klabu ya Barcelona imemweka sokoni. (Sport - kwa Kihispania)
Klabu ya Galatasaray imempa kiungo wa Ureno Bruno Fernandes ofa ya pauni milioni 18.3 kwa msimu licha ya Manchester United kusita kumuuza— kiasi ambacho ni mara mbili ya mshahara wake wa sasa — ili kumshawishi aondoke Old Trafford. (Telegraph - usajili unahitaji)
Liverpool bado ina nia ya kuwasajili wachezaji wawili wa Paris St-Germain, Bradley Barcola (miaka 23) na Ibrahim Mbaye (miaka 18), huku kukiwa na mazungumzo kuhusu ada ya jumla ya pauni milioni 155 kwa winga huyo wa Ufaransa na mshambuliaji huyo wa Senegal. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich ina imani ya kufikia makubaliano mapya na mshambuliaji wa England Harry Kane (miaka 33), ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake. (Bild - kwa Kijerumani)
Como wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina na Italia, Moise Kean (26), kwa mkopo wenye kipengele cha lazima cha kumpatia mkataba wa kudumu katika dili lenye thamani ya pauni milioni 25. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Leeds imemruhusa mshambuliaji kutoka Suriname, Joel Piroe (27), kuelekea West Ham kwa ajili ya vipimo vya afya. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
AC Milan imefikia dili la pauni milioni 34 kumsajili winga wa Ubelgiji, Diego Moreira (22), kutoka Strasbourg. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Sao Paulo na West Ham ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia mshambuliaji wa zamani wa England, Jamie Vardy (39), ambaye kwa sasa ni mchezaji huru. (Talksport)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












