Moja kwa moja, Saba saba: Mamlaka Kenya, Tanzania zachukua tahadhari kukabiliana na tishio la maandamano
Hali ya ulinzi imeonekana kuimarishwa zaidi katika jiji kuu la kibiashara la Tanzania Dar es Salaam, huku mamia ya maafisa polisi na jeshi wakionekana kutanda katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Muhtasari
Mwanamfalme wa Uingereza ashindwa kesi katika Mahakama dhidi ya magazeti mawili
Kiongozi wa chama cha REFORM Uingereza ajiuzulu Ubunge
Mwanamfalme wa Uingereza ashindwa kesi katika Mahakama dhidi ya magazeti mawili
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mwanamfalme Harry
Duke
wa Sussex Mwanamfalme Harry na watu wengine sita wameshindwa kesi yao kuhusu faragha katika Mahakama
Kuu dhidi ya kampuni inayochapisha magazeti ya Daily Mail na Mail on Sunday
Kundi
hilo, ambalo linajumuisha Sir Elton John, Baroness Lawrence na Liz Hurley,
liliishtaki kampuni ya Associated Newspapers Limited (ANL) kwa madai ya
kukusanya taarifa kinyume cha sheria.
Katika
uamuzi wake, Jaji Nicklin amesema madai hayo ni mazito na yanahitaji ushahidi
zaidi wa kushawishi kabla ya kuthibitishwa - lakini walalamikaji walishindwa
kuyathibitisha.
Kesi
ya wiki moja ilishuhudia Mwanamfalme Harry akitoa ushahidi kuhusu makala alizozilalamikia
akisema kampuni hiyo imefanya maisha ya mkewe kuwa "maumivu makubwa."
Akijibu
uamuzi huo, ANL ambayo inachapisha magazeti hayo imesema ni "uthibitisho wa
uandishi wa habari wa Daily Mail."
Kiongozi wa chama cha REFORM Uingereza ajiuzulu Ubunge
Chanzo cha picha, Reform UK
Maelezo ya picha, Nigel Farage amejipatia umaarufu kwa sera zake za kupinga wahamiaji
Nigel
Farage anasema atajiuzulu kama Mbunge wa Clacton, jambo litakalosababisha
uchaguzi mdogo ambao anasema atashiriki kama mgombea.
"Huu
utakuwa uchaguzi mdogo wa wananchi dhidi ya mfumo uliopo madarakani," amesema
katika taarifa ya video, akiongeza kuwa "wananchi wa Clacton ndio
watakaohukumu matendo yangu."
Hatua
hii inakuja kufuatia mzozo kuhusu misaada ya kifedha aliyopokea, baada ya
gazeti la Sunday Times kuripoti kuwa hakutangaza manufaa ikiwemo wafanyakazi na
ulinzi aliyopata kutoka kwa mshirika wake wa muda mrefu, George Cottrell
"Sijafanya
kosa lolote," amesema, akisisitiza kuwa "hajavunja sheria hata
kidogo" huku akiikosoa vyombo vya habari kwa "kuisumbua na
kuishambulia" familia yake
Kiongozi
huyo wa chama cha Reform UK pia anakabiliwa na maswali kuhusu zawadi ya pauni
milioni 5 kutoka kwa mfadhili wa chama hicho, Christopher Harborne, mapema
mwaka 2024, fedha ambazo hakuzitangaza rasmi, akisema kuwa pesa hizo zilikuwa
kwa ajili ya usalama wake binafsi.
Maelezo ya picha, mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia Marine Le Pen.
Mahakama
ya Rufaa ya Paris, Ufaransa imeunga mkono hukumu ya kupatikana na hatia ya
ubadhirifu wa pesa dhidi ya mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia
Marine Le Pen.
Faini
ya Euro 100,000 (Pauni 74,700) kutokana na ubadhirifu wa pesa za Bunge la Ulaya
imethibitishwa pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela; miaka miwili
imesimamishwa na mwaka mmoja atautumikia akiwa amevaa kifaa cha kumfuatilia
mkononi.
Kwa hukumu hiyo Le Pen amesema hatagombea
urais katika uchaguzi wa urais wa Ufaransa wa 2027.
Amesema
kuwa muda wowote atakaokuwa amevaa kifaa hicho kitamzuia kufanya kampeni vizuri,
kwani itambidi kuomba ruhusa kila anapofanya mkutano wa kampeni.
Kwa
kupunguziwa muda ambao amepigwa marufuku kutoshika wadhifa wa umma hadi miezi
15 kutoka miezi 30 iliyobaki kati ya miezi 45, bado angeweza kugombea urais.
Desemba 2023 Le Pen na watu wengine zaidi ya 20 walishtakiwa,
wakituhumiwa kutumia vibaya fedha za bunge la Ulaya na mwezi Septemba 2024 kesi
ilianza na Le Pen akikana kosa lolote.
31 Machi 2025 Le Pen alipatikana na hatia na kupewa kifungo
cha miaka minne jela - ambapo miwili imesimamishwa na mingine miwili ataitumikia
akiwa na kifaa cha kumfuatilia bila ya kifungo cha gereza.
Le Pen alikana kile anachokielezea kama "uamuzi wa kisiasa" na
atakata rufaa dhidi ya marufuku hiyo
2026, kesi ilianza katika Mahakama ya Rufaa mwezi Januari na
kumalizika mwezi Februari, huku uamuzi wa rufaa ukitolewa leo.
Le
Pen ni mwanasiasa anayeongoza chama cha mrengo wa kulia National Rally (RN)
ambacho miongoni mwa sera zake maarufu ni kinapinga wahamiaji nchini Ufaransa.
Siku ya Saba saba: Hali ilivyokuwa jijini Nairobi kupitia picha
Chanzo cha picha, NMG
Chanzo cha picha, NMG
Chanzo cha picha, NMG
Polisi Tanzania yatoa taarifa hali ilivyo mchana wa siku ya Saba saba
Chanzo cha picha, getty images
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa taarifa inayoeleza
kuwa hali ni shwari katika nchi hiyo kufikia mchana wa tarehe 7 Julai, 2026 huku
likisema kuwa watu wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Taarifa ya Polisi inakuja baada ya kuenea kwa ripoti
katika mitandao ya kijamii kuwa kutakuwa na maandamano katika siku ya leo
ambayo ni siku ya mapumziko kupisha maonyesho ya kibiashara ya Sabasaba.
Taarifa ya Polisi ya wakati wa asubuhi ilieleza
kuwa hali ni shwari katika mkoa wa kibiashara wa Dar es Salaam, huku ulinzi
ukiwa umeimarishwa katika mikoa mengine yote ya Tanzania.
Kwa siku kadhaa sasa BBC imeshuhudia vikosi
vya usalama vyenye silaha na magari vikishika doria katika maeneo mbalimbali ya
nchi, huku doria hizo zikishika kasi katika siku ya leo.
Siku ya Saba Saba Kenya: Vijana wadai kukamatwa bila sababu na maafisa wa usalama
Chanzo cha picha, Francis Awino
Na Asha Juma,
Tarehe 7 Julai, inayojulikana kama Saba Saba inaadhimisha
maandamano ya kihistoria ya miaka ya 90 ya kuunga mkono demokrasia ambayo
yalishinikiza serikali kukomesha mfumo wa chama kimoja nchini Kenya.
Mashirika ya kiraia na wanaharakati hutumia siku hii
kuandamana kwa ajili ya haki za binadamu.
Asha Juma amezungumza na kiongozi wa vuguvugu la Mtetezi
linalotetea haki za raia, uchumi na uwajibikaji wa kijamii, Francis Awino
pamoja na vijana Nyanjom Joshua na Beatrice Chepkoech kuelezea kwa nini sikuu
hii inamaana gani.
"Sabasaba ni ya muhimu katika enzi yetu, kwa sababu hutuwezi
kuishi nchi ambayo haina chakula, maji ya kunywa n ahata masomo ni vigumu
kupata. Tunaonyesha serikali tunaanzisha mapambano, tutaendelea na mapambano
hadi Kenya iwe nchi ambayo kila mtu anafurahia kuishi," amesema Francis
Awino.
Vuguvugu hili linasema kila kinachobadilika kila mwaka ni matakwa
ya raia lakini hakuna tofauti kubwa ukilinganisha kilichojitokeza miaka ya
nyuma na sasa.
Awino anasema miongoni mwa matatizo yanayofanya vijana kuandamana
mitaani ni pamoja na kukosa ajira hata baada ya kuhitimu, kushikwa na maafisa
wa usalama bila bila sababu za msingi na mengineo. Bwana Awino ametoa mfano wa
maandamano ya kumbukumbu ya waliofariki wakidai kusitishwa kwa mswada wa Fedha
2024.
"Vijana walikamatwa na kupelekwa maeneo ambayo hawakuyafahamu.
Hayo pia tunayalilia na tutafanya hivyo hadi serikali ifuate katiba,"
amesema Awino.
Pia alizungumzia suala la maafisa wa usalama kuwajibishwa
kwa makosa wanayofanya na kushutumu mashirika husika kwa kutofanya kazi yao
ipasanyo.
"Huwa
tunawapelekea ushahidi kuwa afisa fulani amekiuka sheria lakini wanachofanya mara
nyingi ni kuchukua namba yako na kukuarifu kuwa watakupigia kisha hali
inaendelea kuwa hivyo. Haya mashirika hayafanya kazi wanayopaswa kufanya. wamelalia
kazi yao," Awino amesema.
Polisi imeimarisha vizuizi vya usalama kwenye barabara kuu
za Nairobi huku Wakenya wakiadhimisha Siku ya Saba Saba.
Polisi imesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kudumisha
usalama, amani na utulivu wakati wa maadhimisho ya kila mwaka ya Saba Saba.
Maafisa wa polisi tisa wauawa katika shambulio Pakistan
Chanzo cha picha, EPA
Maafisa tisa wa polisi wameuawa, na kadhaa hawajulikani walipo, baada ya
shambulio la watu wenye silaha katika jimbo la Balochistan kusini-magharibi mwa
Pakistan, afisa mmoja wa serikali ya mtaa ameiambia BBC Urdu.
Naibu Kamishna Abdul Quddus Achakzai amesema washambuliaji hao
waliwafyatulia risasi polisi waliokuwa wakilinda eneo la ujenzi wa bwawa la
mabilioni ya rupia katika wilaya ya Ziarat.
Maafisa wawili wakuu ni miongoni mwa waliouawa, na operesheni ya
utafutaji inaendelea ili kuwapata waliopotea, aliongeza.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo. Maafisa wa
Balochistan walisema vikosi vya usalama viliwaua wanachama 15 wa Kundi la
Taliban wa Pakistani (TPP) kama sehemu ya "operesheni" huko Ziarat.
Maandamano dhidi ya shambulio dhidi ya polisi yamekuwa yakifanyika kando
ya barabara kuu karibu na eneo la tukio.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistani Mohsin Naqvi amelaani shambulio
hilo, akisema maafisa waliouawa ni "fahari ya taifa letu".
Maafisa wanasema walikuwa wakilinda eneo la ujenzi wa Bwawa la Mangi,
ambalo linajengwa ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa maji unaokabili mji mkuu
wa Balochistan wa Quetta.
Mkoa huo, unaopakana na Afghanistan na Iran, umeshuhudia machafuko kwa
miongo kadhaa, huku makundi ya wanamgambo wa eneo hilo yakidai uhuru kutoka serikali
ya Pakistani.
Mwezi Mei, maafisa wa eneo hilo walisema kundi linalotaka kujitenga la Jeshi
la Ukombozi la Balochistan lilikuwa nyuma ya shambulio kwenye treni
iliyokuwa ikisafirisha wanajeshi, na kuuwa watu 20.
Ghana yamkatalia Rais wa Afrika Kusini kufanya ziara
Chanzo cha picha, getty images
Maelezo ya picha, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Vyombo vya habari vya Ghana vimeripotiwa kuwa nchi
hiyo ya Afrika Magharibi imekataa ombi la ziara ya kitaifa ya Rais wa Afrika
Kusini Cyril Ramaphosa.
Gazeti la Ghana Business News limeripoti kwamba
ziara iliyopangwa kufanyika Agosti 2 hadi 4 imekataliwa na Ghana, huku Ghana
ikitaja mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni na chuki dhidi ya Waafrika nchini
Afrika Kusini kuwa ndio sababu.
Kulingana na maafisa wa Ghana waliozungumza na
shirika la habari la Ujerumani la DW, uamuzi huo unakuja huku mvutano
ukiendelea kushuhudiwa kuhusu ghasia za hivi karibuni za chuki dhidi ya wageni
nchini Afrika Kusini.
Vyanzo ndani ya serikali ya Ghana vinasema
ziara iliyopangwa, ambayo ilitarajiwa kufanyika mapema Agosti, ilikataliwa ili
kuepuka uwezekano wa umma na maandamano nchini Ghana huku hisia kuhusu suala
hilo zikiendelea kuwa kubwa.
Inaripotiwa kuwa Accra imeitaka Pretoria
kuchukua hatua madhubuti kushughulikia mashambulizi hayo na kuhakikisha ulinzi
wa raia wa kigeni kabla ya ziara yoyote ya ngazi ya juu kutokea.
Waziri Mkuu wa Ethiopia awatuhumu wapiganaji wa Tigray kushiriki vita Sudan
Chanzo cha picha, addisstandard
Akilihutubia
bunge la Ethiopia tarehe 7 Julai 2026, Waziri Mkuu Abiy Ahmed amewatuhumu
wapiganaji wa Tigray kwa kupeleka wapiganaji kushiriki katika vita vya Sudan. Amedai
vijana kutoka Tigray wanalazimishwa kujiunga na vita hivyo.
"Vijana
wengi kutoka Tigray wamelazimishwa kupigana katika vita vya Sudan. Vijana wa
Tigray wanapoteza maisha yao kwa sababu wasizozijua. Wanauzwa utumwani katika
vita vya Sudan, na kupoteza maisha kwa ajili ya jambo wasilolifahamu," amesema
Abiy.
Ethiopia
yenyewe imetuhumiwa na Sudan kwa kushiriki katika vita hivyo ikishirikiana na
Falme za Kiarabu (UAE). Sudan inadai Ethiopia na UAE zilifanya shambulio la
ndege isiyo na rubani (droni) katika uwanja wa ndege wa Khartoum.
Kwa
upande wake, Ethiopia imeituhumu Sudan kwa kuhifadhi makundi yanayopinga
Ethiopia na kutoa silaha pamoja na msaada wa kifedha kwa wapiganaji wa TPLF.
Hapo
awali, Ethiopia iliituhumu TPLF na serikali ya Eritrea kwa kushirikiana
kuanzisha vita dhidi ya Ethiopia. Katika hotuba yake bungeni leo, Abiy amepuuza
ushirikiano huo, akisema: "Hata kama serikali ya Eritrea, TPLF na Sudan
zitashirikiana, hakuna tishio kwa Ethiopia."
Kauli
hizo zinakuja huku kukiwa na ongezeko la mvutano kati ya serikali kuu na TPLF
katika eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia. Leo, Waziri Mkuu amewatuhumu
wapiganaji wa Tigray kwa kuichokoza serikali kuu. "Kila siku vitendo vya
uchokozi vinavyoweza kusababisha vita hufanywa na vikosi katika eneo la Tigray,
mara kwa mara," aliwaambia wabunge.
Hivi
karibuni, Umoja wa Ulaya ulionyesha wasiwasi, ukionya kuwa hali inayoendelea
katika eneo la Tigray inaweza kudhoofisha Makubaliano ya Pretoria ya mwaka
2022, ambayo yalihitimisha vita vya Tigray vilivyodumu kwa miaka miwili.
Mchezaji wa Mamelodi raia wa Zimbabwe anusurika risasi Afrika Kusini
Chanzo cha picha, ISI Photos via Getty Images
Maelezo ya picha, Divine Lunga
Polisi wa Afrika Kusini wamesema mchezaji wa mpira wa miguu wa Zimbabwe
Divine Lunga amenusurika shambulio la risasi huko Johannesburg.
Nyota huyo wa mpira wa miguu, mwenye umri wa miaka 31, alikuwa
akiendesha gari katika kitongoji cha jiji la Hillbrow siku ya Jumapili wakati
gari lake lilipopigwa risasi na mtu asiyejulikana mwenye bunduki, kulingana na
ripoti.
Lunga, anayechezea timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zimbabwe na klabu ya
Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns, alikimbia bila kujeruhiwa.
Uhalifu wa kutumia bunduki ni tatizo kubwa nchini Afrika Kusini, ikiwa na
mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani.
Msemaji wa polisi Kapteni Tintswalo Sibeko amesema wanachunguza jaribio
la mauaji lakini hakuna mtu aliyekamatwa.
Hakutoa maelezo zaidi, lakini gazeti la The Citizen la Afrika Kusini limesema
Lunga alikuwa njiani kuelekea kanisani na kaka yake mdogo waliposhambuliwa.
Mbappe alaani matamshi ya kibaguzi ya Seneta wa Paraguay
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kylian Mbappe alifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Senegal, Iraq na Sweden kabla ya penalti yake dhidi ya Paraguay.
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe amemlaani Seneta wa Paraguay kama
"mtu asiye na maana" na asiyestahili wadhifa wake baada ya kutoa
matamshi kadhaa ya kibaguzi akidhihaki asili na elimu yake.
Celeste Amarilla, wa Chama cha Liberal Radical Party cha Paraguay,
alichapisha maoni kwenye X baada ya nchi yake kushindwa na Ufaransa katika
hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.
Mbappe alimjibu, "Madam Celeste Amarilla, wewe ni
mwanamke usiya na maana na usiyestahili wadhifa wako."
"Huiwakilishi Paraguay, nchi ambayo ni nzuri na ya heshima katika
mashindano yote."
"Kupitia uzembe wako na ubaguzi wako wa rangi, dunia nzima tayari
imesahau safari na juhudi za kihistoria ambazo wachezaji wako walifanya wakati
wa Kombe la Dunia, na kumpa nafasi mwanamke asiye na uwezo ambaye anatoa
taswira mbaya zaidi ya nchi yake."
"Sitawaruhusu watu kama yeye kueneza chuki na ubaguzi wa rangi
duniani kote."
Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) limetangaza mipango ya kuwasilisha
mashtaka ya jinai, likielezea matamshi ya Amarilla kama "ya kuchukiza
kabisa na yasiyokubalika".
Katika taarifa, FFF imesema: "Matamshi haya ni ya jinai na yana
hatia. Lazima yashtakiwe hapa kama mahali pengine popote. FFF inaripoti suala
hilo kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwa lengo la kesi za kisheria.
Serikali ya Paraguay imesema "inalaani na kukataa kauli"
zilizotolewa na Amarilla, ikisema "zinapingana na maadili na kanuni
zinazohimiza kuishi kwa amani na heshima."
Mbappe alifunga penalti ya ushindi katika kipindi cha
pili cha mchezo wa Jumamosi, na hivyo kufanikiwa kwenda robo fainali dhidi ya
Morocco jiji Boston siku ya Alhamisi.
Akiwa na mabao saba, Mbappe ndiye mfungaji bora wa pamoja katika
mashindano ya mwaka huu, sawa na Lionel Messi wa Argentina na Erling Haaland wa
Norway.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliandika: "Goli jingine kwa
Kylian Mbappe. Dhidi ya ubaguzi wa rangi wakati huu. Namuunga mkono kwa kila
kitu."
Matamshi ya Amarilla yamekuja baada ya yale ya kipa wa zamani wa
Paraguay Jose Luis Chilavert, ambaye alisema kuelekea mechi hiyo kwamba timu
yake ya taifa itacheza na "kikosi kutoka Afrika".
Matamshi hayo pia yalisababisha jibu kutoka kwa rais wa FFF Philippe
Diallo, ambaye alisema Chilavert "anatia aibu".
"Ninalaani kwa nguvu zote matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Jose
Luis Chilavert dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa, ambayo yanadhoofisha maadili
na heshima, udugu, na utofauti katika soka letu," Diallo alisema.
"Kama alikuwa kipa mzuri hapo awali, mtu huyu sasa amegeuka kuwa
fedheha."
Polisi wakamata baadhi ya wanaharakati katika maandamano ya Saba saba Kenya
Chanzo cha picha, NMG
Baadhi ya wanaharakati waliokuwa wameanza kufanya maandamano
katika barabara ya Harambee Avenue wamekamatwa na maafisa wa polisi waliokuwa na
mavazi ya raia.
Chanzo cha picha, NMG
Mwanaharakati huyu amekamatwa katika barabara ya Biashara nchini Kenya.
Chanzo cha picha, NMG
Hata hivyo, katika maeneo kama Githurai hali imeanza kurejea kuwa kawaida.
Raia wameanza kujitokeza katika shughuli zao za kila siku tofauti ilivyokuwa na asubuhi ambapo ukimya ulitanda huku barabara zikiwekewa vizuizi na kusalia mahame.
Milipuko yajeruhi 18 Syria wakati rais wa Ufaransa akifanya ziara
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Video na picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wafanyakazi wa huduma za dharura karibu na miali ya moto na uharibifu unaosababishwa na milipuko hiyo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yuko salama baada ya watu kadhaa
kujeruhiwa katika milipuko iliyoripotiwa karibu na hoteli aliyokuwa amefikilia
katikati mwa Damascus, imesema Ikulu
ya Elysee.
Chanzo cha usalama kimeiambia BBC milipuko hiyo ilisababishwa na
vilipuzi viwili na watu kadhaa wamejeruhiwa. Vyombo vya habari vya Syria vimesema
watu 18, wakiwemo maafisa wanne wa polisi, wamejeruhiwa.
Macron yuko Damascus kwa mazungumzo na mwenzake wa Syria Ahmed al-Sharaa
katika ikulu ya rais.
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Maafisa wa Macron wanasema rais wa Ufaransa hakusikia milipuko yoyote alipokuwa akielekea kukutana na kiongozi wa Syria Ahmed al-Sharaa
Baada ya kumaliza ziara ya Syria, Macron anatarajiwa kuelekea Uturuki kwa mkutano wa kilele wa Nato. Ziara hiyo "inaendelea kama ilivyopangwa", kulingana na Ikulu ya Elysee.
Baada ya ripoti za mlipuko, video na picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha moshi na miali ya moto ikitoka kwenye gari karibu na hoteli katika mji mkuu wa Syria.
BBC Verify imechambua video za milipuko hiyo, ambayo inaonyesha milipuko imetokea takriban mita 125 kutoka hoteli ya Four Seasons, kwenye barabara ya Shoukry al-Quowatly.
Kuwasili Syria Jumatatu jioni, Macron amekua kiongozi wa kwanza wa EU kutembelea nchi hiyo tangu kuanguka kwa utawala wa miaka 24 wa Bashar al-Assad.
Mwanzoni mwa Julai, mlipuko wa bomu katika mgahawa uliojaa watu katikati mwa Damascus, uliwaua watu wasiopungua tisa na kuwajeruhi wengine 22, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Syria.
Polisi Tanzania yasema hali ni shwari asubuhi ya siku ya Saba saba
Chanzo cha picha, mitandao
Maelezo ya picha, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania ni Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Alphonce Misime
Polisi nchini Tanzania imesema hali ya usalama
ni shwari katika jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo huku maonyesho ya Saba saba yakifanya wakati kukiwa na wasiwasi wa kutokea maandamano ya nchi nzima.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania
ni Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Alphonce Misime amesema hali ya
usalama katika viwanja vya Sabasaba na jiji la Dar es Salaam imeimarishwa huku
jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama vikiwatoa hofu wananchi wanaofika
katika viwanja hivyo.
“Niwaambie wananchi walipo majumbani,
wasiogope kuja katika viwanja vya Sabasaba kwani hali ni shwari, hali ni salama,
kuanzia kwenye mitaa ambayo watatoka kuja katika viwanja hivi, ulinzi umeimarishwa,
wasiogope waje,” Misime amesema.
Akizungumza kutoka katika viwanja vya Sabasaba
jiji Dar es Salaam, Misime ameeleza kuwa Jeshi la polisi limeimarisha usalama
katika maeneo yote ya nchi.
Kwa siku kadhaa sasa BBC imeshuhudia askari
wenye silaha za moto na magari wakiwa wametanda katika maeneo mbalimbali ya jiji
la Dar es Salaam baada ya taarifa za uwepo wa maandamano siku ya Sabasaba kusambazwa katika mitandao ya kijamii.
China yahukumu afisa wa zamani kifo kwa kupokea rushwa ya dola milioni 325
Chanzo cha picha, CCTV
Mahakama moja mashariki mwa China imemhukumu kifo aliyekuwa afisa wa jiji kwa kupokea rushwa ya zaidi ya yuan bilioni 2.2 (takriban dola za Marekani milioni 325) katika kipindi cha miaka 30.
Yang Youlin, ambaye alihudumu katika nyadhifa mbalimbali katika jiji la Nanjing kuanzia mwaka 1993 hadi 2023, pia alipatikana na hatia ya ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji wa fedha.
Kiasi cha mali alichopatikana nacho kwa njia haramu ni miongoni mwa vikubwa zaidi vilivyowahi kurekodiwa katika miaka ya karibuni.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Yang mwenye umri wa miaka 69 alitumia nafasi zake kuwasaidia watu kupata zabuni za ujenzi, uhamishaji wa ardhi na ufadhili wa miradi kwa kubadilishana na fedha na vitu vya thamani.
Yang alichunguzwa katika kampeni ya Rais Xi Jinping ya kupambana na rushwa, ambayo imewakumba maafisa wa jeshi, sekta ya benki na maeneo mengine ya ngazi za juu.
Mahakama ya mji wa Changzhou ilisema Jumatatu kuwa Yang alitenda makosa "ya kiwango cha juu sana" ambayo "yalisababisha hasara kubwa kwa maslahi ya taifa na wananchi."
Tangu aingie madarakani, Rais Xi Jinping ameanzisha kampeni kadhaa za kupambana na rushwa. Hata hivyo, wakosoaji wanasema kampeni hizo pia zimetumika kuwaondoa wapinzani wa kisiasa.
Hukumu za kifo kwa makosa ya kifedha na rushwa hutolewa mara chache nchini China, lakini zinaweza kutolewa pale ambapo kesi zinahusisha kiasi kikubwa cha fedha, kwa kawaida kinachozidi yuan bilioni moja.
Kwa mfano, mwaka 2021 aliyekuwa mkuu wa kampuni ya usimamizi wa mali za kifedha, Lai Xiaomin, alinyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya yuan bilioni 1.8 katika kipindi cha miaka 10.
Mahakama nchini China pia zimewahi kupunguza adhabu katika baadhi ya kesi ambapo waliohukumiwa walitoa taarifa zilizosaidia kufichua wahalifu wengine.
Hata hivyo, ingawa Yang pia alishirikiana na mamlaka kwa kutoa taarifa kama hizo, Mahakama ya Changzhou ilisema makosa yake yalikuwa "makubwa sana" kiasi kwamba ushirikiano wake "haukutosha kustahili kupunguziwa adhabu."
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Yang alikiri makosa yote yaliyokuwa yakimkabili na "alionesha majuto katika kauli yake ya mwisho" mbele ya mahakama.
Zaidi ya watu 1,000 wakamatwa katika operesheni ya kimataifa dhidi ya biashara haramu ya binadamu
Chanzo cha picha, Interpol
Zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa katika operesheni ya kimataifa dhidi ya biashara haramu ya binadamu iliyofanyika katika nchi 59.
Operesheni hiyo, iliyoratibiwa na Interpol na kujulikana kama Operation Global Chain, iliwalenga wahusika wa biashara haramu ya binadamu kwa madhumuni ya unyonyaji wa kingono, ajira za kulazimishwa, uhalifu wa kulazimishwa na kuwalazimisha watu kuombaomba.
Kwa mujibu wa mamlaka, mtandao uliokuwa ukiwasafirisha waathiriwa kwenda Cambodia kwa ajili ya ulaghai wa mtandaoni ulivunjwa, pamoja na mtandao mwingine uliokuwa ukiwalazimisha wasichana wenye umri mdogo waliopatikana kupitia mitandao ya kijamii kujiingiza katika biashara ya ngono barani Ulaya.
Kwa jumla, waathiriwa 2,070 au watu wanaoshukiwa kuwa waathiriwa walitambuliwa, wengi wao wakiwa wanawake. Kati ya waliokamatwa, watu 334 wanakabiliwa na tuhuma za biashara haramu ya binadamu, huku 690 wakikabiliwa na makosa mengine yanayohusiana na uhalifu huo.
Interpol, ambayo iliratibu operesheni hiyo kwa kushirikiana na Europol na Shirika la Ulaya la Kulinda Mipaka (Frontex), ilisema matokeo ya operesheni hiyo yamebaini njia na mbinu mpya zinazotumiwa na mitandao ya biashara haramu ya binadamu.
Operesheni hiyo iligundua mwenendo mpya ambapo waathiriwa kutoka Amerika ya Kusini wanasafirishwa kwenda Ulaya kwa ajili ya kazi za kulazimishwa. Takribani asilimia 10 ya waathiriwa waliotambuliwa walikuwa watoto kutoka bara la Amerika waliolazimishwa kufanyiwa unyonyaji wa kingono.
Katika hatua nyingine, mamlaka nchini Colombia zilianzisha kampeni ya uhamasishaji katika viwanja vya ndege ili kuwaonya wasafiri kuhusu hatari ya matangazo ya ajira za ulaghai nje ya nchi.
Interpol pia ilisema Polisi wa Brazil walitambua waathiriwa 406, raia 83 wa Brazil na raia 323 wa kigeni, waliokuwa sehemu ya mtandao wa kimataifa uliokuwa ukiwasafirisha watu kwenda Cambodia, ambako walilazimishwa kushiriki katika ulaghai wa mtandaoni.
‘Maandamano Saba saba’: Ulinzi mkali waendelea Dar Es Salaam
Maelezo ya picha, Polisi wakiimarisha ulinzi (Picha maktaba)
Hali ya ulinzi imeonekana kuimarishwa zaidi katika jiji kuu la kibiashara la Tanzania Dar es Salaam, huku mamia ya maafisa polisi na jeshi wakionekana kutanda katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Hatua hii inafuatia wito wa maandamano kutoka kwa baadhi ya wanaharakati wa mitandaoni, wakidai mabadiliko na uwajibikaji kwa serikali.
BBC imeshuhudia doria za vyombo vya usalama katika maeneo mbali mbali ya jiji hilo.
Hata hivyo, maafisa hao hawajaweka vizuizi vya barabarani na wananchi wapo huru kuendelea na shughuli zai za kawaida. Hata hivyo kuna idadi ndogo ya magari na watu barabarani, leo ikiwa ni sikukuu nchini humo.
BBC imeshuhudia uwepo wa maafisa usalama waliojihami kwa silaha makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Sam Nujoma eneo la Mwenge na Makutano ya Ali Hassan Mwinyi n Barabara ya Kawawa/Mwai Kibaki eneo la Kinondoni Morocco.
BBC pia imeshuhudia uwepo wa Askari wenye silaha katika vituo vingi vya mabasi ya mwendokasi jijini humo. Maafisa hao pia wameonekana katikati ya jiji eneo la Posta ambapo walikuwa wamejihami na gari ambayo humwaga maji ya kuwasha.
Kumeshuhudiwa ulinzi mkali pia katikati njia za kuingia katika bandari kuu ya Dar Es Salaam pamoja na eneo la bandari lenye maghala ya kuhifadhia mafuta upande wa Kigamboni.
Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo duru zinzonesha kuwa hofu ya ghasia na kumbukumbu za mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi wa Oktoba mwaka jana pamoja na kushindikana kwa maandamano yaliyoitishea Desemba 9 mwaka jana huenda kukapungunga matarajio ya kufanyika kwa maandamano hayo siku ya leo.
Makundi kadhaa ya haki za binadamu na upinzani yanasema maelfu ya watu waliuawa katika machafuko yaliyotokana na uchaguzi wa Oktoba 2025, huku takwimu rasmi za serikali zikisema ni takribani watu 500 ndio waliofariki.
Siku ya Saba Saba: Polisi waweka vizuizi vya usalama kote jijini Nairobi
Polisi imeimarisha vizuizi vya usalama kwenye barabara kuu za Nairobi huku Wakenya wakiadhimisha Siku ya Saba Saba.
Polisi imesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kudumisha usalama, amani na utulivu wakati wa maadhimisho ya kila mwaka ya Saba Saba. The Star imeripoti
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, Msemaji wa Polisi, Michael Muchiri, alisema hatua za kuimarisha usalama zimechukuliwa kutokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo baadhi ya maandamano yaligeuka kuwa ya vurugu, na kusababisha uvunjifu wa amani pamoja na kuvurugika kwa shughuli za kawaida za biashara.
“Huduma ya Kitaifa ya Polisi inapenda kuwafahamisha wananchi wote kwamba, kutokana na yaliyoshuhudiwa wakati wa maadhimisho ya Saba Saba katika miaka iliyopita, baadhi ya watu wamehusika katika vitendo vya kuvunja amani, jambo lililoathiri shughuli za kawaida za wale ambao hawashiriki maandamano,” ilisema taarifa hiyo.
Muchiri alisema vizuizi hivyo vinatumika kudhibiti mienendo ya watembea kwa miguu na magari ndani ya jiji, huku polisi wakilenga kuzuia vurugu na kuhakikisha usalama wa umma.
Ripoti zinaonesha kuwa maafisa wa polisi wamepelekwa katika maeneo mbalimbali ya Nairobi na miji mikuu kama Kitengela, Mlolongo, Rongai, Githurai, Waiyaki Way na maeneo mengine.
Baadhi ya sehemu za katikati mwa jiji la Nairobi zimetangazwa kuwa maeneo yasiyoruhusiwa kufikiwa.
Muchiri aliwataka wananchi kushirikiana na maafisa wa polisi na kufuata maelekezo ya usalama ili kusaidia kudumisha amani na utulivu siku nzima.
Polisi pia wameonya kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo visivyo halali atachukuliwa hatua za kisheria.
Maadhimisho ya Saba Saba, yanayofanyika kila mwaka tarehe 7 Julai, yamekuwa yakihusishwa kihistoria na maandamano yanayodai mageuzi ya kisiasa na kiutawala, huku mamlaka mara nyingi zikiongeza idadi ya maafisa wa usalama kwa matarajio ya mikusanyiko mikubwa ya watu.
Safari ya Ronaldo katika Kombe la Dunia yafikia mwisho kwa machozi
Mmoja wa wasakata kabumbu mahiri kuwahi kutokea duniani Cristian Ronaldo wa Ureno amelazimika kuimaliza kazi yake bila kutwaa tuzo kubwa zaidi duniani baada ya mechi yake ya mwisho kwa Ureno kumalizika kwa kushindwa 1-0 na Hispania katika hatua ya 16 bora.
Ronaldo alibubujikwa machozi huku hadithi yake ya Kombe la Dunia ikimalizika jijini Dallas baada ya kushuhudia goli la dakika za majeruhi la Mikel Merino likiwapa majirani zao nafasi ya kutinga robo fainali.
Mshindi huyo wa Ballon d'Or mara tano, mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tano na bingwa wa Euro 2016 mwenye umri wa miaka 41, ana rekodi ya dunia ya kufunga mabao 976 kwa vilabu na nchi yake.
Amefunga mabao sita kwa rekodi ya Kombe la Dunia. Lakini ushindi wake wa karibu zaidi ya kombe la dunia ni wakati Ureno ilipocheza nusu fainali katika fainali zake za kwanza mwaka 2006 huko Ujerumani.
Leo usiku ni Misri dhidi ya Argentina na Uswisi ikicheza na Colombia kukamilisha hatua ya 16 bora.
Zelensky kuishinikiza NATO kuipatia Ukraine mifumo ya ulinzi wa anga baada ya mashambulizi makali ya Urusi
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Ukraine anapanga kutumia mkutano wa NATO nchini Uturuki kuwahimiza washirika wa Kyiv kuipatia mifumo ya ulinzi wa anga inayohitaji kwa dharura ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi yanayozidi kuongezeka.
Wito wa Volodymyr Zelensky wa kuomba msaada umeongezeka uzito baada ya makombora ya Urusi kushambulia mji mkuu wa Ukraine mara mbili ndani ya kipindi kisichozidi wiki moja, yakipiga majengo ya makazi na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 50.
Mkutano huo mjini Ankara pia utampa Zelensky fursa ya kukutana na Donald Trump katika mazungumzo muhimu na kusisitiza hoja yake kwamba mashambulizi ya "kikatili" ya Urusi yanaonesha udhaifu badala ya nguvu, na kwamba Vladimir Putin anapaswa kushinikizwa kuingia katika mazungumzo yatakayolenga kufikia amani yenye "heshima."
Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Ukraine yanakuja wakati nchi hiyo imekuwa ikiongeza mashambulizi yake ya masafa marefu kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya Urusi, ikilenga viwanda vya kusafisha mafuta na maeneo ya kijeshi, hali iliyosababisha upungufu mkubwa wa mafuta na kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Urusi.