Mahakama ya Ufaransa yaunga mkono hukumu dhidi ya Marine Le Pen

Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images
Mahakama ya Rufaa ya Paris, Ufaransa imeunga mkono hukumu ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa pesa dhidi ya mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia Marine Le Pen.
Faini ya Euro 100,000 (Pauni 74,700) kutokana na ubadhirifu wa pesa za Bunge la Ulaya imethibitishwa pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela; miaka miwili imesimamishwa na mwaka mmoja atautumikia akiwa amevaa kifaa cha kumfuatilia mkononi.
Kwa hukumu hiyo Le Pen amesema hatagombea urais katika uchaguzi wa urais wa Ufaransa wa 2027.
Amesema kuwa muda wowote atakaokuwa amevaa kifaa hicho kitamzuia kufanya kampeni vizuri, kwani itambidi kuomba ruhusa kila anapofanya mkutano wa kampeni.
Kwa kupunguziwa muda ambao amepigwa marufuku kutoshika wadhifa wa umma hadi miezi 15 kutoka miezi 30 iliyobaki kati ya miezi 45, bado angeweza kugombea urais.
Desemba 2023 Le Pen na watu wengine zaidi ya 20 walishtakiwa, wakituhumiwa kutumia vibaya fedha za bunge la Ulaya na mwezi Septemba 2024 kesi ilianza na Le Pen akikana kosa lolote.
31 Machi 2025 Le Pen alipatikana na hatia na kupewa kifungo cha miaka minne jela - ambapo miwili imesimamishwa na mingine miwili ataitumikia akiwa na kifaa cha kumfuatilia bila ya kifungo cha gereza.
Le Pen alikana kile anachokielezea kama "uamuzi wa kisiasa" na atakata rufaa dhidi ya marufuku hiyo
2026, kesi ilianza katika Mahakama ya Rufaa mwezi Januari na kumalizika mwezi Februari, huku uamuzi wa rufaa ukitolewa leo.
Le Pen ni mwanasiasa anayeongoza chama cha mrengo wa kulia National Rally (RN) ambacho miongoni mwa sera zake maarufu ni kinapinga wahamiaji nchini Ufaransa.













































