Moja kwa moja, Trump asema mazungumzo ya Doha ni muhimu huku Iran ikisema hakuna mkutano uliopangwa

Marekani na Iran zatofautiana kuhusu mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika leo Doha

Muhtasari

Trump asema mazungumzo ya Doha ni muhimu huku Iran ikisema hakuna mkutano uliopangwa

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Morocco yatinga 16 bora kwa penalti

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Michuano ya Kombe la dunia imeendelea kushuhudia matokeo ya kushtua baada ya Morocco kutinga hatua ya 16 bora kwa kuiondoa Uholanzi kwa mikwaju ya penati kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu hadi baada ya dakika 120.

    Morocco sasa imeungana na Brazil, Canada na Paraguay katika hatua ya 16 bora, ikivunja rekodi ya Uholanzi ya kutofungwa na timu ya Afrika katika michuano hiyo.

    Katika mechi nyingine ya kusisimua, mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa na Paraguay kwa mikwaju ya penati 4-3, kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu hadi mwisho wa dakika 120.

    Ujerumani haikuwahi kupoteza mechi kwa penati kwenye kombe la dunia.

    Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz, pamoja na mshambuliaji wa Newcastle United, Nick Woltemade, walikosa penati zao baada ya kudakwa na kipa wa Paraguay, Orlando Gill.

    Maelezo zaidi:

  2. Trump asema mazungumzo ya Doha ni muhimu huku Iran ikisema hakuna mkutano uliopangwa

    g

    Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mazungumzo mapya kati ya wawakilishi wa Marekani na Iran mjini Doha, akisema kuwa mazungumzo hayo "yanaweza kuwa muhimu".

    Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa mazungumzo katika siku za karibu, ikisema safari ya wawakilishi wake kwenda Doha inalenga kufuatilia kuachiwa kwa mali za Iran zilizogandishwa.

    Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema dola bilioni sita kati ya dola bilioni 12 za mali za Iran zilizogandishwa zitaachiliwa na hivi karibuni zitapatikana kwa serikali.

    Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu kauli za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kusisitiza kwamba shughuli za kuondoa mabomu ya baharini katika Mlango wa Hormuz zitafanywa na Iran pekee.

    Maelezo zaidi:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 30/06/2026.