Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Marekani na Iran wako karibu kumaliza vita?
Ripoti zinaashiria kuwa, Marekani na Iran wanakaribia kukubaliana kumaliza vita.
Kulingana na gazeti la Marekani la Axios, ikulu ya White House imedokeza kuwa iko karibu kuafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kulingana na ripoti hiyo, pendekezo la White House ni ukurusa mmoja wenye hoja 14.
Baadhi ya matakwa ni Iran kusitisha mradi wa nyuklia, kuondoa vikwazo na kufungua mlango bahari wa Hormuz.
Mradi wa nyuklia na kufungua mlango bahari wa Hormuz, ni masuala ambayo mataifa hayo mawili yamekuwa yakitofautiana pakubwa.
Kulingana na gazeti la Axios, pendekezo hilo la Marekani lina masharti yatakayochochea kumalizika kwa vita.
Ripoti hiyo pia inasema Marekani inatarajia kupata majibu kutoka kwa Iran chini ya saa 48 ila bado inaendeleza kizuizi katika bandari za Iran.
Trump adokeza kuafikia makubaliano
Ebrahim Rezaei, msemaji wa baraza la usalama katika bunge la Iran kuwa "matamanio"
Rezaei alisema kuwa "wako macho na tayari" iwapo Marekani itakataa makubaliano hayo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa Iran, Ismail Bakei, aliiambia shirika la habari la ISNA kwamba pendekezo la Marekani la kumaliza vita bado "linazingatiwa."
Bakei alisema kuwa Iran iliwasilisha maoni yake kuhusu pendekezo hilo la Marekani kupitia wapatanishi wa Pakistan.
Aidha kupitia mtandao wa X Bakei alisema kuwa "Mazungumzo yanahitaji angalau jitihada za kweli ili kutatua mzozo."
"Mazungumzo yanahitaji nia njema, hii ina maana kwamba mazungumzo hayamaanishi mabishano, kulazimisha, udanganyifu, usaliti au kutumia nguvu," aliongezea.
Watalaam wanasemaje?
Watalaam wanasema kuwa makubaliano yoyote ya kumaliza vita huwa vigumu kuafikiwa, na huhitaji mchakato mrefu haswa ikija katika suala la mradi wa nyuklia wa Iran.
Mwanahabari wa Ikulu ya White House Bernd Debusmann pamoja na Holly Dagres mtaalam wa sera , anasema utawala wa Trump hautaridhika na makubaliano yoyote iwapo suala la mradi wa nyuklia hautaangaziwa kikamilifu.
Kuna mashaka pia iwapo kusitisha "Freedom Project" na kuruhusu uhuru wa usafiri wa majini katika mlango bahari wa Hormuz kutachochea makubaliano kuafikiwa haraka.
Afisa mwandamizi wa zamani wa Pentagon aliiambia BBC kwamba, "Iwapo Mkataba huu wa Maelewano utaafikiwa, utahakikisha kuachiliwa kwa meli zilizozuiliwa na itakuwa hatua kubwa katika kumaliza vita hivi."
"Ikiwa hautaafikiwa, unaweza kuipa Iran ujasiri zaidi."
Hayo yakijiri, kituo cha kuendesha oparesheni za kijeshi cha Marekani CENTCOM kilitangaza kuwa ilifyatua risasi dhidi ya meli moja wa kubeba mafuta ya Iran katika Ghuba ya Oman, na kufanya meli hiyo kushindwa kuendelea na safari yake
Jeshi la Marekani lilisema katika chapisho la mitandao ya kijamii kwamba meli ya mafuta ya M/T Hasna ilikuwa ikijaribu kuelekea bandari ya Iran licha ya vizuizi vya Marekani.