Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Glasi moja ya bia inaweza kuimarisha afya ya ubongo na kuongeza vitamini mwilini - utafiti
Kunywa kileo aina ya bia "kuna uwezo mkubwa" wa kuongeza afya ya akili yako, kulingana na utafiti
Vitamini ya B6 ni nzuri kwa afya ya akili, damu na kinga ya mwili na hupatikana katika vyakula tofauti.
"Glasi moja ya bia inaweza kupa 15% ya vitamini B6 ambayo mwili huhitaji. Pombe pia ambazo hazina vileo huwa na manufaa ya vitamini B6.
Viambato ambavyo hutumika kutengeneza bia ni kama vile shayiri,ngano na hamira.
Zote hizi zina vitamini B6.
Vitamini B6 ni kiambato muhimu ambacho tunapata kutoka kwa chakula, haswa nyama,samaki, viazi na unga wa shayiri.
Ni vigumu sana kwa mtu kuwa na upungufu wa vitamin B6.Ila wakati mwingine viwango hivyo hushuka pamoja na vitamini zingine kama za B12, ambayo huleta uchovu na uoga.
Vitamini B6 kwenye bia
Utafiti uliofanywa hivi karibuni ulifanya majaribio wa bia tofauti nchini Ujerumani na kugundua kuwa
- Bia aina ya Bock ilikuwa na kiwango cha juu cha vitamini B6 na pia vitamini hio ilipatikana kwa bia aina ya Lager,dark lager na bia ya ngano.
- Pombe ya mchele pia ilikuwa na vitamini B6.
- Baada ya kiungo cha ethanol kuondolewa kwa pombe ambazo hazina vileo, bia hizo zilisalia na viwango vya juu vya vitamini B6 kutokana na mkoroganyo wa kutengeneza pombe ambao ulikuwa wa juu kuliko bia za hamira.
- Kiwango cha wastani cha bia katika utafiti huu kilitoa asilimia 20 ya kiwango kinachopendekezwa cha vitamini B6.
- Bia isiyo na pombe ina asilimia 59 ya vitamini hiyo.
Kulingana na Huduma ya Afya ya Taifa ya Uingereza (NHS), wanaume wanahitaji miligramu 1.4 na wanawake wanahitaji miligramu 1.2 za vitamini B6.
Kulingana na utafiti, lita moja ya bia inaweza kuwa na kati ya miligramu 0.3 hadi 1 ya vitamini B6.
Profesa Michael Ryklik, mwandishi wa utafiti huo, anasema kwamba hata ukitumia kiwango kinachopendekezwa cha pombe, bado hakitoshi kuruhusu mamlaka husika kuisifiwa kwa kiwango cha vitamini kilichochapishwa kwenye chupa.
"Matokeo haya ya utafiti yanafaa tu kwa wale wanaotaka kuboresha kiwango chao cha vitamini mwilini." Anasema
Bia ya zamani ya Kijerumani aina ya Bock ina kiwango kikubwa cha vitamini B6 kuliko bia nyingine kwa sababu ina kiwango cha juu cha pombe, kinachoanzia 6.5%.
Bridget Benelm kutoka Taasisi ya Lishe ya Uingereza anasema kuwa idadi ya watu wenye upungufu wa vitamini B6 nchini Uingereza ni ndogo sana kwa sababu vitamini hiyo hupatikana katika aina nyingi za vyakula.
"Hatuwezi kupendekeza kwa mtu yeyote kwamba bia au kinywaji kingine chochote cha pombe kichukuliwe kama chanzo kikuu cha virutubisho,vitamini hizi zinapaswa kupatikana kupitia lishe," anasema.
"Isipokuwa kama mtu anafuata utaratibu maalum wa chakula, ni nadra sana kukosa kupata kiasi cha kutosha cha vitamini B6."
Benelm anaongeza kuwa ikiwa una matatizo mengine ya kiafya, kama vile uraibu wa pombe au ugonjwa wa figo, unaweza kupata changamoto.
Watafiti wanasema kwamba vitamini zingine, kama vile B12 na B2 hupatikana katika vyakula vya maziwa au vya wanyama.
"Vitamini hii husaidia katika mmeng'enyo wa chakula na uzalishaji wa nishati mwilini."
Wataalam wanashauri kuwa watu wanaofuata lishe ya mboga au vegan wachague njia mbadala za kuongeza vitamini hizo mwilini, kama zile zinazopatikana kwenye maziwa au mtindi ulioboreshwa kwa virutubisho.
End of Pia unaweza kusoma: