Lifahamu kombora la kisasa la Fateh III lililotengenezwa na Pakistan

.

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 4

Baada ya jeshi la Pakistan kuzindua kombora la Fateh III, silaha hiyo iliyo na uwezo wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu imeanza kulinganishwa na kombora la BrahMos la India.

Mnamo Mei 7, idara ya habari ya kijeshi ya Pakistan ilitoa picha ya kombora la Fateh-III katika video ya matangazo inayoashiria kuhusu utayari wa kijeshi wa nchi hiyo.

Ingawa idara ya habari ya jeshi la Pakistai haijafichua uwezo wa kombora la Fateh-III, wataalam wa ulinzi wanaamini kuwa ni kombora la mwendo wa kasi, linalosafiri mara tatu hadi nne ya kasi ya sauti, ambayo Pakistan imeunda ili kufikia malengo ya mashambulio sahihi katika siku zijazo.

Ukifuatilia mitandao ya kijamii, baadhi ya wachambuzi wanalinganisha Fateh-III na BrahMos, ambayo Jeshi la India lilisema liliitumia dhidi ya Pakistan wakati wa "Operesheni Sindoor".

Katika taarifa hii tunaangazia kombora la Fateh-III na linalingana vipi na BrahMos kwa kulinganisha uwezo na ufanisi wa silaha hizo.

Kombora la Fateh-3 lina kitu gani cha kipekee?

Bilal Hussain Khan, mwanzilishi wa shirika la habari za ulinzi na uchambuzi la Quwa lenye makao yake mjini Toronto, na mtafiti wa masuala ya ulinzi, alisema kwamba taarifa zilizopatikana hadi sasa kuhusu kombora la Fateh-3 zinaonyesha kwamba jeshi la Pakistan linajishughulisha na mpango wa kutengeneza kombora lake la kipekee.

Makombora ya Fateh ni silaha za kawaida zinazotumiwa kwa mashambulio ya usahihi ya masafa marefu dhidi ya shabaha, ambayo ni vigumu kufikia au kuangusha kwa sababu husafiri katika miinuko ya chini.

Fateh-1 ina inasafiri kwa kasi ya kilomita 140, wakati Fateh-2 ina safu ya hadi kilomita 400. Taarifa iliyotolewa na jeshi la Pakistan mnamo Aprili 28, 2026, ilisema kwamba kombora asilia la Fateh-2 lililotengenezwa hivi karibuni lilikuwa limefanyiwa majaribio na kwa ufanisi mkubwa.

Bilal Hussain Khan anaeleza kuwa wakati Fateh-4, ambayo ina umbali wa kilomita 750, pia ilijaribiwa kama kombora la kurushwa chini, Fateh-3 inaonekana iliundwa kuwa kombora la kusafiri kwa kasi kubwa.

Alisema kuwa video na picha zilizotolewa na ISPR zinaonyesha kuwa kombora la Fateh-3 linaweza kusafiri kwa kasi zaidi kuliko kasi ya sauti, ambayo ni kutokana na injini maalum iitwayo "ramjet engine". Picha hiyo pia inaonyesha kuwa muundo wake "unafanana na kombora la HD-1 lililotengenezwa na China."

.

Chanzo cha picha, Getty Images

HD-1 ni kombora la masafa marefu ambalo lilitengenezwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya China mwaka 2018. Kulingana na kampuni hiyo, linasafiri kwa kasi kati ya kilomita 2,716 na 4,321 kwa saa, ambayo ni kasi ya juu zaidi -mara kadhaa kuliko kasi ya sauti.

Kwa kuwa Pakistan inaagiza vifaa vyake vingi vya ulinzi kutoka China, Bilal Hussain Khan anaamini kuwa huenda Pakistan imepata leseni ya kutengeneza kombora la HD-1 ndani ya nchi.

Je, inaweza kulinganishwa na Brahmos?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bilal Hussain Khan aliongeza kuwa kombora la BrahMos la India pia linatumia injini ya "ramjet" kuongeza kasi ya sauti, na lina mifumo ya mwongozo na kutafuta shabaha.

"Sawa na BrahMos, HD-1 inaweza kurushwa kutoka ardhini na angani."

Vyombo vya habari vya India viliripoti kuwa kombora hilo la BrahMos lina uwezo wa kufikia shabaha hadi umbali wa kilomita 290 huku likisafiri kwa mwendo wa kasi wa ajabu likiwa linaruka, jambo ambalo hupunguza muda wake wa kusafiri, huwapa walengwa muda mchache sana wa kujikinga, na hufanya mashambulizi yake kuwa ya haraka sana kiasi kwamba ni vigumu kwa mfumo wowote wa ulinzi wa kombora duniani kulizuia.

Kulingana na BrahMos Aerospace, kombora hilo lina uwezo wa kukwepa rada ya adui.

Wakati huo huo, ingawa safu ya kombora la Fateh-3 haijafichuliwa, Bilal Hussain Khan anakadiria kwamba ikiwa inachukuliwa kuwa toleo la "kiwango cha kusafirisha nje" la kombora la HD-1 la China, linaweza kufikia hadi kilomita 280. Lakini, kwa kuwa Pakistan pia imeunda makombora yenye masafa marefu zaidi, anaamini kuwa yanaweza kuongezwa hadi kilomita 400 au 500.

Ameongeza kuwa kwa upande wa mwongozo na teknolojia ya upatikanaji wa shabaha, uwezo wa makombora hayo unaweza kulinganishwa na ule wa BrahMos, kwa sababu silaha za kisasa za China zina nguvu zaidi.

Kwa mtazamo wake, kwa kuwa Pakistan haina vifaa vya kisasa vya kusanifu na kufanyia majaribio injini za "ramjet" na "scramjet" za makombora, kuna uwezekano mkubwa wa kuiomba China msaada.

Alisema kuwa suala hili lilijadiliwa sana mnamo 2018 wakati kampuni ya China ilipotoa kombora la HD-1 kwa Pakistan, na kulikuwa na ripoti kwamba huenda kulikuwa na uhamishaji wa teknolojia.

Kidokezo kingine, alisema, ni kwamba picha iliyotolewa hivi karibuni ya jaribio la Fateh-3 haionyeshi gari linalotumiwa kurushia kombora hilo.

Pia alisema japo India inatengeneza BrahMos ndani ya nchi, kuna uwezekano kwamba injini za ramjet kuagizwa kutoka Urusi. Akiangazia kombora la Fateh-3, alisema kuna uwezekano kwamba Pakistan itaagiza injini hizo kutoka China, na kwamba mfumo wa mwongozo utatengenezwa kwa ushirikiano na China.