Moja kwa moja, Marekani na Iran zatoa madai kinzani kuhusu udhibiti wa Mlango wa Hormuz

Kila upande unasema wanaudhibiti mlango wa Hormuz na kulaumiana kwa mashambulizi ya meli yanayoendelea katika njia hiyo muhimu.

Muhtasari

Marekani na Iran zatoa madai kinzani kuhusu udhibiti wa Mlango wa Hormuz

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Israel yapeleka wanajeshi zaidi katika kijiji ambako familia za Palestina zimezingirwa

    D

    Chanzo cha picha, Reuters

    Israel imesema itapeleka wanajeshi zaidi katika kijiji kimoja cha Ukingo wa Magharibi, ambako walowezi wa Kiyahudi wamezizingira familia mbili za Wapalestina ndani ya nyumba zao tangu Jumapili.

    Video iliyotolewa inaonyesha kundi la kwanza la wanajeshi wa Israel likiingia katika eneo hilo, huku baadhi yao wakionekana kusali pamoja na wakazi wa Kiyahudi wenye misimamo mikali.

    Maafisa zaidi wa usalama walipelekwa katika eneo hilo na kuondoa hema lililokuwa limewekwa hapo. Hata hivyo, waliondoka baada ya mapigano kuzuka, na wakazi kurejea katika eneo hilo.

    Familia za Wapalestina zinazoishi katika kijiji cha Qasra, kusini mwa Nablus, zimesema zimekatiliwa huduma za maji na umeme, huku akiba yao ya chakula ikizidi kupungua.

    Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, makazi yote ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel ni kinyume cha sheria.

    Soma Zaidi:

  2. Mamlaka ya ICE yapanga kuwapatia maafisa glovu zinazoweza kutoa mshtuko wa umeme

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maafisa wa Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha nchini Marekani, ICE, wanaweza kuanza kutumia glovu zinazoweza kutoa mshtuko wa umeme wanapotekeleza majukumu yao ya kiusalama.

    ICE imepanga kutumia hadi dola milioni 20 kununua glovu hizo zinazojulikana kama Generated Low Output Voltage Emitter, GLOVE, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Jumatatu na Idara ya Usalama wa Taifa, DHS.

    Glovu hizo zina uwezo wa kutoa mshtuko wa umeme wa hadi volti 380, karibu mara tatu ya kiwango cha umeme kinachotolewa na soketi ya kawaida nchini Marekani.

    Mashirika ya kutetea haki za kiraia, likiwemo American Civil Liberties Union, ACLU, yameeleza wasiwasi kuhusu matumizi ya glovu hizo.

    ICE imekuwa ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu mbinu zake wakati wa operesheni za utekelezaji wa sheria, ambazo zimesababisha maafisa wake kuhusishwa katika matukio kadhaa ya watu kuuawa kwa kupigwa risasi.

    DHS imeiambia BBC kuwa ICE inaendelea kutathmini mahitaji ya maafisa wake walio katika maeneo ya utekelezaji wa sheria, ili kuhakikisha wanapata vifaa vinavyohitajika kuwakamata na kuwaondoa nchini wahamiaji wanaokiuka sheria za uhamiaji.

    Kampuni ya Compliant Technologies LLC, inayotengeneza glovu hizo, imeiambia BBC kuwa haiwezi kutoa maoni kuhusu mauzo hayo.

    DHS imesema mkataba wa ununuzi wa glovu hizo bila mchakato wa zabuni unaweza kuchapishwa mapema Ijumaa.

    Glovu hizo huwashwa kwa kubonyeza kitufe na zinaweza kutoa hadi mishtuko 30 ya umeme kwa sekunde. Pia zina vichakataji vidogo vinavyorekodi kila matumizi ya kifaa.

    Compliant Technologies inasema kwenye tovuti yake kuwa glovu hizo hazisababishi majeraha na zinatumiwa na taasisi mbalimbali za utekelezaji wa sheria.

    Soma Zaidi:

  3. Caroline Levitt kujiuzulu kama msemaji wa Ikulu ya Marekani - Trump

    x

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Levitt, atajiuzulu wadhifa huo mwishoni mwa mwezi huu.

    Trump amesema katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwamba Levitt anaondoka kwenye nafasi hiyo ili kutumia muda zaidi na watoto wake wadogo pamoja na familia yake, akisema kuwa anaelewa na kuheshimu uamuzi huo kikamilifu.

    Trump amemtaja Caroline Levitt kuwa miongoni mwa wasaidizi wake anaowaamini zaidi.

    Rais huyo ameongeza kuwa Levitt sasa atakuwa mmoja wa washauri wake muhimu wa nje ya serikali na ataendelea kuwa sauti yenye ushawishi ndani ya Chama cha Republican.

    Levitt, mwenye umri wa miaka 28, aliteuliwa kuwa msemaji wa Ikulu mwaka jana na kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushika wadhifa huo.

    Hadi sasa haijafahamika mara moja ni nani atakayemrithi katika nafasi hiyo.

  4. Serikali ya Uingereza yaonya kuhusu athari za kufungwa kwa Mlango wa Hormuz kwa uchumi

    x

    Chanzo cha picha, AP

    Serikali ya Uingereza imeingiwa na wasiwasi kwamba kuendelea kwa usumbufu wa usafirishaji wa meli kupitia Mlango wa Hormuz kunaweza kudhoofisha zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo mwakani.

    Makadirio ya ndani ya Hazina ya Uingereza yanaonyesha kuwa iwapo usumbufu huo utaendelea hadi mwisho wa mwaka, ukuaji wa Pato la Taifa unaweza kushuka hadi asilimia 0.3 mwaka 2027.

    Maafisa wa Hazina wamewasilisha tathmini hiyo kwa Waziri Mkuu, huku serikali ikisema inaendelea kujiandaa kwa matukio mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

    Hata hivyo, serikali imeonya kuwa makadirio ya ukuaji wa asilimia 0.3 yanatokana na hali mbaya zaidi kuliko ilivyotarajiwa, na si utabiri wake wa msingi.

    Tathmini hiyo inakuja wakati uchumi wa Uingereza tayari ukikabiliwa na ukuaji dhaifu. Maafisa wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu takwimu mpya za Pato la Taifa ili kubaini athari za mzozo huo kwa uchumi.

    Vita vya Mashariki ya Kati na mzozo kati ya Marekani na Iran vimesababisha kupanda kwa bei za nishati na kuvuruga kwa kiasi kikubwa usafirishaji wa meli kupitia Mlango wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.

    Soma Zaidi:

  5. Marekani na Iran zatoa madai kinzani kuhusu udhibiti wa Mlango wa Hormuz

    D

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza tena kuwa Marekani ina “udhibiti kamili” wa Mlango wa Hormuz, licha ya kupungua kwa shughuli za usafirishaji katika njia hiyo muhimu ya majini hadi kiwango cha chini zaidi kwa wiki moja, huku vita dhidi ya Iran vikiendelea.

    Kwa upande wake, Tehran imesisitiza msimamo wake wa kuendelea kupinga Marekani na kuufanya Mlango wa Hormuz ubaki umefungwa hadi masharti yake yote yatimizwe.

    Trump amesema watu wengi wanaita kizuizi cha Marekani katika Mlango wa Hormuz “ukuta wa chuma” na kwamba Iran haina uwezo wa kukizuia.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amesema Marekani ina udhibiti kamili wa Mlango wa Hormuz na kuongeza kuwa anaamini itaendelea kuudhibiti.

    Trump amedai Iran haina jeshi la wanamaji wala jeshi la anga, huku wanajeshi wa Iran wakidaiwa kutolipwa mishahara. Pia amesema Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, limedhoofishwa pakubwa na linarudi nyuma.

    Aidha, Trump amesema hali ya uongozi wa Iran bado haijulikani, huku akidai nchi hiyo haina fedha na kwamba kinachobaki ni “habari za uongo na mfumuko wa bei wa asilimia 300”.

    Trump amesisitiza kuwa Iran huzungumza tu bila kuchukua hatua.

    Unaweza kusoma;

  6. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 13/08/2026.