Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Saudi Arabia iliishambulia Iran kwa siri?
Saudi Arabia ilitekeleza mashambulizi ya siri dhidi ya Iran kama hatua ya kujibu mashambulizi yaliyolenga taifa hilo wakati wa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Mashambulizi hayo ambayo hayakutangazwa rasmi na inaashiria hatua ya kwanza iliyochukuliwa kijeshi na Saudi Arabia dhidi ya Iran, na jinsi taifa hilo liko tayari kujilinda dhidi ya mashambulizi.
Mashambulizi hayo, yaliyofanywa na jeshi la anga la Saudi Arabia, yanakadiriwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Machi.
Alipoulizwa kuhusu shambulio hilo afisa mmoja mkuu wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Saudi Arabia alikataa kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu iwapo mashambulizi hayo yalifanyika.
Mataifa ya Ghuba kuanza kujibu mashambulizi
Mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya Iran, yanaonyesha kupanuka kwa mzozo unaoendelea .
Tangu Marekani na Israel ziliposhambulia Iran, Iran imekuwa ikirusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya nchi zote sita za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC), ikilenga si tu kambi za kijeshi za Marekani bali pia maeneo ya raia, viwanja vya ndege na miundombinu ya mafuta, Pamoja na kufunga Mlango Bahari wa Hormuz, hatua ambayo imeathiri biashara ya kimataifa.
Falme za Kiarabu (UAE) pia imefanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, gazeti la Wall Street Journal liliripoti siku ya Jumatatu.
Hatua za Saudi Arabia na UAE zinafichua hali halisi ya vita hivyo ambavyo imekuwa ikifichwa kwa muda mrefu.
Mashambulio, kisha kusitisha mapigano
Maafisa wa Iran na maafisa wengine kutoka mataifa ya magharibi walisema Saudi Arabia ilijulisha Iran kuhusu shambulio hili, suala ambalo limeharibu uhusiano kati ya mataifa jayo mawili.
Ila mataifa hayo mawili kwa sasa yamekubaliana kusitisha mashambulizi baada ya Marekani kutangaza usitishaji mapigano dhidi ya Iran.
Iran na Saudi Arabia, mataifa mawili makubwa ya Kiislamu Mashariki ya Kati ,yamekuwa yakiwaunga mkono makundi yanayopingana katika migogoro inayoendelea ukanda huo.
Makubaliano yaliyosimamiwa na China mwaka 2023 yalirejesha uhusiano wa ataifa hayo mawili, ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa mapigano kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na Saudi Arabia nchini Yemen.