"Una wazimu" Simu ya mzozo kati ya Trump na Netanyahu yavuruga mazungumzo na Iran

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais wa Marekani Donald Trump wamebishana na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,kuhusu wanajeshi wa Israel kuendeleza oparesheni nchini Lebanon, na kuvuruga mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

Iran imesema iwapo Israel itaendelea kuishambulia Lebanon, watasitisha mazungumzo ya kupatikana kwa amani na Marekani.

Katika mkutano na wanahabari, mwanahabari wa axios alimuuliza Trump iwapo alimuambia Netanyahu kwa njia ya simu kuwa "amekuwa wazimu" na kukosa shukran.

Trump alijibu na kusema "ndio nilisema hivyo, sisemi nilikuwa na hasira, ila nimekasirishwa na vita vinavyoendelea Lebanon"

Aliongezea kuwa " nampenda Netanyahu, nimekuwa nikishirikiana na yeye vizuri"

Trump ndiyo rais pekee wa Marekani ambaye amekosana na Waziri mkuu wa Israel.

Netanyahu anajulikana kwa kujaribu ustahimilivu wa ikulu ya Whitehouse na mara nyingi hajakuwa akikosolewa.

Mabishano ya hivi karibuni yametokea wakati Rais Trump anatarajia kuwe na makubaliano ya kusitisha mapigano kati yake na Iran, na kufungua mlango wa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia.

Aidha suala la kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz bado halijatatuliwa.

Marafiki wakuu

Netanyahu amepuuzia semi kuwa kuna utafauti kati yake na mshirika wao wa karibu, Marekani.

"wakati mwingine kama tu katika familia tunatofautiana, ila huwa tunapata njia ya kutatua" Netanyahu alisema katika mahojiano na CNBC

Aliongezea kuwa wanaweza kukosana asubuhi na kufikia makubaliano jioni.

Aidha wataalama wanasema kuwa maneno aliyotumia Trump katika mawasiliano yao ya simu ni kuonyesha kuchoka na hatua za Israel ambazo haziambatani na malengo ya Marekani.

Uungwaji mkono wa Israel umepungua

Israel na Marekani wanakubaliana kuhusu Iran kutomiliki silaha za nyuklia.

Ila nchini Lebanon, maslahi yao yanatofautiana, kwani Israel imeapa kuiangamiza kundi la Hezbollah, huku mazungumzo kati ya Iran na Marekani yakiendelea.

Iran imesisitiza kuwa makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano lazima yajumuishe Lebanon.

Haya yote yanajiri wakati ambapo raia wa Marekani wameanza kukosoa uungwaji mkono ambao Marekani wamaekuwa wakiipa Israel kwa muda mrefu.

Viongozi wengi pia wamekosoa hatua ya Israel kumshinikiza Trump kuingia vitani, suala ambalo Ikulu ya White House na Netanyahu wamekanusha.

Mahusiano yenye wasiwasi

Viongozi wengine wa Marekani, wamekuwa wakikerwa nah atua za Netanyahu.

Netanyahu amewahi kubishana na rais wa zamani Bill Clinton kuhusu kutekelezwa kwa makubaliano ya amani ya mwaka wa 1993 ya Oslo peace Accords.

Netanyahu pia alikuwa na mahusiano magumu na rais Barack Obama baada ya Waziri huyo kuhutubia bunge la congress mwezi Machi mwaka wa 2015 kuhusu sera ya Iran, bila kujulisha ikulu ya White House.

Mahusiano yake na rais Joe Biden pia yalizorora, baada ya kuishtumu Marekani kwa kukataa kuwapa silaha.

"Amekuwa na mahusiano ya wasiwasi na Marekani" anasema Natan Sacks mtaalam wa mahusiano ya Marekani na Israel kutoka taasisi ya Middle East Institute, mjini Washington.

Anaongezea kuwa ni "mtu anayejuwa kujadili na si muaminifu"

Ila haijulikani kama utaofauti walionao na Trump kwa sasa utaharibu uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.