Afghanistan: Kwa nini serikali mpya ya Taliban ni ushindi kwa Pakistan na kikwazo kwa India?

Chanzo cha picha, AFGHAN ISLAMIC PRESS
Saa kadhaa baada ya Taliban kutangaza serikali ya mpito nchini Afghanistan, inasemekana ushawishi wa Pakistan umejitokeza kuashiria nchi hiyo imepata ushindi mkubwa.
Mullah Mohammad Hassan Akhund, ambaye ni kiongozi mwenye misimamo mikali katika Baraza la Rahbari-Shura, atakuwa waziri mkuu mpya wa Afghanistan.
Huyu ni yule yule Mullah Akhund ambaye aliharibu sanamu ya Wabuddha mjini Bamiyan mwakwa 2001.
Kabla ya uteuzi huo Mullah Hassan, kulikuwa na uvumi kuwa Abdul Ghani Baradar, ambaye ni mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Taliban mjini Doha, Qatar, huenda akachukua uongozi wa Afghanistan.
Awali, hakukua na makubaliano juu ya kuunda serikali chini ya uongozi wa Taliban.
Lakini Jenerali Faiz Hamid, mkuu wa shirika la kiintelijensia wa Pakistani ISI, alipowasili Kabul siku tatu baadaye, Taliban wakatangaza uongozi wa juu wa serikali
Baada ya tangazo hilo la Taliban nchini Afghanistan, Mtaalamu mashuhuri wa kimkakati wa India Brahma Chelanialiandika katika mtandao wake wa Twitter, "Mtu aliyejumuishwa na Umoja wa Mataifa katika orodha ya magaidi, na ambaye alilibomoa sanamu ya Buddha, atakuwa Waziri Mkuu wa Afghanistan.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Sirajuddin Haqqani ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani ni mwanachama wa mtandao hatari wa Haqqani na tunasema Taliban sio ile ya zamani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwanini ni kikwazo kwa India?
Gazeti la Indian Express limeandika katika ripoti yake kwamba ushawishi wa jeshi la Pakistan unaonekana wazi katika serikali ya Taliban.
Indian Express aliandika, "Serikali mpya ya Afghanistan inatawaliwa na shirika la kigaidi la Mtandao wa Haqqani na kikundi cha Taliban kinacholenga Kandahar katika baraza jipya la mawaziri, wakati kundi la Taliban lenye makao yake Doha lililoanzisha mazungumzo ya kimataifa na pia kuwasiliana na New Delhi, limewekwa kando.
Mawaziri 20 kati 33 katika baraza jipya la mawaziri la Taliban, ni wafuasi wa kundi la Taliban linacholenga Kandahar na mtandao wa Haqqani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Jambo linalotia India wasiwasi zaidi ni uteuzi wa Sirajuddin Haqqani kama Waziri mpya wa Mambo ya Ndani wa Afghanistan.
Mwanahabari wa gazeti la Pakistan 'International the News' Ziaur Rahman ameandika katika Twitter yake kuhusu serikali mpya ya Taliban, akisema, "Kuna mawaziri wasiopungua sita katika serikali ya mpito ya Taliban ambao wamejifunza kutoka Seminari ya Jamia Haqqania (Akora Khattak) ya Pakistan."
Sirajuddin Haqqani Anatajwa kuwa kipenzi cha shirika la kijasusi la Pakistan (ISI). Sirajuddin ni mkuu wa matandao wa Haqqani na anadaiwa kuhusika na shambulio la mwaka 2008 dhidi ya ubalozi wa India mjini Kabul.
Kati ya mwaka 2009 na 2010, mtandao wa Haqqani ulilenga maslahi ya Wahindi na India.
Kujumuishwa kwa Haqqani katika serikali ya Afghanistan inatafsiriwa kama habari mbaya kwa India.

Chanzo cha picha, BBC URDU
Kwa nini Pakistan imeshinda?
Kama waziri wa mambo ya ndani, Haqqani hatasimamia tu mikakati ya kiusalama ya Afghanistan pekee, lakini pia atawateua magavana 34 wa mikoa. Inasemekana hii inamaanisha ISI itakuwa na jukumu katika uteuzi wa magavana wa mikoa.
Hatua hiyo, itakuwa kikwazo cha kimkakati kwa India.
Jina la Sirajuddin Haqqani lilikuwa limewekwa katika orodha ya kimataifa ya magaidi.
Idara ya mambo ya nje ya Marekani ilikwa imetangaza zawadi yad ola milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa Sirajuddin. Haqqani pia alisakwa Januari mwaka 2008 kuhusiana na shambulio dhidi ya hoteli mjini Kabul.
Watu sita waliuawa katika shambulio hilo miongoni mwao raia wa Marekani.
Shirika la ujasusi la Marekani FBI, pia lilisema Haqqani alidaiwa kuhusika na mauaji ya mwaka 2008 ya Rais wa Afghanistan wa wakati huo, Hamid Karzai.
Mullah Mohammad Hassan Akhund ndiye Waziti Mkuu mpya wa Afghanistan na jina lake liko katika orodha ya magaidi ya Umoja wa Mataifa
Kwao ni Kandahar na Taliban pia ilianzishwa hapa. Mullah Mohammad ni mmoja wa waanzilishi wa Taliban.
Alihudumu kama mkuu wa Rehbari Shura kwa miaka 20 na anasadikiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Kiongozi Mkuu wa Taliban, Mullah Hibtullah Akhundzada.
Mullah Mohammad Hassan alikuwa waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Taliban kuanzia mwaka 1996 hadi 2001.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mulla Baradar haaminiki
Mullah Baradar atakuwa mkuu wa serikali Mulla Hassan. Kando na hilo, Abdul Salam Hanafi, ambaye ni ria wa Uzbekistan, ameteuliwa kuwa makamu wa pili wa Waziri Mkuu. Mullah Baradar ni muanzilisha mwenza waTaliban.
Alikamatwa na shirika la kiintelijensia la Pakistan mnamo mwezi Februari 2010 mjini Karachi baada ya majadiliano ya wazi na Hamid Karzai.
Aliachiliwa mwaka 2018 kwa ushirikiano na utawala wa Marekani. Mullah Baradar alikuwa akiongoza ofisi ya siasa Taliban mjini Doha tangu mwaka 2019 na mazungumzo ya kimataifa yalikuwa yakiendelea chini ya uongozi wake.
Mwezi Machi 2020, Baradar alizungumza na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kwa nji aya simu. Donald Trump alikuwa amekubaliana na hilo hivi karibuni.
Ilikuwa imesemekana Mullah Baradar angelikuwa kiongozi wa serikali ya Afghanistan, lakini kulikuwa na uvumi kwamba Pakistan haikumuamini, kwa hivyo ilikuwa vigumu.
Kati ya mawaziri 33 walioteuliwa katika serikali mpya ya Taliban, ni watatu tu ambao sio - Wapashtun.










