Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Juventus wafukuzia kumpata Zirkzee

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi, Joshua Zirkzee,25, kwa mkopo kutoka Manchester United bila kuwa na sharti la kumnunua moja kwa moja. (Gazzetta dello Sport)

Liverpool haina mpango wa kumsajili beki wa Tottenham na England, Djed Spence, 25, katika usajili la majira ya joto, licha ya mchezaji huyo kukabiliwa na changamoto ya majeraha hivi karibuni. (Mirror)

Arsenal na Manchester United zimewapeleka wapelelezi wa vipaji kumtazama mshambuliaji aliye na umri wa miaka 20, Kaua Elias, akifunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu akiichezea Shakhtar Donetsk, huku AC Milan na Porto nazo zikimnyatia mchezaji huyo wa Brazil. (Sun)

Liverpool imeongeza kasi ya mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Paris St-Germain na Senegal, Ibrahim Mbaye,18, baada ya kijana huyo kuweka wazi nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo bingwa ya Ufaransa. (Teamtalk)

Mazungumzo kati ya West Ham na Tottenham kuhusu winga wa Israel mwenye umri wa miaka 27, Manor Solomon, yamesisitishwa kwa sasa kutokana na sababu za kifedha, West Ham haiko tayari kukubaliana na marupurupu ambayo Spurs wangetaka iwapo itafanikiwa kurejea Ligi Kuu yaEngland. (Athletic - usajili unahitajika)

Ipswich na Everton ni miongoni mwa klabu zinazotaka kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Senegal Krepin Diatta, 27, ambaye ni mchezaji wa upande wa kulia anayeweza kucheza nafasi mbalimbali lakini ni mchezaji huru kwa sasa baada ya mkataba wake na Monaco kumalizika mwezi Juni. (Footmercato - kwa Kifaransa)

Pia, Ipswich imepiga hatua kubwa katika mazungumzo na klabu ya Fulham kuhusu mpango wa kumsajili moja kwa moja kiungo wa Serbia mwenye umri wa miaka 29, Sasa Lukic. (Sky Sports)

Galatasaray imemuongeza mshambuliaji wa Arsenal na Brazil aliye na umri wa miaka 25, Gabriel Martinelli, kwenye orodha yao ya wachezaji wanaolengwa kusajiliwa. (Gianlucadimarzio - kwa Kiitaliano)

Sunderland ina nafasi kubwa ya kumsajili winga wa Msumbiji, Geny Catamo, kutoka Sporting Lisbon, huku Aston Villa, Brentford na Everton zikiwa miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 25. (Teamtalk)