Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Arsenal, Man City zinamgombea Neto wa Chelsea
Arsenal, Manchester City na Al-Hilal zinamvizia winga wa Chelsea, Pedro Neto, na zinaweza kuwasilisha ofa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la usajili la Januari. (Caught Offside)
Chelsea inataka kukamilisha usajili wa kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, mapema, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo msimu ujao, baada ya ofa ya pauni milioni 60 kutoka Chelsea kukataliwa katika dirisha la hivi karibuni la usajili. (Teamtalk)
Mshambuliaji wa Chelsea, Christopher Nkunku, mwenye umri wa miaka 28, alikataa ofa kutoka Manchester United na Newcastle United kabla ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda RB Leipzig. (Bild & Sky Sport Germany via Caught Offside)
Mshambuliaji wa Marekani, Folarin Balogun, anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Saudi Arabia, ambako dirisha la usajili bado liko wazi. Monaco inakabiliwa na shinikizo la kifedha la kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 baada ya yeye kujiondoa katika uhamisho wa kwenda Everton dakika za mwisho za siku ya mwisho ya usajili. (Football Insider)
Mkataba wa kiungo mshambuliaji wa Newcastle United, Jacob Murphy, unaisha msimu ujao, lakini mchezaji huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 31 anaweza kupewa mkataba mpya na klabu hiyo. (Football Insider)
Winga wa zamani wa Chelsea, Hakim Ziyech, ameachana na Wydad na mchezaji huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 33 amehusishwa na uhamisho wa kwenda klabu ya Brazil, Botafogo. (Goal)
Kiungo wa England, Curtis Jones, mwenye umri wa miaka 25, amesema mazungumzo yake na kocha wa Inter Milan, Cristian Chivu, yalikuwa muhimu katika uamuzi wake wa kuhamia klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool msimu huu wa joto. (Mirror)