Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Liverpool kumsajili Ismaila Sarr kutoka Crystal Palace
Liverpool itazingatia jaribio jingine la kumsajili Ismaila Sarr kutoka Crystal Palace mwezi Januari baada ya kushindwa kufikia makubaliano kuhusu winga huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 28 kabla ya mwisho wa dirisha la usajili la majira ya joto. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Brazil anayetaka kuondoka Tottenham, Richarlison, anatarajia kukamilisha uhamisho kwenda Ligi ya Kulipwa ya Saudi Arabia (Saudi Pro League) ambapo usajili unaruhusiwa hadi tarehe 12 Oktoba baada ya kushindwa kujiunga na Trabzonspor kabla ya dirisha la usajili nchini Uturuki kufungwa siku ya Ijumaa. (Standard)
Arsenal inakaribia kufikia makubaliano ya mkataba mpya na meneja Mikel Arteta, ambaye mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa msimu huu; wakati huo huo, klabu hiyo inapiga hatua katika mazungumzo ya mikataba mipya na kiungo wa England Declan Rice (27), mbunifu wa mashambulizi kutoka Norway Martin Odegaard (27), na beki wa Uholanzi Jurrien Timber (25). (Teamtalk)
Arsenal iliulizia kuhusu winga wa Ujerumani Kevin Schade wakati wa majira ya joto lakini ikaachana na mpango huo kwa kuwa Brentford haikuwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Teamtalk)
Manchester United itaendelea kumfuatilia beki wa kushoto wa Newcastle United, Lewis Hall (21), ikilenga uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa England msimu ujao wa joto. (Football Insider)
Kiungo wa Ubelgiji, Amadou Onana, ametia saini mkataba mpya na Aston Villa utakaodumu hadi mwaka 2031. (Sacha Tavolieri)
AC Milan bado inamtaka beki wa Sporting, Goncalo Inacio (25), na huenda ikajaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Tuttomercatoweb - Italia)
Manchester United inaendelea na mazungumzo ya kumsajili kiungo wa England, Louis Page, kutoka Leicester City baada ya kushindwa kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Manchester Evening News kupitia Evening Standard)
Lyon ilifikiria kumrejesha klabuni hapo mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Karim Benzema, lakini mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 kama balozi wa Ligi ya Kulipwa ya Saudi Arabia ulimzuia kufanya uhamisho huo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Aston Villa na Sunderland zilikuwa miongoni mwa klabu zilizokuwa na nia ya kumsajili beki Mfaransa Matthieu Udol, lakini Lens ilimzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka. (Foot Mercato, kupitia Get French Football News)