Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, "Je una akili timamu bwana afande?" - Lissu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, anaendelea leo, Jumanne Agosti 11, 2026, kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.

Moja kwa moja

Na Eagan Salla

  1. Lissu amuhoji shahidi kama alipewa jina la mwanachadema yeyote aliyekua hatarini kwa vitisho

    Lissu: Waeleze majaji kama uliwasilisha hiyo barua

    Shahidi: Ipo

    Lissu: Ipo Mahakamani

    Jajji: Shahdi embu jibu kama umeleta au hujaleta mawakili wa serikali watakuuliza baadae pia

    Lissu: Kwa hiyo jibu ni lipi

    Shahidi: Sijaleta

    Lissu: Nataka maswali yangu yajibiwe kwemye ushahidi wako, jana ulisema hivi baada ya kaungalia hiyo video uliona kwamba mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kuchapisha kwa umma, kwa kuchapisha kwemye Jambo TV. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Shahidi kwenye ushahidi wako kuhusu tuhuma ulisema, uchaguzi mkuu uko kwa mujibu wa Katiba na mlinzi mkuu wa Katiba ni serikali. Umewahi kusoma Katiba?

    Shahidi: Kipindi cha nyuma

    Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee Katiba, Ibara ya 26 - "Kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuzifuata na sheria za nchi hii, wewe umesema ni serikali

    Shahidi:.......

    Lissu: Ulisema kulikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kupiga watu mawe na mengineyo, waeleze majaji kama hayo maneno yako kwenye maelezo yako

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Jana ulisema hivi, hiyo video mliyoiangalia iliwekwa kwenye 'memori kadi' ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi ili kuithibitisha, sasa waeleze majaji kama hayo yapo kwemye maelezo yako

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na wengine 15 waliopita hawakuwasilisha video Mahakamani naomba waeleze majaji kama umewasilisha hiyo video

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Kwakuwa wewe ni shahidi wa 16 na hakuna aliyewasilisha ripoti ya kubaini uhalisia wa hizo video, waeleze majaji kama umewasilisha hiyo ripoti ya uchunguzi

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Unasema ulimuelekeza Inspekta Michael kuchukua vielelezo pamoja na ripoti ya uchunguzi na kukabidhiwa kwa mtunza nyaraka. Je, hayo yapo kwenye maelezo yako?

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Baada ya kufanya yote ambayo mlikua mmeshafanya uliwasiliana na Ma RCO nchi nzima, hiyo ipo sitakuuliza, sasa kwenye maelezo yako jana umetaja majalada ya uchunguzi toka mikoa mbalimbali; Ruvuma, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam. Mimi nakuuliza juu ya jalada la Dar es Salaam, toka ofisi ya ZCO ambalo namba zake ni….. waeleze majaji kama lipo kwenye maelezo yako.

    Shahdii: Hayapo

    Lissu: Jana ulisema mtuhumiwa alikamatwa Mbinga na kusafirishwa usiku huo huo mpaka Dar es Salaam, Kituo Kikuu cha Kati na kufikishwa ofisi ya Deputy ZCO. Waeleze majaji kama hapo maelezo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Ulieleza pia jinsi ulivyopeleka jalada ofisi ya DPP na baadae jalada kurejeshwa kwenu kuendelea na upelelezi, waeleze majaji kama hicho kipande kipo

    Shahidi: Hakipo

    Lissu: Unasema mlipata taarifa mashahidi kutishiwa, je kwemye maelezo yapo?

    Shahdi: Hayapo

    Lissu: Unasema mliwasiliana na ofisi ya DPP ili kuweza kuwapatia ulinzi mashahidi, Je yapo?

    Shahdi: Yapo

    Lissu: Unasema mliomba kwa barua sema kama yapo

    Shahidi: hayapo

    Lissu: Unasema ulikula kiapo ili kuwaombea ushahidi, Je yapo?

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Hayo ni kutoka kwenye ushahidi wako jana sasa twende kwingine, umewaeleza majaji kwamba umesoma hiyo hati ya kiapo?

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Waeleze majaji kwenye hati hii uliyosaini kama ulitaja jina la shahidi yeyote

    Shahdi: Hapana

    Lissu: Waleze majaji kama ulipewa jina la mwanachadema yeoyote aliyekua hatarini kwa vitisho

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waleze majaji kama ulitaja mwanachama yeyote alikua akitoa vitisho hivyo

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waleze majaji kama ulitaja siku au mahali

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waeleze majaji kama ulitaja aina ya vitisho

    Shahidi: Ndio nilitaja

    Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimuoneshe shahidi kiapo chake

    Inaendelea..............

  2. Lissu: Unataka na Mawakili wakae hapo na wao niwakaange?

    Lissu: Umeeleza kwamba ulipofika kwa Deputy ZCO, George Pademi baada ya kutambulishwa timu, uliwapangia majukumu na ulikuwa na timu tatu. Waeleze majaji hawa watu uliowataja jana kama wako kwenye maelezo yako uliyoandika mwaka jana

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Nyongeza nyongeza.

    Pia ulieleza ulikuwa na timu ya watu uliowataja jana pia kama wako kwemye maelezo yako

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Pia ulieleza ulikuwa na timu ya tatu ya Legal and Advisory, unataka kuonyesha mlifuata sheria, unasema ulikuwa na mtu ambaye jina lake hukumbuki alikuwa na jina la kibantu alitoka ofisi ya DPP Dodoma, je waeleze majaji kama hayo maelezo yapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Tubaki hapo nilimuuliza shahidi wa kwanza George Bajemu alisema hakukuwa na mwanasheria kwenye timu yenu, je tumuamini nani

    Shahidi: Kulikua na mwanasheria

    Lissu: Basi tukuamini wewe George ni liongo

    Lissu: Unasema mkiwa ofisini kwa kutumia kompyuta mlitazama hiyo video Jambo TV kwa saa mbili na usheee mkiwa timu nzima waambie majaji kama yapo hayo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Hapo hapo, Shahidi wa kwanza, George Bajemu aliambia Mahakama alioneshwa vipande vipande na Kaaya wewe unasema mlitazama mkiwa na timu nzima tumuamini nani

    Shahidi: …. Kabla hajajibu….

    Wakili wa serikali anakatisha kidogo na kuomba kwamba Ushahidi wa Bajemi ulikua wa tarehe nne na huyu anaongelea ushahidi wa kuanzia tarehe 8 naomba wafuate rekodi sawa sawa

    Lissu: Waheshimiwa majaji hawa mawakili wa serikali si wana haki ya re-examination watauliza kwa wakati wao, wako nane wanaanzaje kunifundisha mimi kufanya dodoso wasubiri zamu yao

    Kimya kidogo Majaji wanaongea……

    Jaji anatoa ufafanuzi waendeleee ila kwa kufuata taratibu

    Lissu: Narudia swali langu George Bajem anasema mliona video vipande vipande wewe unasema mlitamza yote Majaji wa amini kipi

    Shahidi: George yeye na Kaaya walitazama vipande vipande na mimi baadae baada ya kuteuliwa ndio tulikaa tukatazama kama timu kwemye kompyuta maalumu

    Lissu: Waheshimiwa majaji maelezo ya George Bajem yako kwenye 'information' na niliyafanyia dodoso kwa kina na hayakuwa 'tendered' ila yako kwenye rekodi za Mahakama na nina haki ya kumuuliza shahidi kwa kutumia maelezo haya

    Shahidi: Hayo sio maelezo yangu hiyo ni rekodi ya Mahakama siyajui

    Lissu: Haya ndio maelezo mliyokusanya ninyi Jeshi la polisi na mkayaleta unasema hujui

    Shahidi: Maelezo ya George ni ya tarehe 4 na yangu ni tarehe nane

    Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi asome maelezo yake yote kuanzia mwanzo

    Shahidi: Anasoma maelezo yake…….

    Lissu: Mpaka hapo kuna mahali mmeangalia video?

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Tuendeleee, kwenye maelezo yako ya jana umesema ulipotazama hiyo video ulimuona mtuhumiwa Lissu na nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na Chadema waeleze majaji kama hayo yapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Kwenye maelezo yako ulisema Lissu alikua akihutubia umma wa watanzania waambie majaji kama hayo yapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema kwamba mliwasiliana na Idara ya Uhamiaji ambayo iliwathibitishia Lissu ni Raia wa Tanzania je hayo yapo kwenye maelezo yako?

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Waeleze majaji kama umewasilisha Mahakamani barua kama uliwasiliana Idara ya uhamiaji

    Shahidi: Barua zipo

    Lissu: Umewasilisha Mahakamani?

    Shahidi: Kimya.....

    Lissu: Unataka na mawakili wakae hapo na wao ni wakaange?

    Itaendelea…..

  3. "Je una akili timamu bwana afande?" - Lissu

    Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa 16 wa Jamhuri, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amin Mahamba aliyeanza naye jana:

    Lissu: -Shahidi habari yako ulilala vizuri?

    Shahiri: Salama Ahsante

    Lissu: Sasa jana nilikua nakupitisha kwenye maelezo yako uliyotoa kizimbani naomba leo ukijibu utoe sauti kikakamavu kama askari anayeweza kuendesha gwaride.

    Lissu: Waeleze majaji kama mwaka 2014 uliteuliwa kuwa OCCID Kyela waeleze majaji kama ipo?

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Waelezema majaji kama (maelezo ya) ulifanya kazi Kyela kama OCCID kwa miaka miwili na baadae ukahamishiwa Ruvuma

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Na ulikuwa RCO wa mkoa wa ruvuma kwa miaka mitano

    Shahidi - Hayapo

    Lissu: January 2023 ulihamishiwa Dar kama Naibu ZCO kanda maalumu waeleze majaji kama hayo maelezo yapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Ukiwa Deputy ZCO ulikua unasinamia wapelelezi wote wa Kanda maalumu

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Kama RCO Kinondoni ulikuwa mkuu wa wapelelezi wote wa mkoa wa kipolisi Kinondoni waambie majaji kama hayo maelezo yapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Mwezi Mei 2024 ukahamishwa na kupelekwa kwenye kitengo X ambapo upo mpaka leo waeleze majaji kama ipo kwenye maelezo yako

    Shahidi - Hayapo

    Lissu: Sasa shahidi kwenye ushahidi wako wa jana ulisema hivi tarehe 8/04/2025 nikiwa ofisini kwangu masaa ya mchana nilipigiwa simu na mkuu wangu wa kazi DCP Nganzi kwenye ofisi za ZCO Dar es Salaam, ili kwenda kuratibu na kusimamia upelelezi dhidi ya mtuhumiwa Tundu Lissu, waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako kilelezo namba D15

    Shahidi: Yapo

    Lissu: Waeleze majaji kama kuna sehemu inamhusu mtuhumiwa Tundu lissu

    Shahidi: Yapo

    Lissu: Isome tena , Lissu anamsomea tena

    Na anamuuliza: Je kwenye maneno uliyasema jana kuna majina Tundu Lissu

    Shahidi: Yapo

    Lissu: Je una akili timamu bwana afande? kuna jina Tundu Lissu

    Shahidi: Yapo

    Lissu: Ndio maana nasema unajifanya mjanja huna lolote afande mpelelezi mbobevu

    Lissu: Ulisema jana ulipofika ulipoitwa uliona jalada mezani ambalo lilimtaja mtuhumiwa Tundu Lissu

    Shahidi: Yapo

    Lissu: Kwenye karatasi yapo

    Shahidi: Hayapo

    INAENDELEA...........

  4. Picha kutoka Mahakamani

  5. Lissu awasili Mahakama Kuu

    Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amewasili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili.

    Lissu anatarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, katika hatua ya 'cross-examination'.

    Jana, Mahamba alimaliza kutoa ushahidi wake wa msingi baada ya kueleza kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, ikiwemo video ya hotuba ya Lissu na madai ya polisi kuhusu kauli zake za kuzuia uchaguzi. Lissu alianza kumuhoji shahidi huyo jana na leo punde anatarajiwa kuendelea na maswali yake.

  6. Lissu alivyoanza kumuhoji shahidi

    Baada ya Mahamba kumaliza ushahidi wake wa msingi, Lissu alianza kumuhoji katika hatua ya cross-examination.

    Lissu alimuuliza kama anajiona kuwa afisa mpelelezi mwenye uzoefu mkubwa.

    Shahidi: "Ni kweli."

    Lissu kisha akamuuliza kama alipanda cheo kwa kutungia watu kesi za uongo, kutesa watuhumiwa au kukosa uadilifu.

    Shahidi: "Sio kweli."

    Lissu pia alidai kuwa shahidi na timu yake walishirikiana na wahalifu waliofanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka jana.

    Shahidi: "Sio kweli."

    Lissu aibua tofauti kati ya ushahidi na maelezo ya shahidi

    Lissu alimwomba shahidi kueleza kama baadhi ya taarifa alizozitoa mahakamani zilikuwepo kwenye maelezo yake ya awali.

    Katika maswali kadhaa, shahidi alijibu:

    "Hayapo."

    Miongoni mwa mambo hayo ni maelezo kuhusu mafunzo yake ya polisi, kituo chake cha kwanza cha kazi, mafunzo maalumu aliyodai kuyapata mwaka 2006, kuwa mkufunzi na baadhi ya majukumu aliyowahi kufanya.

    Maelezo ya shahidi yapokelewa kama kielelezo D15

    Baada ya mabishano mafupi kati ya Lissu na upande wa mashtaka kuhusu utaratibu wa kutumia maelezo hayo, mahakama iliruhusu yaendelee kutumika.

    Maelezo hayo yalipokelewa na mahakama kama kielelezo D15.

    Baadaye Jaji Dunstan Ndunguru aliahirisha kesi hadi leo saa tatu asubuhi.

    Kesi inaendelea leo na Lissu anatarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi katika hatua ya kumuuliza maswali shahidi kupima uamini na kuonyesha migongano (cross-examination)

  7. Shahidi: "Baadhi ya watu walihamasika na kauli za Lissu"

    Mahamba pia alieleza kuwa katika upelelezi wao walipokea majalada kutoka mikoa mbalimbali, yakiwemo Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Ruvuma.

    Alisema baada ya kuyasoma, walibaini baadhi ya watu waliokuwa kwenye majalada hayo walikuwa wamehamasika na kauli za Lissu, na akaelekeza watafutwe na waandikwe maelezo kama mashahidi katika kesi hiyo.

    Shahidi azungumzia pia kukamatwa kwa Lissu

    Mahamba alisema Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, akiwa Mbinga mkoani Ruvuma, na kusafirishwa hadi Dar es Salaam siku hiyo hiyo.

    Alisema Lissu alifika Dar es Salaam Aprili 10 na kufikishwa kituo cha polisi, ambako alisomewa tuhuma lakini hakutoa maelezo, akisema atayatoa mahakamani.

    Baadaye, alisema, Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka.

    Shahidi azungumzia pia vitisho kwa mashahidi

    Mahamba pia alidai kuwa wakati upelelezi ukiendelea, baadhi ya mashahidi waliripoti kutishiwa iwapo wangetoa ushahidi dhidi ya Lissu.

    Alisema polisi walichunguza ujumbe na maoni kwenye mitandao ya Facebook, TikTok, Instagram na X, na baadaye kuwasiliana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhusu usalama wa mashahidi hao.

    Alisema hatua zilichukuliwa ili baadhi ya mashahidi hao walindwe.

  8. Lissu apinga tafsiri ya shahidi

    Wakati shahidi akieleza tafsiri hiyo, Lissu alipinga baadhi ya maswali ya upande wa mashtaka, akisema shahidi alikuwa akileta mambo ambayo hayapo kwenye shtaka linalomkabili.

    Lissu: "Mimi ni mshitakiwa wa uhaini, sikuwaambia watu wachome na kuchana kura. Haya maneno wanaokoteza na wanayaleta kwa mlango wa nyuma."

    Lissu aliwaomba majaji wasiruhusu ushahidi ambao, kwa mtazamo wake, ungeipeleka kesi kutoka kwenye shtaka la uhaini kwenda kwenye madai mengine ambayo hayamo katika hati ya mashtaka.

    Baada ya majadiliano, Jaji Dunstan Ndunguru alimruhusu wakili wa Serikali kuendelea na maswali.

  9. Shahidi: "Tulitazama video ya Lissu kwa zaidi ya saa mbili", Kwa ufupi - Kilichojiri Mahakani jana, Agosti 10

    Shahidi wa upande wa mashtaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, alieleza mahakama kuhusu namna timu yake ilivyofanya uchunguzi wa kauli za Tundu Lissu zilizohusishwa na shtaka la uhaini.

    Mahamba alisema baada ya kupokea taarifa kuhusu uchunguzi huo, aliwapangia maofisa majukumu mbalimbali, yakiwemo kukusanya taarifa, kuhoji na kumkamata mtuhumiwa.

    Alisema timu yake ilitazama video ya hotuba ya Lissu iliyokuwa imechapishwa kwenye YouTube na Jambo TV.

    Wakili wa Serikali: "Mliweza vipi kuiangalia?"

    Shahidi: "Tukiwa pale ofisini kuna kompyuta maalumu ambayo anaitumia Inspekta Michael, ndiyo tuliitumia kuangalia hiyo video."

    Alisema waliitazama video hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa zaidi ya saa mbili.

    Shahidi alisema kwenye video hiyo alimwona Lissu akiwa amevaa vazi rasmi la CHADEMA na akihutubia umma kwa Kiswahili.

    Mahamba alisema katika video hiyo alisikia Lissu akizungumza kuhusu kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uasi.

    Shahidi alidai kuwa kutokana na kauli hizo, timu ya upelelezi iliona Lissu alikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi na kuitisha Serikali.

    Alisema kauli hizo zilionyesha kile alichokitafsiri kama tishio kwa Serikali na kuvuruga uchaguzi.

  10. Lissu aendelea kumhoji shahidi wa 16 wa Jamhuri katika kesi ya uhaini

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, anaendelea leo, Jumanne Agosti 11, 2026, kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.

    Kesi hiyo, yenye Jalada la Jinai Na. 1 la mwaka 2025, ilianza kusikilizwa Mahakama Kuu baada ya Lissu kushtakiwa kwa shtaka la uhaini linalohusishwa na kauli zake kuhusu kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

    Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, akiwa Mbinga mkoani Ruvuma, na siku iliyofuata akafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kusomewa shtaka la uhaini pamoja na makosa mengine yaliyohusishwa na kauli zake.

    Kesi hiyo ilisimama kwa takribani miezi mitano tangu Februari 24, 2026, kabla ya kuanza tena jana, Agosti 10, chini ya Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.

    Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea kwa mfululizo kuanzia Agosti 10 hadi Septemba 7, 2026.

    Jana, shahidi wa 16, Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, alimaliza kutoa ushahidi wake wa msingi. Alieleza mahakama kuhusu upelelezi uliofanywa na polisi, ikiwemo namna walivyopitia video ya hotuba ya Lissu iliyochapishwa na Jambo TV na kauli walizodai zilihusisha kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uasi.

    Mahamba pia alieleza kuhusu majalada ya uchunguzi kutoka mikoa mbalimbali, kukamatwa kwa Lissu na madai ya vitisho dhidi ya baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka.

    Leo, Lissu ameanza hatua ya cross-examination, ambapo anamuuliza shahidi kuhusu uadilifu wake kama afisa wa polisi, uzoefu wake wa upelelezi na tofauti kati ya ushahidi alioutoa jana na maelezo yake ya awali.

    Endelea nasi hapa kwa taarifa za moja kwa moja kutoka Mahakama Kuu Dar es Salaam.

  11. Kutoka Mahakamani - Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu