WARIDI WA BBC: 'Niliambiwa ninapoteza muda kujitolea kusafisha mazingira'

s
Maelezo ya picha, Nimejitolea kutunza mazingira
    • Author, Martha Saranga
    • Nafasi, BBC SWAHILI
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Anaingia kwenye mitaro iliyojaa vumbi na takataka mbalimbali kama makaratasi, plastiki na majani, anasafisha kwa kujitolea bila kujali kuwa hakuna ujira wowote atakaolipwa baadae.

Kuona mazingira yaliyofurika takataka yakibadilika na kuwa safi inampa furaha na kujisikia vizuri kwamba amefanya jambo la maana kwa jamii yake.

Irene Mmbaga 20, anajivunia kujitolea kufanya usafi wa mazingira tangu akiwa mtoto.

Anasema ''nilipata msukumo kutoka kwa mama yangu.''

Mama yangu ni msafi sana.Wakati wote utakuta mazingira ya nyumbani kwetu ni safi.

Irene anasema alimaliza kidato cha nne mwaka jana mkoani Singida ambako aliishi na wazazi wake. Ni mwaka huu alipata msukumo wa kuchapisha mtandaoni maudhui yake akifanya usafi kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Kwa sasa anaishi Kigamboni jijini Dar es salaam na dada yake ambaye anamsaidia mahitaji yake madogo madogo.

'Nina malengo ya kusomea fani ya mazingira mwaka ujao. Ndoto yangu ni kufika katika chuo cha Oxfod nchini Uingereza kupata elimu ya juu zaidi' ili nifungue shirika la kutunza mazingira hapa nchini.

Kupitia utunzaji wa mazingira nitaweza kuhakikisha jamii yangu inakuwa salama kwa kizazi cha sasa na vijavyo.

Inahitaji kuwa na maarifa ili kuielimisha jamii zaidi, kwani bado baadhi ya watu hawana uelewa mzuri kuhusu utunzaji wa mazingira.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP, linasema hali ya utunzaji wa mazingira duniani kwa sasa iko katika hatua ya dharura na hatarishi, kwa kukabiliwa na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bioanuwai, na uchafuzi wa mazingira.

Ninafarijika jitihada zangu zinazaa matunda

s
Maelezo ya picha, Irene anasema anajivunia kuona jamii inapokea vizuri kampeni yake ya usafi katika wilaya yake Kigamboni
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili WhatsApp bofya kutufuatilia
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Irene anasema anafarijika kuona wazazi wake na familia wamepokea vizuri uamuzi wake wa kujitolea kufanya usafi wa mazingira.

Anakumbuka siku aliyoalikwa na mkuu wa wilaya wa Kigamboni Dalmia Mikaya ili kushiriki nae katika kampeni ya usafi wa mazingira ya fukwe jijini Dar es salaam, hatu ahiyo ilimpa nguvu na kuona kwamba jitihada zake sio bure.

''Ninakumbuka nilifika wa kwanza ufukweni na baadae walijitokeza watu wengi kuunga mkono zoezi hilo.''

Hatu ahii inanifanya kutowazingatia baadhi ya watu wanaofikiri kwamba ninapoteza muda, si kweli.

Ninatoa hamasa kwa jamii kutunza mazingira kwa usalama wetu sote.

Na hata watu wa afya waliniandikia katika maoni mtandaoni kuzingatia vifaa vya kutunza usalama wa afya yangu ninapofanya usafi.

Nilipokea vizuri ushauri wao na ninauzingatia.

Irene anasema anajivuni akutumia mitandao ya kijamii kuwafikia vijana na wasichana kuwapati ahamasa ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii nzima.

''Tunaweza kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha mambo mema yenye tija kwa jamii' kama ninavyofanya mimi.''

Irene anasema amesikia wito ukitolewa na serikali kwa jamii kujiandaa kufuatia ujio wa mvua za Elnino.

s
Maelezo ya picha, Irene anashauri mamlaka za mataifa ya Afrika mashariki kufanya suala la usafi wa mazingira kuwa endelevu.

Nchini Tanzania, Kenya na Uganda, Mamlaka zimekwishatoa tahadhari kuhusu mvua za El nino ambazo zitakuwa kubwa kuliko kawaida, na kueleza mikakati yao ya namna ya kukabiliana na athari zozote zitakazoambatana na mvua hizo.

Kufurika kwa mitaro, madaraja na miundo mbinu nyingine za majitaka ni moja kati ya changamoto ambazo hutatiza jamii katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Irene anasisitiza kwamba usafi wa mazingira pia ni moja ya maandalizi ya kudhibiti au kupunguza athari za mvua kubwa kama hizo zinazotarajiwa.

'Kuzibua mitaro,kukusanya takataka na kuzichoma moto,kufyeka majani na kuzoa takataka ni baadhi tu ya mambo ambayo ninafanya ili kuruhusu mitaro kupitisha maji ya mvua vizuri'

Itatusaidia pia kujiepusha na maradhi.

Irene anashauri mamlaka za mataifa ya Afrika mashariki kufanya suala la usafi wa mazingira kuwa endelevu.