Ukweli kuhusu alama za Freemasons na maana zake

H

Chanzo cha picha, FREEMASON

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 7

Mara nyingi kumekuwa na mijadala mikubwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu Freemasons, maarufu kama Wamasoni. Wengine wamekuwa wakiwahusisha na ushawishi mkubwa katika siasa, uchumi na taasisi mbalimbali duniani, huku wengine wakiamini kuwa mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo yanachangiwa na nadharia zisizothibitishwa.

Na katika siku tunazoishi, wanamuziki kama Madonna, Jay-Z na Kanye West wote wamewahi kushutumiwa kujihusisha na kundi la Iluminati ikiwemo matumizi ya alama au ishara ya Jicho.

Utumiaji wa alama hii umeonekana hata kwa wasanii wengine zaidi kama Bentham, Le Barbier, Thomson, Barton na wengine wengi hivyo basi sio ushahidi tosha kuwa alama ya jicho inahusishwa na ushetani lakini pia inaweza kuwa nembo kama yoyote ile.

Katika Afrika Mashariki pia, si jambo la ajabu kuona picha au alama zinazodaiwa kuhusishwa na Freemasons zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikiambatana na madai mbalimbali kuhusu siri za kundi hilo.

Lakini alama hizi zina maana gani kwa mujibu wa Freemasons wenyewe? Na zipi ni tafsiri zinazotolewa na wakosoaji wao?

Freemasons ni akina nani?

R

Chanzo cha picha, Amanda Ruggeri

Kwanza tujue kundi hili la Freemasonry ni jumuiya ya kindugu iliyoibuka kutoka vyama vya waashi wa mawe waliohusika na ujenzi wa makanisa na majengo makubwa barani Ulaya katika Zama za Kati. Kadiri muda ulivyopita, ilibadilika na kuwa jumuiya inayosisitiza maadili, maendeleo binafsi na shughuli za kijamii.

Wanachama wake husema wanamtambua Muumba Mkuu wa Ulimwengu, wanayemuita Great Architect of the Universe. Hata hivyo, jumuiya hiyo haimtaji kwa jina maalumu la dini fulani, jambo ambalo limekuwa likizua tafsiri tofauti kutoka kwa watu wa imani mbalimbali.

Jicho linaloona kila kitu

d

Chanzo cha picha, Alarmy

Moja ya alama zinazojulikana zaidi ni Jicho Linaloona Yote, linalojulikana pia kama Eye of Providence.

Kwa mujibu wa Freemasons, alama hiyo humaanisha kwamba Mungu anaona matendo na mawazo yote ya wanadamu na hivyo humkumbusha mwanachama kuishi maisha ya uadilifu.

Hata hivyo, wakosoaji wa Freemasons hutafsiri alama hiyo tofauti. Wapo wanaodai kuwa ni ishara ya mamlaka ya siri au hata nguvu za kishetani. Hakuna ushahidi wa kihistoria unaothibitisha madai hayo.

Kwa upande wa historia, alama ya jicho ilitumika katika sanaa ya Kikristo karne nyingi kabla ya kuhusishwa na Freemasons, ikiwa ni ishara ya uangalizi wa Mungu kwa wanadamu.

Kw upande mwingine , wasiounga mkono freemason wanasema jicho linalosema sio jicho la "Mungu" , wanachokiamini ni kwamba jicho hilo ni "jicho la shetani," ambalo kupitia shughuli zao, wanatafuta kutawala dunia, na kufanya "kila kitu kiwe chini ya utawala wao."

Herufi G

F

Chanzo cha picha, FREEMASON

Herufi G ni mojawapo ya alama maarufu katika Freemasonry.

Kwa mujibu wa jumuiya hiyo, herufi hiyo huwakilisha neno 'God' linalomaanisha Mungu, au Geometry, taaluma iliyokuwa muhimu kwa waashi wa kale.

Kwa mujibu wa kitabu cha "Explanation of Masonic Symbols" kinachoangalia alama za freemason kilichoandikwa na "Dr. Cathy Burns," , anasema, "herufi G inawakilisha Venus, moja ya sayari ulimwenguni. Na Venus huwakilisha kiungo cha kiume kwa wanaume, na pia ni moja ya majina ya shetani.

Freemason wanawajibika kuamini kwamba yupo kiumbe mkuu ambaye wanamwita "mbuni mkubwa wa ulimwengu," hata kama hawamwiti Mungu.

Lakini baadhi ya waandishi waliokosoa Freemasons wametoa tafsiri nyingine kuhusu alama hiyo. Tafsiri hizo hazikubaliki na Freemasons wenyewe na hazijathibitishwa kama msimamo rasmi wa jumuiya hiyo.

Pembetatu

d

Chanzo cha picha, Alamy

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Pembetatu pia ni alama inayojitokeza mara nyingi katika Freemasonry.

Kwa mujibu wa mafundisho yao, inawakilisha ukamilifu, usawa na hatua za maendeleo ya mwanachama katika kujifunza maadili na hekima.

Aidha, namba tatu ina nafasi muhimu katika historia ya Freemasonry kutokana na muundo wa mafunzo yake.

Ina degrees 33, na namba tatu inahusiana na nguvu na umuhimu wa mchakato wa kukua na kuelewa siri za ulimwengu.

Wanaamini kuwa namba tatu ni muhimu katika mchakato wa kujua ukweli, maana yake ikiwa ni mchakato wa hatua tatu.

Yaani kujitambua, kujifunza, na kutenda.

Walakini, kwa upande mwingine, namba 666 (ambayo inadaiwa ni namba ya mpinga-Kristo) pia inachukuliwa kama namba inayohusiana na nguvu za giza.

Ikitokea mara nyingi katika masuala ya kishetani na udhibiti wa ulimwengu.

Freemasons hutumia pembetatu kama alama ya ushirikiano na nguvu ya kutawala dunia kupitia hatua tatu,

Kutoka kwa mzee hadi kwa mwanafunzi, na hatimaye kuwa mstaafu mwenye hekima na nguvu.

Wakosoaji, kwa upande mwingine, wamekuwa wakihusisha alama hiyo na nadharia mbalimbali kuhusu makundi ya siri, ingawa madai hayo hayana ushahidi wa moja kwa moja unaokubalika.

Lakini kwanini watu hulinganisha alama hii na masuala ya ushetani?

s

Chanzo cha picha, The Uffizi Galleries)

Awali kabisa, alama hiyo ya jicho ilikuwa na Kikiristo na matumizi ya kwanza kabisa ya alama hiyo yanahusishwa na michoro ya dini hasa ya kumwakilisha mungu.

Ilibuniwa kama ishara ya uangalizi wa huruma ya Mungu juu ya wanadamu

Alama ya nyoka

Alama ya nyoka ni moja ya alama zinazotumika sana katika Freemasonry na miongoni mwa taasisi zinazohusiana nayo, kama vile Illuminati.

Hii ni alama ambayo ina mizizi katika Biblia na tamaduni za kale.

Katika kitabu cha Hesabu 21:8-9, Musa alitengeneza nyoka wa shaba na kuwaambia Waisraeli kuwa atakayeangalia nyoka huyo atapata uponyaji kutoka kwa sumu ya nyoka waliokutana nayo jangwani.

Nyoka kwao ni ishara ya nguvu na uponyaji, lakini pia inahusiana na hekima na ushawishi, kama vile ilivyokuwa kwa yule nyoka aliyejitokeza kwa Hawa katika Bustani ya Edeni.

Hapa nyoka anawakilisha busara na uwezo wa kumshawishi binadamu kufanya dhambi, lakini pia uwezo wa kutibu.

Freemasons wanapotumia nyoka kama alama, wanajivunia hekima, nguvu, na uwezo wa kubadilisha hali ya mambo.

Walakini, hii pia ina maana ya kutumia nguvu za siri kumshawishi na kumtawala mtu kwa kutumia ujuzi wa kipekee na udhibiti wa hali ya dunia.

Ikiwa ni pamoja na mifumo ya kifedha, kisiasa, na kidini.

Katika baadhi ya tafsiri za Freemasonry, nyoka huwakilisha hekima, maarifa na uwezo wa kubadilika.

Lakini kwa kuwa nyoka pia anatajwa katika simulizi la Bustani ya Edeni, baadhi ya wakosoaji huiona alama hiyo kama ishara ya udanganyifu au nguvu za giza. Maana hizi hutegemea zaidi imani na mtazamo wa mtu kuliko msimamo rasmi wa Freemasons.

Jicho la tatu

C

Chanzo cha picha, Gamma-Keystone via Getty Image

Baadhi ya watu pia hulihusisha Freemasonry na kile kinachoitwa "jicho la tatu", wakidai kuwa linaashiria uwezo wa kuona mambo yaliyofichika.

Hii ni alama inayohusiana na mtindo wa uangalizi, ambapo Freemasons wanaamini kwamba macho haya yanawakilisha uwezo wa kutawala na kuona mbali.

Hali ambayo inahusisha ufanisi wao wa kudhibiti mambo yanayoendelea.

Kwa maana nyingine, jicho hili linawakilisha uangalizi wa karibu wa kile kinachofanywa kwa siri, na mara nyingi hutumika kwenye alama za Freemasons na Illuminati.

Kama vile jicho linavyoona, ndivyo walivyo Freemasons, wanaweza kuona kile ambacho wengine hawawezi kuona.

Hii ina maana ya udhibiti wa kijamii, kifedha, na kiutawala wa watu, huku wakifanya mambo kwa siri, bila kuwaonyesha wengine.Kwa mujibu wa maandiko ya Freemasonry, ili kuwa mwanachama wa shirika hili, mtu anahitaji kuwa na uwezo wa kifedha.

Hii inamaanisha kwamba Freemasons huchagua watu wanaojiweza kifedha ili kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kwa njia bora na yenye nguvu.

Hii inahusisha ujenzi wa shule, hospitali, vituo vya watoto yatima, na miradi mingine ya kijamii ambayo inasaidia kuboresha jamii.

Hata hivyo, watafiti wa historia ya Freemasonry wanaeleza kuwa si alama ya msingi katika mafundisho rasmi ya Freemasons, bali mara nyingi imechanganywa na alama kutoka katika tamaduni na falsafa nyingine.

Alama ya dola ya Marekani

Moja ya mada inayozua mjadala mkubwa ni uwepo wa jicho ndani ya pembetatu kwenye The Great Seal ya Marekani, ambayo pia inaonekana kwenye noti ya dola moja.

Hali hiyo imechangia kuibuka kwa madai kwamba Freemasons wanadhibiti serikali ya Marekani au mfumo wa fedha duniani.

Wanaopinga Freemason wanaongeza kwa kusema mwandishi "Michael Benson" anasema kupitia kitabu chake cha "Inside Secret Societies" kwamba "alama ya jicho inayoonekana kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye pesa ya dola moja, inaonyesha ni namna freemason wanavyotawala Marekani na dhamira yao ya kutawala dunia, ikiwa tu yoyote anayetengeneza alama hiyo na kuchora michoro yao, anakuwa na asili ya Freemason.

Hata hivyo Freemason wenyewe wanapingana na dhana hiyo kuhusu utawala wao Marekani na kwenye pesa pamoja na dhamira inayosema kutawala dunia.

Hata hivyo, wanahistoria wanaeleza kuwa hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa alama hiyo kwenye dola ilikusudiwa kuwakilisha Freemasons. Serikali ya Marekani na Freemasons wamekuwa wakikanusha madai hayo kwa miaka mingi.

Kwa nini alama zao huzua mijadala?

D

Chanzo cha picha, Amanda Ruggeri

Freemasons hutumia alama nyingi katika shughuli zao, majengo na nyaraka zao. Kwa mujibu wao, alama hizo ni njia ya kufundisha maadili, hekima na historia ya jumuiya yao.

Lakini wakosoaji wao wanaamini baadhi ya alama hizo zinaashiria nguvu za siri au malengo ya kisiasa na kiuchumi. Hadi sasa, madai mengi yanayohusisha Freemasons na njama za kutawala dunia hayajathibitishwa kwa ushahidi huru.

Ukweli ni upi?

d

Chanzo cha picha, PA Media

Kwa zaidi ya karne mbili, Freemasons wameendelea kuwa miongoni mwa jumuiya zinazozua mijadala duniani. Wafuasi wao wanasema ni jumuiya ya maadili, udugu na huduma kwa jamii, huku wakosoaji wakiendelea kuhusisha kundi hilo na nadharia mbalimbali za siri.

Kilicho wazi ni kwamba alama nyingi zinazohusishwa na Freemasons zina tafsiri tofauti kulingana na chanzo kinachozieleza. Wakati Freemasons wenyewe huziona kama ishara za maadili, hekima na maendeleo binafsi, wakosoaji wao huzipa maana zinazohusisha ushawishi wa siri au njama za kutawala dunia.

Kutokana na tofauti hizo, ni muhimu kutenganisha ukweli uliothibitishwa na nadharia zisizo na ushahidi.

Alama peke yake haziwezi kuthibitisha uwepo wa njama au malengo ya siri bila ushahidi unaoweza kuthibitishwa.