Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Juve wanamtaka Reijnders, Silva kutua Barca

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wanaongoza orodha ya vilabu vya Italia vinavyomtaka kiungo Mholanzi wa Manchester City, Tijjani Reijnders (27), ambaye alijiunga na City akitokea AC Milan kwa pauni milioni 46.3 msimu uliopita. (Football Insider)
Kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, anataka mshambuliaji wa Denmark Will Osula (22) abaki klabuni hapo licha ya kuvutia ofa kutoka vilabu vingine. Osula ana thamani ya pauni milioni 30 na mkataba wake unamalizika Juni 2029. (Shields Gazette)
Crystal Palace wanamwona Andoni Iraola kama chaguo lao la kwanza kuwa kocha mpya baada ya Mhispania huyo kutangaza ataondoka AFC Bournemouth mwishoni mwa msimu. Hata hivyo, Chelsea pia wanamnyatia kocha huyo mwenye umri wa miaka 43. (Football Insider)
Real Madrid wanapanga kumbakiza mshambuliaji wa Brazil Endrick (19) katika majira ya kiangazi licha ya kusakwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea. (TeamTalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Ureno na Manchester City, Bernardo Silva (31), baada ya mchezaji huyo kutangaza ataondoka England mwishoni mwa msimu. (Barca Universal)
Kocha wa Coventry City, Frank Lampard, anataka kiungo wa zamani wa England Ross Barkley (32) kuwa usajili wake wa kwanza wa majira ya kiangazi, huku mkataba wa kiungo huyo na Aston Villa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu. (Alan Nixon via Give Me Sport)
Real Sociedad wanajaribu kumzuia kipa wa Hispania Alex Remiro (31) kujiunga na Barcelona kwa kumpa mkataba mpya. (Football Espana)









