Tetesi za soka Ulaya: Barcelona inamfuatilia Joao Pedro

Joao Pedro ndiye kinara wa mabao Chelsea msimu huu na anahitaji mabao matatu pekee kufikisha mabao 20, hatua itakayomfanya kuwa mshambuliaji wa kwanza wa kati wa The Blues kufikia rekodi hiyo tangu Diego Costa msimu wa 2016 hadi 2017.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao Pedro ndiye kinara wa mabao Chelsea msimu huu na anahitaji mabao matatu pekee kufikisha mabao 20, hatua itakayomfanya kuwa mshambuliaji wa kwanza wa kati wa The Blues kufikia rekodi hiyo tangu Diego Costa msimu wa 2016 hadi 2017.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Barcelona imeanza kumfuatilia mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Joao Pedro kama mbadala wa muda mrefu wa Robert Lewandowski anayetarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu.

Kwa mujibu wa Marca, nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amewekwa juu katika orodha ya wachezaji wanaotajwa kuziba pengo la mshambuliaji huyo wa Poland mwenye miaka 37. (Marca).

Aston Villa nayo inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji chipukizi wa Paris Saint-Germain na Senegal Ibrahim Mbaye, 18, huku klabu hiyo ya Ligi Kuu ikielekea kuwekeza zaidi kwa vijana dirisha hili la usajili. (Mail)

Barcelona pia inaweza kuelekeza nguvu zake kwa beki wa Tottenham na Argentina Cristian Romero iwapo jitihada za kumsajili Alessandro Bastoni kutoka Inter Milan zitagonga mwamba. (AS)

Beki huyo wa kati wa Italia mwenye miaka 27 ameonekana kuwa chaguo la kwanza, lakini Romero, 28, amewekwa kama mbadala muhimu.

Aston Villa iko tayari kumuuza winga wa England Tommi O'Reilly, 22, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Crewe Alexandra, huku Oxford United, Portsmouth na Huddersfield Town zikionesha nia ya kumsajili. (Mail)

Coventry City, iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, itashindana na Leeds United kuwania kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Lois Openda, 26. (Sport Witness)

Nyota huyo wa RB Leipzig kwa sasa anacheza kwa mkopo Juventus ya Italia.

Wawakilishi wa winga wa Newcastle na England Anthony Gordon wamekuwa katika mawasiliano na Bayern Munich kwa miezi kadhaa, huku kocha Vincent Kompany akiridhia uwezekano wa usajili wa mchezaji huyo mwenye miaka 25. (Florian Plettenberg)

Kiungo wa Middlesbrough Hayden Hackney, 23, anakaribia kucheza kwa Ligi Kuu, huku Brighton ikijiunga na Nottingham Forest katika kinyang'anyiro cha kumwania kumsajili. (Football Insider)

Nottingham Forest, Aston Villa na Crystal Palace zote zinapigania kumnunua kiungo chipukizi wa Rangers Bailey Rice, 19. (Teamtalk)

Aston Villa pia inatarajiwa kuongeza kasi ya harakati za kumwania kipa wa Manchester City James Trafford, 23, kama mbadala wa Emiliano Martinez iwapo ataondoka. (Football Insider)

Wakati huo huo, kocha wa Barcelona Hansi Flick, mwenye umri wa 61, anatarajiwa kuongeza mkataba wa miaka miwili, huku maelezo ya mwisho ya mkataba wake yakikamilishwa wiki ijayo.(Mundo Deportivo)

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid