Arsenal wamuweka Kenan Yildiz kwenye rada yao

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wanachunguza uwezekano wa wa kumnasa winga wa Juventus na timu ya taifa ya Uturuki, Kenan Yildiz, mwenye umri wa miaka 21. (Independent)

Atletico Madrid wanajaribu kukamilisha dili la kumnasa mshambuliaji wa Senegal, Nicolas Jackson, 25, kutoka Chelsea. (Marca - in Spanish)

Manchester City wanaongeza kasi katika harakati za kumnasa chipukizi nyota wa Brazil, Allan Elias (22), kutoka Palmeiras, huku mazungumzo kati ya pande hizo yakiendelea. (ESPN)

Manchester City wagonga mwamba katika harakati za kutaka kumsajili kiungo wa England Adam Wharton, 22, baada ya ombi lao kukataliwa na Crystal Palace. (Sun)

Tottenham wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 29, huku wakipanga hatua ya kumnasa nyota huyo wa Ufaransa. (Football Insider)

Inter Milan wameonyesha nia kubwa ya kumsajili Gabriel Martinelli, 25, ambao wanafikiria kuchukua hatua ya kumng'oa Arsenal (Corriere dello Sport - in Italian)

AC Milan ambao sasa wanapania kuimarisha safu yao ya ulinzi wameelekeza nguvu zao katika kumsajili beki wa kati, huku Ruben Dias wa Manchester City akiibuka kama mmoja wa walengwa wao wakuu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Beki wa kati wa Bayer Leverkusen na Burkina Faso, Edmond Tapsoba, 27, ameibuka kama mmoja wa mabeki wanaowindwa zaidi barani Ulaya, huku vigogo wa Ligi Kuu England, Manchester United, Tottenham na Newcastle zikivutiwa na huduma zake. (Teamtalk)

Beki wa Ufaransa Axel Disasi, 28, yuko hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Chelsea kwenda Crystal Palace. (Sun)

Barcelona bado hawajawasilisha ofa kwa Lautaro Martinez, lakini Inter Milan hawana mpango wa kumuuza nyota huyo wa Argentina, ambaye anaendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi chao. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Barcelona pia wanazingatia uwezekano wa kuwasajili washambuliaji wa Villarreal, Ayoze Perez wa Hispania, 33, na Georges Mikautadze wa Georgia, 25, huku wakiendelea kutathmini chaguo zao za kuimarisha safu ya ushambuliaji. (Marca - in Spanish)