Nchi 10 za Afrika ya jangwa la sahara zinazoagiza silaha kwa wingi

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa uagizaji wa silaha katika nchi za Afŕika umepungua kwa takriban -41%, kulingana na ŕipoti ya Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm (SIPRI), nchi za Afŕika ya Jangwa la Sahaŕa zimeongeza uagizaji wao.
Hapa tunawasilisha kwako nchi 10 za Afrika ya Jangwa la Sahara ambazo zinaagiza silaha nyingi zaidi, kama ilivyoorodheshwa na SIPRI.
Nchi kama Nigeria, Senegal na Mali ni miongoni mwa nchi zinazoagiza silaha nyingi kutoka nje, na kufanya sehemu ya kanda hiyo kufikia 13%, kulingana na SIPRI.
Nchi hizi 10 zilitokana na majibu yaliyotolewa na mtaalamu Dk. Mathew George, mkurugenzi wa SIPRI Arms Programme.
1.Nigeria
Nigeria inachukuliwa kuwa nchi inayoongoza kwa kuingiza silaha katika eneo hilo.
Takriban asilimia 16 ya silaha zinazoingizwa katika eneo hilo zinatoka Nigeria.
Aina za kawaida za silaha zinazoagizwa na Nigeria ni ndege za kivita, helikopta, magari ya kivita, meli na ndege zisizo na rubani.
Nigeria imenunua silaha kutoka vyanzo mbalimbali, sio nchi moja pekee.
Imenunua silaha kutoka Uturuki, Korea Kusini, China, Uholanzi, Ufaransa, Italia, Brazili, Marekani, Urusi, Afrika Kusini, Pakistan, Canada, Saudi Arabia, Austria na Malaysia.
Inachangia moja ya sita ya uagizaji wa silaha zote kutoka Afrika ya kusini na Jangwa la Sahara.
2. Senegal
Senegal imepiga hatua kubwa katika suala la uwezo wa kijeshi, baada ya kuwekeza milioni 298.46.
Ununuzi wake wa silaha unakadiriwa kuwa 8.8% ya mapato lake la taifa
Imekuwa muagizaji mkubwa wa pili wa silaha katika eneo hilo, ikinunua meli za majini na makombora kwa ulinzi wa pwani na uchunguzi wa mafuta na gesi baharini, pamoja na ndege kwa uchunguzi wa angani.
3.Mali
Vikosi vya kijeshi vya Mali vimeimrika kwa kasi tangu 2020. Mapambano dhidi ya makundi yenye silaha yamesababisha kuongezeka kwa nguvu za kijeshi za Mali.
Mali imekuwa nchi ya tatu kwa uagizaji wa silaha barani Afrika, hasa katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Iliwekeza milioni $272.17 katika silaha, ikiwakilisha 8% ya silaha zote zilizoagizwa kutoka Afrika.
Inafaa kuelezewa kwamba Mali imebadilisha ushirikiano wake wa kijeshi, na kuendeleza uhusiano wa karibu na Urusi kufuatia mzozo na Ufaransa.
Mali imeagiza nje magari ya kivita, kubeba askari, ndege, ndege zisizo na rubani, silaha nzito nzito, makombora na vifaa vingine.
4. Ethiopia
Kutokana na mvutano wa ndani unaotokana na mzozo wa Tigray, Ethiopia imezidi kununua ndege zisizo na rubani na kuzitegemea zaidi.
Imenunua ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, mizinga, magari ya kivita, wabeba askari, na ndege za mafunzo na za kivita.
Nchi ambazo Ethiopia imenunua silaha ni pamoja na Urusi, Uturuki, Iran, Marekani, Falme za Kiarabu na Bosnia.
Jumla ya thamani ya silaha zilizonunuliwa ni milioni $172.85.
5. Angola

Chanzo cha picha, Getty Images
Angola, ambayo imekuwa kwenye vita kwa muda mrefu, imekuwa ikinunua silaha kwa kasi kwa miaka mitano iliyopita.
Imenunua takriban 4.7% ya silaha zake. Angola inatanguliza ulinzi wa pwani na usimamizi wa anga.
Bidhaa ilizonunua ni pamoja na injini za ndege na boti za kijeshi. Ilitumia milioni $160.3 kwa silaha hizi. Nchi ilizonunua silaha hizi ni pamoja na Uhispania, Belarus, Ufaransa na Canada.
6. Kenya
Kenya inakabiliwa na hali ngumu ya usalama, haswa katika mipaka yake, na kuibuka tena kwa uhalifu na mashambulio ya kundi la Al-Shabaab, haswa kaskazini mashariki, pwani na Nairobi.
Ili kukabiliana na hili, Kenya imenunua silaha zinazokadiriwa kugharimu milioni 140.62.
Imenunua ndege za kubeba wanajeshi, makombora ya masafa marefu, ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB-2 na aina mbalimbali za helikopta, zikiwemo Hughes-500D.
Nchi ambazo imenunua silaha hizo ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, Israel, Uturuki, Marekani na Korea Kusini.
7. Mauritania
Ijapokuwa Mauritania ni miongoni mwa nchi zenye utulivu katika Afrika ya Sahel, nchi hiyo inakabiliwa na vitisho vya ugaidi kwenye mipaka yake ya kaskazini na mashariki hasa katika eneo la kati ya Algeria na Mali.
Mauritania imenunua silaha zenye thamani ya milioni $134.36.
Imenunua makombora ya kukinga vifaru, mgari ya kubeba askari, magari mengine, makombora ya kujihami , ndege zisizo na rubani za kijasusi, na magari ya kivita.
8. Burkina Faso
Burkina Faso imekuwa katika vita kwa miaka mingi na mashambulizi ya makundi ya kijihadi na kusababisha vifo vingi na kuhama kwa raia.
Burkina Faso ilinunua mabomu, makombora, magari ya kivita, silaha nzito, ndege, helikopta za mashambulizi, mizinga, ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB-2 na makombora mengine mengi.
Kwa jumla, ilinunua silaha kwa dola milioni 127.64.
9. Ivory Coast
Ingawa kusini mwa nchi hiyo kuna utulivu, Cote d'Ivoire inafuatilia kwa karibu mikoa yake ya kaskazini inayopakana na Burkina Faso na Mali, ambako kuna tishio la mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kijihadi.
Serikali imetumia dola bilioni 120.33 kununua silaha.
Ivory Coast imenunua helikopta nyepesi za AS-350 na H-125, helikopta za kivita, magari ya kivita, na boti za walinzi wa pwani.
10. Rwanda

Chanzo cha picha, Getty Images
Rwanda imeongeza uwezo wake wa ulinzi wa anga, na kununua silaha ambazo ni asilimia 3.5 ya jumla yake. Imetumia faranga milioni 118.73 za Rwanda kununua silaha hizi.
Aina za silaha zilizonunuliwa na Rwanda ni pamoja na helikopta za kivita, magari ya kivita, makombora ya kutungulia ndege na vifaa vingine.














