Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fedha zinazotokana na mauzo ya mafuta ya Iran zinaenda wapi?
Hatua ya Marekani ya kuidhinisha uuzaji wa mafuta ya Iran kupitia leseni inayofahamika kama "General X," inayotoa msamaha wa siku 60 imezua mjadala mkubwa mjini Washington. Uamuzi huo unaiwezesha Iran, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takribani miongo minne, kupokea mapato kutokana na mauzo ya mafuta yake.
Uidhinishaji huu ambao ambao haujaweka wazi maelezo ya masuala nayoibuka umezua maswali mengi. Tunachanganua maswala hayo na majibu yake katika taarifa hii
Leseni ya nini na lini?
Mara baada ya vita vya vya Iran ambayo Marekani imejiridhisha kuwa vilifikia malengo ya kijeshi lakini havikufikia malengo ya kimkakati yaliyowekwa—hadi wa leo—Marekani imefungua njia ambayo itawezesha mabilioni ya dola kuingia katika hazina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Chini ya "Leseni ya General X," "shughuli zote za kawaida na muhimu" za uzalishaji, uuzaji, utoaji, na uondoaji wa mafuta ya asili ya Iran na bidhaa zinazotokana na petroli inaruhusiwa hadi Agosti 21, 2026. Gesi asilia na LNG hazijajumuishwa moja kwa moja kwenye leseni hii, lakini kinachoondolewa ni uti wa mgongo wa Iran, bidhaa za mafuta na fidia kwa uharibifu uliosababishwa na vita vya Marekani na Israel dhidi yake.
Kifungu cha kwanza cha leseni kinaondoa shaka yoyote kuhusu asili ya bidhaa hizi na kubainisha kuwa leseni hii itajumuisha bidhaa zinazotengenezwa na taasisi zinazokabiliwa na vikwazo chini ya vifungu vya 560, 561 na 594 vya Ibara ya 31 ya Sheria za Marekani.
Kwa ufupi, Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta, Kampuni ya Kitaifa ya Kemikali ya Petroli, na mashirika mengine ya nishati ya serikali ya Iran yanaweza kutumia leseni hii katika suala la bidhaa, hata ikiwa kwenye orodha tofauti za vikwazo, zikiwemo silaha za maangamizi makubwa, haki za binadamu au ugaidi.
Bila shaka msamaha huu ni leseni ya mafuta, lakini ili ili kufikia utekelezaji wake bila kuondoa vikwazo, Marekani imelazimika kufungua kwa muda vifungo vingi vya kisheria vya vikwazo hivyo.
Kwa mantiki hiyo, Marekani imekubali kwamba katika siku hizi 60, sehemu ya mapato ya mafuta yanayokusanywa kupitia msamaha huu wa muda yatapitia mfumo ambao Washington yenyewe umewekea vikwazo, kwa mfano, kwa kuwa na nafasi katika mipango ya silaha za Iran au kwa uhusiano wake na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi.
Kiutendaji, popote ambapo vyombo hivi vilivyoidhinishwa na watu binafsi wamejumuishwa katika mfumo wa "kawaida na muhimu" wa mauzo ya mafuta, marufuku ya kigaidi na silaha pia huondolewa kwa muda.
Kwa mfano, Persian Petrochemical Industries Holding na matawi yake 39, ambayo yaliwekewa vikwazo kwa kutoa "msaada wa kifedha kwa Kambi ya kijeshi ya Khatam al-Anbiya," kitengo cha uhandisi na kiuchumi cha Walinzi wa Mapinduzi; na Kampuni ya Kitaifa ya Tangi ya Iran imesalia kwenye orodha ya Idara ya Hazina ya Marekani ya watu binafsi na mashirika yaliyowekewa vikwazo, lakini leseni ya muda ya biashara imetolewa kwa bidhaa zao za viwandani, yaani mafuta na kemikali za petroli.
Kwa mtazamo wa kisiasa, Marekani imetanguliza usitishaji vita, kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, na udhibiti wa bei ya mafuta duniani katika hatua hii, badala ya mshikamano wa kiishara wa muundo wa vikwazo.
Hakuna tena mazungumzo juu ya mpango wa kombora na wasiwasi juu ya ufadhili wake. Badala yake, Washington imeondoa vikwazo vingi chini ya mpango huo ili kuiridhisha Iran katika hatua ya kwanza ya makubaliano hayo na kuhakikisha kuwa mafuta ya Iran yanaweza kuuzwa bila ya benki na makampuni kuhofia vikwazo vya kisheria.
Tunazungumzia kiasi gani cha fedha?
Makadirio ya mapato ya siku 60 ya Iran kutoka kwa Leseni ya Geberal X yanatofautiana. Wakfu wa Ulinzi wa Demokrasia, ambao unaunga mkono sera ya shinikizo la juu zaidi dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na vikwazo vikubwa, unaweka kiasi hicho kuwa karibu dola bilioni 8.
Baadhi ya vyombo vya habari vinavyounga mkono utawala wa Trump, kama vile New York Post, vinakadiria kiasi hiki kuwa cha juu kidogo, kwa dola bilioni 10.
Bert Erickson, mtaalam wa masuala ya jiografia na mkurugenzi mkuu katika shirika la ushauri la hatari la Obsidian, aliiambia BBC Persian kwamba kulingana na uwezo wa uzalishaji wa Iran na mapipa yaliyo tayari kuuzwa, ikiwa mapipa milioni 2.3 hadi 2.4 ya mafuta yatauzwa kila siku kwa siku 60 zijazo, ikichukua $80 kwa pipa, Iran ingepata karibu dola bilioni 10, ambayo inaweza kwenda moja kwa moja kwenye benki kuu. Kulingana naye, hii ni faida kubwa ya fedha za kigeni kwa Iran.
Bw. Ericsson anasema kwa kuwa inachukua wiki 2 hadi 3 kusafirisha mafuta kutoka Ghuba ya Uajemi hadi Asia ya Mashariki, hiyo inasalia takriban siku 43 kwa shughuli na utoaji wa mafuta hayo: "Kampuni pia zinatakiwa kuhesabu hatari ambayo kibali chake huenda kilifutwa wakati wa uwasilishaji. Kwa hiyo katika wiki chache za kwanza, China na pengine mataifa kadhaa ya Kusini-mashariki mwa Asia huenda yakawa wanunuzi wakuu."
Mtazamo wa wengi huko Washington ni kwamba utaratibu huu wa Marekani utadumu tu hadi uchaguzi wa katikati ya muhula, ili soko la mafuta lisiwageuze wapiga kura kutoka kwa ufuasi wa Republican wa Bw. Lakini Bw. Erickson anaamini kwamba "kwenye karatasi hii ni idhini ya siku 60 lakini kiuhalisia, itaongezwa hadi makubaliano ya kina ya nyuklia yatakapofikiwa: "Tulipoteza siku 66 bila mpango. Hakuna kilichobadilika wakati Mlango wa bahari wa Hormuz ulipofungwa, ni usambazaji wa mafuta ulimwenguni tu ndio ulipungua na tukapoteza uwezo wetu wa kujadiliana. Sasa Iran itapata kibali hiki kila baada ya siku 60 la sivyo inafunga tena Mlango-Bahari wa Hormuz."
Kwa mtazamo wa utawala wa Trump, idhini hii itasaidia kupunguza bei ya mafuta duniani na inachukuliwa kuwa makubaliano ya kiuchumi ili kuiweka Iran kwenye meza ya mazungumzo. Wakati huo huo, rais wa Marekani anaweza kufuta msamaha huu wakati wowote na kila kitu kitarejea mahali ilipokuwa, kwa kuwa hakuna vikwazo vilivyoondolewa.
Fedha za mafuta zinaingia kwenye mifuko ya nani?
Sehemu nyingine muhimu ya aya hii ya pili ya idhini ni kwamba, Idara ya Hazina ya Marekani imesisitiza kwamba malipo yoyote ya ununuzi wa mafuta au bidhaa za petroli yafanywe kwa dola, na malipo haya yanaweza kuelekezwa kwa Iran, serikali ya Iran, au "mtu yeyote aliyeidhinishwa," upitia njia ya malipo ya moja kwa moja kwa Benki Kuu na benki za biashara za Iran zilizoidhinishwa; benki ambazo hapo awali zilikuwa zimetengwa kwenye mfumo wa malipo ya dola.
Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Iran iliwekewa vikwazo mnamo Oktoba 2020 na kupitia agizo la Donald Trump nambari 13224, ambalo pia linajumuisha Benki Kuu, miongoni mwa mambo mengine, "msaada wa kifedha kwa Kikosi cha Quds cha IRGC."
Kupitia msamaha huu wa sasa, Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Iran na Benki Kuu ya Iran zinaweza kuwa muuzaji na mpokeaji wa mapato ya mauzo, mtawalia, licha ya vikwazo vinavyohusiana na ugaidi.
Wakati huo huo, Kampuni ya Kitaifa ya meli ya mafuta ya Iran, ambayo pia uliwekewa vikwazo na utawala wa kwanza wa Donald Trump, inaweza tena kufanya mauzo ya mafuta ya Iran na meli yake ya mafuta, ndani ya kwa siku hizi 60.
Kampuni ya Petrochemical Industries Holding ya Ghuba ya Uajemi na matawi yake 39 yaliwekewa vikwazo karibu mwaka mmoja uliopita, mnamo Juni 2019, kwa "msaada wa kifedha kwa Kituo cha Khatam al-Anbiya," ambacho kinaitwa tawi la uhandisi na uchumi la IRGC. Kampuni hiyo inasemekana kumiliki asilimia 40 ya petroli ya Iran na asilimia 50 ya mauzo yake ya nje ya petroli, na kwa kuzingatia msamaha huu, inaweza kuwa muuzaji na mpokeaji wa mapato ya mauzo hayo.
Hakuna hata taasisi moja hizi au watu binafsi waliowekewa vikwazo watakaotolewa kwenye orodha ya vikwazo, lakini leseni ya muda ya muamala wa dola imetolewa kwa bidhaa zao.