Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iran na Marekani zinapopigana, kwa nini mshindi awe Erdogan?
Gazeti la Uingereza la The Telegraph, limekuwa likifuatilia matukio yanayoendelea nchini Uturuki, na jinsi rais wa taifa hilo Recep Tayyip Erdogan ametumia vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kujinufaisha.
Katika ripoti inayosema 'Erdogan ndiye mshindi halisi wa vita hivi' chapisho hilo la gazeti linasema Rais huyo amekuwa akikandamiza upinzani, bila yeyote kujua duniani.
Gazeti hilo linaelezea jinsi watu wengi waliangazia tukio ambalo polisi wa Uturuki walivamia makao makuu ya chama cha Republican peoples party, chama kikuu cha upinzani, kuvunja lango la ofisi za chama hizo na kurusha vitoa machozi.
Mwandishi wa chapisho hilo alisema "Hakuna yeyote anayeangazia au kuipa umakini kinachoendelea uturuki tangu vita na Iran kuanza. Erdogan anatumia kile kinachoendelea duniani kujinufaisha ndani nan je ya nchi"
Siku tisa tu baada ya vita vya Marekani na Iran kuanza, alianzisha tena kesi ya Ekrem Imamoglu, meya wa mji wa Instanbul, ambaye amekuwa mpinzani mkuu wa Erdogan.
Kiongozi huyo wa upinzani anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, kuongoza genge la majambazi, mashtaka ambayo anakanusha.
Mashtaka haya hayakulaaniwa na taifa lolote la magharibi hata kutoka chama cha Leba cha Uingereza ambacho kimekuwa na ukaribu na chama cha upinzani cha Uturuki.
Gazeti la The Telegraph, lilimnukuu mkurugenzi wa taasisi ya Middle East mjini Washington Gonul Tol, aliyesema, " mazingira ya sasa ni bora sana kwa Erdogan, na anatumia hali ya sasa kufanya anachotaka"
Uturuki imejunufaisha kuwa kuuza silaha kwa Iraq,ambayo ilinunua mifumo 20 ya ulinzi wa angani. Indonesia pia imenunua droni Zaidi ya 20 kutoka Uturuki, huku Porugal ikitarajiwa kupokea meli mbili za kivita kutoka Uturuki.
Tangu mwaka wa 2023, Uturuki imekuwa ikiathirika na mfumuko wa bei za bidhaa, huku umaarufu wa Erdogan ukipungua wakati ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa mwaka wa 2028. Ila uongozi wa Erdogan umedumu kutokana na kupata uungwaji mkono kutoka mataifa mengine.
Malengo ya Trump yakipungua huenda 'akashindwa'
Gazeti la The Guardian liliangazia makubaliano ya amani kati ya Marekani na Iran, na kuashiria jinsi msimamo wa Trump umeacha kuwa mkali kama awali.
Kulingana na Gazeti hilo, ukali wa awali wa Trump umepungua kutokana na uhalisia wa hali ilivyo kwa sasa.
Umakini wa Trump kutaka mlango bahari wa Hormuz kufunguliwa kunaashiria jinsi Iran imepata ushawishi na nafasi ya kufanya majadiliano na Marekani bila kutumia silaha.
Wachambuzi wengi wanasema kubadilika kwa msimamo wa Trump ni ishara ya kushindwa katika vita hivyo.
Wafuasi wa chama cha Republican wana wasiwasi kuwa Trump huenda akaafikia makubaliano na Iran kama yale yaliyoafikiwa na rais wa zamani Barrack Obama, ambayo Trump aliyafuta katika awamu yake ya kwanza ya uongozi.