Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Nimewapiga marufuku wanaume wengi kwenye kliniki yangu ya masaji kwa sababu ya tabia zao'
Baada ya miezi mitatu tu ya kufanya kazi kama mtaalamu wa masaji aliyehitimu, Maria aliamua kuchagua zaidi ni nani anayemtibu.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 38 anakataa kupokea wateja wapya wa kiume baada ya tabia isiyofaa kutoka kwa baadhi ya watu iliyomfanya ahisi hofu na kukosa raha.
BBC Scotland News imezungumza na baadhi ya matabibu wengine wa kike ambao wanasema wanakabiliwa na maombi ya mara kwa mara ya 'ziada', kuzomewa na kurudisha nyuma mipaka waliyoweka.
Viongozi wa sekta hiyo wanasema tabia ya kujamiiana ni tatizo la kawaida na mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kuweka kila mtu salama.
Maria, ambaye sasa anamiliki Tiba ya Massage ya Mikono katika Mashariki ya Ayrshire, aliiambia BBC kuwa huondoka kwenye chumba hicho ili kuwapa fursa wateja kujiandaa.
Wanavua nguo zao za juu lakini huvaa chupi zao na kulala kwenye meza ya masaji iliyofunikwa na blanketi.
Anasema mteja mmoja, ambaye tangu wakati huo amekataa kumuona, alikuwa akiomba kusalia utupu.
"Nilikuwa nikiingia ndani na alikuwa amelala chini akitazama chini ya meza akiwa ametandaza miguu na chupi iliyolegea sana," anasema.
"Tulizungumza juu ya kila kikao, na alisema, 'Ninaelewa lakini siipendi'.
Katika tukio tofauti, mwanamume huyo alijaribu kumwonyesha kinena kabla hajageuka na kumkumbusha kwamba hakuwa amefunzwa kutibu eneo hilo.
Pia kulikuwa na pongezi za mara kwa mara kwamba alikuwa akimsaidia "kumuweka hai".
"Ninapotazama nyuma sasa, naona jinsi alivyokuwa akijaribu kupata imani yangu na kupunguza umakini wangu."
Wakati mteja mwingine pia alibishana kuwa hataki kufunikwa, aliamua kuwa imetosha na akaanzisha biashara yake iliyolenga wanawake.
"Ilikuwa kama uzoefu wa jumla wa wanaume," anasema.
"Nusu saa kabla ya massaji, nilikuwa na mkazo sana kila wakati. Ningepitia tu matukio kuhusu kile kinachoweza kutokea na jinsi ninapaswa kufanya.
"Ninapowafanyia wanawake, ni tofauti. Sijisikii kutishiwa. Sisikii woga," anasema.
Bado ana wateja wawili wa kiume wa muda mrefu lakini hatakubali mtu yeyote mpya.
Anasema biashara yake sasa inaimarika polepole na Maria anasema anahisi furaha zaidi na anapenda sana kazi yake.
Dani alifunzwa kuwa mtaalamu wa masaji miaka sita iliyopita, baada ya kufutwa kazi ya kuuza mapipa.
Baada ya kufanya kazi katika baadhi ya spas kuu za Uskochi, alijiingiza mwaka jana na kuzindua biashara yake ya masaji - Drift by Dani.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 35, anayeishi Glasgow, atatibu tu wanaume anaowajua au 'waliotumwa kwake ' ikiwa wateja wengine wanawafahamu.
Anasema usalama ndio kipaumbele chake kikuu, haswa anapofanya kazi usiku sana akiwa peke yake.
Wakati fulani alimkataza mteja kwa kufanya mzaha kwa marafiki zake kwamba alikuwa akiwapa 'mwisho wenye furaha'.
"Inachukua mtu mmoja tu kuamini aina ya jambo kama hilo ambalo pia linaharibu sifa yangu," anasema.
"Nilimwambia haruhusiwi kurudi," anasema.
"Imenichukua muda kupata wateja, kujenga sifa hiyo kwa hiyo ni jambo zito wakati ambapo unapaswa kulinda usalama wako."
Dani na Maria wanasema wangependa kuona mafunzo sanifu zaidi kwa matabibu kuhusu jinsi bora ya kukabiliana na tabia zisizofaa na hatua za kuzingatia wanapoona hatari ..
Sekta ya masaji haina baraza linalosimamia kisheria nchini Scotland na hakuna sheria zinazodhibiti wataalamu wa masaji.
Maria pia anasema angependa kuona bodi inayoongoza ili wataalamu wa tiba waweze kuripoti matukio kama hayo.
"Hatuna pa kwenda isipokuwa polisi lakini wakati mwingine tunajiuliza. Je! inatosha?" Anasema.
Jenny Storey amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa miaka 25.
Anamiliki shule ya saluni na mafunzo na ni msemaji wa Jumuiya ya Uingereza ya Tiba ya Urembo & Cosmetology (BABTAC).
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 44 anasema kuna "taharuki" kuhusu jumbe zisizofaa kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo linapelekea wanawake wengi kuchagua kutowatibu wanaume.
"Ninasikia vibaya, ninahisi karibu kukata tamaa kwa sababu hutokea mara kwa mara," anasema.
"Matamshi kama vile, 'Je, unatoa mwisho wenye furaha' na aina mbalimbali za matamshi yasiyofaa kama hayo.
"Kama vile watu wengine wanachukulia kuwa mzaha , ni kudhalilisha kile tunachofanya kwenye tasnia na inaweza kuwafanya watu wahisi wasiwasi ," anasema.
Jenny anasema tatizo hilo si geni lakini halipaswi kuvumiliwa.
Katika kazi yake ya kwanza ya spa akiwa na umri wa miaka 19, anasema mteja alimfungia katika chumba cha matibabu pamoja naye.
Alifanikiwa kutoroka kupitia mlango mwingine lakini anasema tukio hilo linaunda jinsi anavyowafunza wafanyikazi wake sasa.
"Ni wazi haitokei kwa watu kila wakati na sio haki kuwapaka tope wanaume wote , kwa sababu tuna wateja wa ajabu wa kiume, lakini ni muhimu kuwaandaa na kile kinachoweza kutokea na jinsi ya kukabiliana nayo," anasema.
Jenny, ambaye anamiliki saluni ya Urban Retreat, hawazuii wanaume lakini anasema kuna wachache ambao huwafanya wahidi vibaya.
"Sijui kwa nini imeenea sana katika tasnia yetu kwa sababu tasnia nyingine yoyote, haiwezi kuvumiliwa," anasema.
Msemaji wa serikali ya Scotland alisema: "Kila mtu ana haki ya kujisikia salama mahali pake pa kazi na tabia iliyoelezwa haikubaliki kabisa.
"Yeyote anayepitia aina hii ya unyanyasaji anahimizwa kutafuta usaidizi."