Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Marcus Rashford kujiunga na Barcelona

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Ofa kutoka Saudi Arabia kwa winga wa Barcelona wa Brazil Raphinha, 29, huenda ikaongeza matumaini ya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kujiunga na klabu hiyo ya La Liga kutoka Manchester United. (Talksport)

Uchezaji mzuri wa Crysencio Summerville katika Kombe la Dunia akiwa na Uholanzi unaathiri matumaini ya Manchester United ya kumsajili, huku Paris St-Germain sasa pia ikimtaka winga huyo wa West Ham mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)

Manchester United hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 23 msimu huu wa joto, licha ya Barcelona na Atletico Madrid kumtaka. (TeamTalks)

Brighton wanafikiria kumpa Yasin Ayari mkataba mpya au kumruhusu kiungo huyo wa kati wa Sweden, 22, kuondoka huku kukiwa na hamu inayoongezeka kutoka kwa Newcastle. (Football Insider)

Arsenal wana matumaini Declan Rice anaweza kusaidia kumshawishi kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23, kujiunga nao kutoka Aston Villa msimu huu wa joto. (Mirror)

Orodha ya uhamisho ya Juventus majira ya kiangazi ni pamoja na mlinda lango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 33, na mlinzi wa Uingereza John Stones, 32, ambaye aliondoka Manchester City msimu huu wa joto. (Gazzetta dello Sport - In Italy).

Leeds wamewasilisha dau la ufunguzi la takriban £20m kwa Southampton kwa kiungo wa Ireland Kaskazini Shea Charles, 22. (Teamtalk),.

Mshambulizi wa Senegal Nicolas Jackson, 25, hatashinikiza kuhama Chelsea kwani analenga kumvutia meneja mpya Xabi Alonso katika maandalizi ya msimu mpya. (Football Insider)

Stade Rennais inakaribia kumnunua mshambuliaji wa Sunderland Mhispania Eliezer Mayenda, 21. (Foot Mercato - In French)

West Ham wanachunguza kumnunua beki Mwingereza Adam Webster, 31, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Brighton mwishoni mwa msimu. {Sun)

Iwapo Orlando City itamnunua mshambuliaji wa Mexico Santiago Gimenez, 25, kutoka AC Milan basi Waitaliano hao watamnunua mshambuliaji wa PSG wa Ureno Goncalo Ramos, 25. (Corriere dello Sport - In Itali).