Je, ni klabu gani zilizo na wachezaji wengi zaidi kwenye Kombe la Dunia 2026?

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City itakuwa na wachezaji 19 ambao mara ya mwisho waliwachezea mechi za vilabu wakishiriki Kombe la Dunia la 2026 katika eneo la Amerika Kaskazini.
Sio kwamba ni idadi kubwa zaidi ya klabu yoyote katika soka ya Uingereza, lakini pia ni kiasi cha juu zaidi cha klabu zote kote duniani.
Kuna timu 17 ambazo zina wachezaji 10 au zaidi kwenye Kombe la Dunia ambao walicheza mpira wa vilabu mara ya mwisho, ambapo watano kati yao ni wa Uingereza.
Arsenal wako katika nafasi ya tatu kwenye orodha hiyo pamoja na klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain, timu hiyo ikiishinda Arsenal katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi.
Vilabu vyote viwili vina wachezaji 17 ambao waliwawakilisha hivi majuzi wakishiriki michuano hiyo.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wako nafasi ya pili wakiwa na wachezaji 18, huku mabingwa wa Uhispania Barcelona wakiingia kwenye tano bora wakiwa na wachezaji 15.
Crystal Palace na Manchester United zote zina wachezaji 12 kila moja, sawa na Al-Hilal ya Saudi Pro League na Atletico Madrid ya Uhispania.
Liverpool (11) ni timu nyingine ya Uingereza ikiwa na wachezaji 10 au zaidi wanaoshiriki michuano hiyo. Timu ya Bundesliga Borussia Dortmund na Galatasaray kutoka Uturuki wako sawa.
Wanaokamilisha orodha ya timu zenye wawakilishi 10 au zaidi ni Slavia Prague (Jamhuri ya Czech), AC Milan (Italia), PSV Eindhoven (Uholanzi), Real Madrid (Hispania) na Fenerbahce (Uturuki).
Makala haya ni ya hivi punde zaidi kutoka kwa timu ya Niulize Chochote ya BBC Sport. Swali hili linatoka kwa Mark huko Elland.












