Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Barcola akubali kuhamia Liverpool

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Bradley Barcola, 23, amekubali kwa maneno kujiunga na Liverpool, lakini hakuna uhakika kuhusu uhamisho huo kwani kuna pengo kubwa kati ya klabu hizo mbili kuhusu ada. (L'Equipe)
Kuhamia kwa Barcola kwenda Liverpool kunaweza kusababisha mabingwa wa Ligue 1 PSG kujaribu kuipiku Real Madrid ili kumsajili winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, kutoka RB Leipzig. (L'Equipe)
Real Madrid haina nia ya kumuuza mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Vinicius Jr, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unamalizika msimu ujao wa joto, na wana imani kwamba atakubali mkataba mpya na klabu hiyo. (Sky Sports)
Vyanzo vya habari vya Newcastle United vinasisitiza kwamba klabu hiyo haiko kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mpango wa kumuuza nahodha wa Magpies, Bruno Guimaraes, 28, kwa Gunners na klabu hiyo ya Tyneside inatarajia mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kurudi mazoezini Ijumaa. (Northern Echo)
Bayern Munich hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji raia wa Colombia, Luis Diaz, licha ya Al-Hilal kuvutiwa naye, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amewaambia mabingwa hao wa Ujerumani kwamba anataka kubaki nao. (Sky Sports Germany)

Chanzo cha picha, Getty
Everton itadai takriban pauni milioni 70 kwa winga wa Senegal, Iliman Ndiaye, 26, huku Manchester United na Al-Hilal wakionyesha nia ya kumsajili. (Mirror)
Manchester United wako tayari kumruhusu mshambuliaji wao raia wa Uholanzi, Joshua Zirkzee aondoke na wako kwenye mazungumzo na Juventus kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Gazzetta dello Sport)
Nottingham Forest inakaribia kupata mkataba wa euro milioni 40 (pauni milioni 34) kumsajili beki wa kati wa Ivory Coast, Ousmane Diomande mwenye umri wa miaka 22 kutoka Sporting. (A Bola)
Coventry City wamekubali mkataba wa pauni milioni 22.5 kumsajili kipa Mwingereza, Carl Rushworth, 25, kutoka Brighton. (Telegraph)
Beki wa zamani wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu, mwenye umri wa miaka 27, anafanya mazoezi na Crystal Palace baada ya kuondoka Ajax msimu huu wa joto, lakini hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan kujiunga na Eagles. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Manchester City, Kalvin Phillips anakamilisha usajili wa mkopo kwa Sheffield United baada ya kuachwa nje ya orodha ya kikosi cha klabu hiyo kwa ajili ya ziara yao ya maandalizi ya msimu. (Mail)















