Duru ya kwanza ya mazungumzo ya Marekani na Iran yahitimishwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, amesema kuwa “hatua kubwa imefikiwa” kuelekea kumaliza mzozo nchini Lebanon.

Muhtasari

Skip Video and continue reading
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matagazo yetu ya leo. Kwaheri.

  2. Watu wauawa kwa ufyatuaji risasi shule Ufilipino

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Ufilipino wamewakamata wavulana wawili wanafunzi wa shule ya sekondari kufuatia tukio la ufyatuaji risasi shuleni lililowaua wanafunzi watatu na kuwajeruhi wengine saba.

    Shambulio hilo lilitokea katika shule ya sekondari katika mji wa Tacloban.

    Polisi wanasema huenda unyanyasaji wa shuleni ndio uliosababisha tukio hilo.

    Maafisa wamesema moja ya bunduki zilizotumika ilimilikiwa na afisa wa polisi, ambaye sasa amekamatwa.

    Silaha ya pili ilisajiliwa kwa kampuni ya ulinzi.

    Nchini Ufilipino, umiliki wa silaha unadhibitiwa vikali, lakini kuna soko kubwa la silaha zisizo halali.

  3. Vance asema Iran itawaruhusu wakaguzi wa nyuklia kurudi nchini humo

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vance amesema Iran itawaruhusu wakaguzi wa nyuklia kurejea nchini humo — hatua muhimu inayotakiwa na jumuiya ya kimataifa — huku mazungumzo na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) yakitarajiwa kuanza “mapema leo”.

    Makamu wa rais wa Marekani alisema kuwa hatua kubwa imefikiwa baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran ili kufikia makubaliano ya mwisho ya kumaliza vita, akirejelea kauli ya wapatanishi.

    Alisema pande husika zimejadili kufunguliwa upya kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na “uratibu wa kuepusha migogoro kwa ajili ya usitishaji mapigano wa kikanda”.

    Makubaliano ya maelewano yaliyosainiwa wiki iliyopita yanajumuisha ahadi ya kufungua tena mlango huo wa bahari na kusitisha mapigano “katika pande zote” — ikiwa ni pamoja na Lebanon.

    Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mapema Jumatatu, wapatanishi Qatar na Pakistan walisema kwamba baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo, Marekani na Iran wamekubaliana juu ya “njia itakayofuatwa kufikia makubaliano ya mwisho ndani ya siku 60”. Vance alieleza mazungumzo hayo kama yaliyoweka “msingi mzuri” kwa mazungumzo ya kufikia suluhisho la mwisho.

    Akizungumza nchini Uswisi Jumatatu asubuhi, makamu wa rais alisema suala la nyuklia ndilo “labda ambalo tunalifurahia zaidi kama Wamarekani”.

    “[Hii] ni hatua muhimu kwa wananchi wa Marekani na ya kwanza kuelekea kumaliza kabisa mpango wa silaha za nyuklia nchini Iran,” alisema.

    Soma zaidi:

  4. Guinea yapiga marufuku uuzaji wa dhahabu ghafi nje ya nchi

    .

    Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images

    Guinea imepiga marufuku uuzaji nje wa dhahabu isiyochakatwa katika juhudi za kukuza uchakataji wa ndani wa madini hayo ya thamani.

    Sera hiyo—iliyoanza kutekelezwa mara moja—inakuja baada ya Rais wa Guinea Mamadi Doumbouya kukutana na wazalishaji wa dhahabu wa viwandani na wachimbaji wadogo pamoja na wanunuzi, na inalenga kuimarisha uchumi na kuunda ajira zaidi.

    “Guinea sasa itahitaji dhahabu yake ichakatwe ndani ya nchi. Dhahabu ghafi haitatoka tena nje ya Guinea,” alisema, akiongeza kuwa nchi nyingine zimekuwa zikinufaika kiuchumi kwa kuchakata na kufanya biashara ya malighafi zao.

    Guinea ni mzalishaji wa sita kwa ukubwa wa dhahabu barani Afrika, kulingana na Baraza la Dhahabu Duniani (World Gold Council).

    Nchi nyingine za Afrika pia zimechukua hatua kama hizi kuongeza uchakataji wa ndani na kuongeza thamani katika sekta ya madini katika miaka ya hivi karibuni.

    Nchini Tanzania na Uganda, uuzaji nje wa madini yasiyochakatwa kama dhahabu na shaba tayari umepigwa marufuku, wakati Ghana inapanga kupiga marufuku uuzaji wa dhahabu ghafi ifikapo mwaka 2030.

    Zimbabwe, mzalishaji mkubwa wa lithiamu barani Afrika, imepiga marufuku uuzaji nje wa madini hayo yanayotumika kutengeneza betri kuanzia 2027.

    Dhahabu ni moja ya bidhaa kuu za mauzo ya nje za Guinea, ikiwa imesafirisha zaidi ya tani 22 za madini hayo katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kulingana na mamlaka.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Martha Karua yuko njiani kurejea Kenya baada ya kuzuiwa kuingia Uganda

    Wakili Mkuu na kiongozi wa Chama cha People's Liberation Party (PLP), Martha Karua, yuko njiani kurejea Nairobi baada ya kuzuiliwa na kunyimwa ruhusa ya kuingia Uganda mapema leo.

    Karua ameondoka Entebbe na anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) baadaye leo.

    Kulingana na timu yake, wakili huyo alizuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kabla ya kurejeshwa alikokuwa ametoka mara tu alipowasili Uganda. Hadi sasa, mamlaka za Uganda hazijatoa maelezo rasmi kuhusu sababu za uamuzi huo.

    Wanahabari wamealikwa kuhudhuria mkutano katika uwanja wa ndege wa JKIA, mara tu baada ya kuwasili kwake.

    Inatarajiwa kuwa Martha Karua atazungumzia mazingira yaliyopelekea kuzuiliwa kwake, kunyimwa kuingia nchini Uganda, pamoja na kurejeshwa kwake.

    Soma zaidi:

  6. Mahakama Kenya yampata Waziri wa Afya na hatia

    .

    Chanzo cha picha, Aden Duale

    Maelezo ya picha, Waziri wa Afya, Kenya Aden Duale

    Mahakama ya Kenya imempata Waziri wa Afya, Aden Duale, na hatia ya kudharau mahakama kwa kuruhusu ujenzi kuendelea katika kituo chenye utata cha karantini ya Ebola, licha ya kuwepo kwa amri za kusitisha mradi huo.

    Waziri huyo ameagizwa kufika mahakamani kesho (Juni 23) kwa ajili ya kusikilizwa kuhusu hatua za adhabu na hukumu, ambapo mahakama itaamua vikwazo vinavyostahili kutokana na kosa hilo la kudharau mahakama.

    Katika uamuzi uliotolewa Jumatatu, mahakama ilisema kuwa serikali ilishindwa kutekeleza amri zilizokuwa zimezuia kuanzishwa na kuendeshwa kwa kituo hicho hadi kesi ya kikatiba inayopinga mradi huo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

    Katika uamuzi wake, Jaji Patricia Nyaundi alikataa hoja ya Wizara ya Afya kwamba ushirikiano kati ya Kenya na Marekani kuhusu kituo hicho ulikuwa umesitishwa, na kwamba kazi zozote zilizoendelea zilikuwa zikifanywa na serikali ya Kenya pekee kama sehemu ya maandalizi ya kitaifa dhidi ya Ebola.

    Mahakama ilisema kuwa serikali haiwezi kukwepa kutii amri za mahakama kwa kubadilisha tu maelezo au sura ya mradi unaoendelea.

    “Anachojaribu kufanya mshtakiwa wa pili ni kukwepa utekelezaji wa amri kwa kubadili au kufafanua upya shughuli za ujenzi zinazoendelea,” alisema jaji huyo, akiongeza kuwa “amri ya mahakama haiwezi kuzuiliwa au kukwepwa kwa kutumia maneno ya hila au mbinu za ukwepaji.”

    Jaji huyo alibaini kuwa Waziri wa Afya alikuwa anafahamu kikamilifu amri za mahakama na alielewa kuwa zilihitaji shughuli zote za ujenzi katika eneo la Laikipia kusimamishwa. Hata hivyo, ujenzi uliendelea licha ya agizo hilo.

    “Mahakama huangalia kile kilichofanyika kwa uhalisia wake, si kwa maelezo yanayotolewa baadaye,” alisema jaji huyo. “Amri ya mahakama si mwaliko wa kutumia ujanja; ni agizo linalopaswa kutekelezwa.”

    Uamuzi huo unafuatia kesi iliyowasilishwa na taasisi ya kutetea haki za kikatiba ya Katiba Institute, ambayo ilidai kuwa maafisa wa serikali walipuuzia amri za mahakama kwa kuendelea na kazi za ujenzi wa kituo hicho na kwa kushindwa kuweka wazi nyaraka zinazohusiana na mradi huo.

    Hata hivyo, kuhusu suala la utoaji wa nyaraka, mahakama iliamua kuwa Katiba Institute haikuweza kuthibitisha kuwa kulikuwa na nyaraka nyingine zilizofichwa kutoka kwa mahakama au umma. Kwa hivyo, madai ya kudharau mahakama yanayohusiana na kutofichuliwa kwa nyaraka yalitupiliwa mbali.

    Pia unaweza kusoma:

  7. Mwanasheria wa Kenya Martha Karua azuiwa kuingia Uganda - shirika la mawakili

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wakili mkuu wa Kenya na Waziri wa Sheria wa zamani Martha Karua amezuiwa kuingia Uganda na kuamriwa kurejea nyumbani, kulingana na Chama cha Wanasheria cha Uganda.

    Karua alikuwa amewasili tu katika uwanja wa ndege wa Entebbe kuungana na timu inayomtetea wakili mwenzake kutoka Uganda Erias Lukwago, ambaye wamekuwa wakimwakilisha kiongozi wa upinzani aliyezuiliwa Kizza Besigye, anayekabiliwa na kesi ya uhaini.

    Lukwago mwenyewe alishtakiwa wiki iliyopita kwa kosa linalohusiana na uhaini, na kesi yake ya kusikilizwa ombi la dhamana ilikuwa imepangwa kufanyika leo Jumatatu.

    Taarifa kutoka ofisi yake ya utendaji inasema kuwa tangu alipowasili Entebbe asubuhi ya leo, Karua hajaweza kupatikana kwa mawasiliano, simu zake za mkononi zimezimwa na hakuna mawasiliano ya moja kwa moja yaliyopokelewa kuhusu alipo au hali yake.

    “Karua alikuwa amepangiwa kurejea Nairobi leo lakini bado hajapatikana kwa mawasiliano,” taarifa hiyo inasema.

    Kwa mujibu wa ofisi yake, aliwasili Entebbe asubuhi hii kwa ndege ya Kenya Airways akiwa pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Kenya, Charles Kanjama.

    Wawili hao walikuwa wakisafiri kuhudhuria uamuzi wa mahakama kuhusu ombi la kuachiliwa kwa dhamana la mwanasheria na meya wa zamani wa Jiji la Kampala, Erias Lukwago, ambaye anakabiliwa na shtaka linalohusiana na uhaini.

    Wakati Bw. Kanjama aliruhusiwa kuingia nchini, Bi. Karua anaripotiwa kuzuiliwa mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege. Kwa mujibu wa Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki, anatarajiwa kurejea Nairobi baadaye leo.

    Timu yake ya wanasheria imeeleza wasiwasi kuhusu hali yake ya kutowasiliana na mtu yeyote na kusema kuwa inatafuta ufafanuzi kutoka kwa mamlaka za Uganda.

    Mamlaka za Uganda bado hazijatoa taarifa yoyote kuhusu sababu za kuzuiliwa kwake au kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Makumi ya watu wameruhiwa, 18 hawajulikani walipo baada ya mlipuko katika kituo cha gesi Qatar

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Watu 54 wamejeruhiwa na 18 hawajulikani walipo baada ya mlipuko kutokea katika kituo kikubwa cha gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG) cha Ras Laffan nchini Qatar.

    Mlipuko huo ulitokea wakati wafanyakazi walikuwa wakianzisha tena shughuli zilizokuwa zimesitishwa kufuatia shambulio la Iran mwezi Machi.

    Mamlaka zilisema kuwa “ajali ya kiufundi” ilitokea katika kituo cha Barzan kinachosambaza gesi kwa matumizi ya ndani ya nchi, na kwamba hakukuwa na tishio kwa usalama wa umma.

    Mlipuko huo ulitetemesha madirisha na kuhusiwa katika maeneo ya kati ya Doha, jambo lililowatia hofu wakazi walioko zaidi ya kilomita 70 kutoka Ras Laffan.

    Wizara ya Mambo ya Ndani ya Qatar ilisema katika taarifa kwamba watu 54 wamejeruhiwa huku timu za uokoaji zikiendelea kuwatafuta watu 18 waliopotea.

    Timu za dharura zilipelekwa eneo la tukio, na moto uliosababishwa na mlipuko huo umeweza kudhibitiwa.

    Soma zaidi:

  9. Duru ya kwanza ya mazungumzo ya Marekani na Iran yamalizika kwa matumaini

    .

    Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock

    Mazungumzo ya kwanza kati ya Marekani na Iran kuhusu kufikia makubaliano ya mwisho ya kumaliza vita yamehitimishwa kwa kile ambacho wapatanishi, Qatar na Pakistan, wameelezea kuwa ni “hatua ya kutia moyo.”

    Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mapema Jumatatu, Qatar na Pakistan zilisema kwamba pande husika zimekubaliana kuhusu “mwelekeo wa kufuata kufikia makubaliano ya mwisho ndani ya siku 60.”

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, amesema kuwa “hatua kubwa imefikiwa” kuelekea kumaliza mzozo nchini Lebanon.

    Hati ya Makubaliano yaliyotiwa saini wiki iliyopita inajumuisha ahadi ya kusitisha mapigano katika maeneo yote ya mzozo, ikiwemo Lebanon, pamoja na kufunguliwa tena kwa mlango Bahari wa Hormuz.

    “Upatanishi wa Pakistan na Qatar umeleta maendeleo makubwa katika juhudi za kumaliza vita vya Lebanon,” Araghchi aliandika kwenye mitandao ya kijamii.

    Aliongeza kuwa mauzo ya nje ya mafuta na bidhaa zingine husika yameruhusiwa kuendelea, vikwazo vya usafirishaji vimeondolewa, baadhi ya mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa zimeachiliwa, na mpango mkubwa wa ujenzi upya na maendeleo umeanzishwa nchini Iran.

    Wajumbe wakuu wa Iran waliondoka kwenye mazungumzo yaliyofanyika nchini Switzerland siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, huku majadiliano ya kiufundi kati ya pande husika yakitarajiwa kuendelea.

    Taarifa ya pamoja ya wapatanishi ilisema kuwa njia maalum ya mawasiliano imeanzishwa ili kuzuia matukio na kutoelewana, kwa lengo la kuhakikisha usalama wa meli za kibiashara zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

    Soma zaidi:

  10. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran atangaza kusitishwa kwa vikwazo vya mafuta

    Ujumbe wa Iran

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kusitishwa kwa vikwazo vya mafuta na kuondolewa kwa mzingiro wa majini

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameripoti kuwa marufuku ya mauzo ya mafuta na bidhaa za petrokemikali nje ya nchi imesitishwa, huku mzingiro wa majini ukiondolewa.

    Aidha, Araghchi amesema kuwa baadhi ya mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa nje ya nchi zimeachiwa, na kwamba mpango mkubwa wa Iran wa ujenzi upya wa uchumi na maendeleo umeanza kutekelezwa.

    Waziri huyo alitangaza hayo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X.

    Pia aliishukuru Pakistan na Qatar kwa juhudi zao za upatanishi, akisema kuwa mazungumzo hayo "yameleta maendeleo makubwa katika kumaliza vita nchini Lebanon."

    Araghchi alikuwa akirejelea vifungu vya 1, 10 na 11 vya hati ya makubaliano ya maelewano kati ya Iran na Marekani, ambavyo utekelezaji wake ndio msingi wa mazungumzo yanayoendelea kuelekea kufikiwa kwa makubaliano ya mwisho.

    • Kifungu cha 1 kinasema kuwa Marekani, Iran na washirika wao watatangaza kusitishwa mara moja na kwa kudumu kwa operesheni za kijeshi katika maeneo yote ya mzozo, ikiwemo Lebanon.
    • Kifungu cha 10 kinahusu utoaji wa vibali na misamaha inayohitajika kwa usafirishaji wa mafuta, bidhaa za petroli na huduma zinazohusiana nazo, ikiwemo sekta za benki na usafiri.
    • Kifungu cha 11 kinahusu mali za Iran zilizozuiwa nje ya nchi, suala ambalo lilikuwa miongoni mwa vikwazo vikubwa katika mazungumzo hayo.

    Kwa sasa, Araghchi yuko nchini Uswisi kwa ajili ya duru ya mazungumzo yanayoendelea kati ya Iran na Marekani kuhusu makubaliano ya mwisho ya kumaliza mzozo na kupunguza mvutano wa kikanda.

    Unaweza kusoma;

  11. Netanyahu asema: “Sifanyi kila kitu ambacho Trump anataka”

    Trump na Netanyahu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa watu wengi hudhani yeye na Rais wa Marekani, Donald Trump, hufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu katika kila jambo, lakini si kweli kwamba kila mara wanaafikiana.

    Netanyahu aliongeza kuwa si wakati wote hufuata matakwa ya Marekani, akisisitiza kuwa Israel hufanya maamuzi yake kwa kuzingatia maslahi yake ya kitaifa.

    Kauli hiyo imekuja baada ya Trump pamoja na Makamu wa Rais wa Marekani, J. D. Vance, kumkosoa hadharani.

    Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Sera uliofanyika mjini Jerusalem, Netanyahu alisema hataruhusu Iran kupata silaha za nyuklia na kwamba majeshi ya Israel yataendelea kuwepo kusini mwa Lebanon kwa muda wowote utakaoonekana kuwa wa lazima kwa usalama wa nchi yake.

    Akihutubia Mkutano wa JNS mjini Jerusalem, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema:

    "Nchini Marekani, watu husema kwamba Rais Trump hufanya kila ninachomwambia afanye. Nchini Israel, watu hudhani kwamba mimi hufanya kila anachotaka Trump. Lakini hakuna kati ya mambo hayo yaliyo ya kweli."

    Netanyahu alitumia kauli hiyo kusisitiza kwamba yeye na Rais wa Marekani, Donald Trump, wanafanya maamuzi kwa kujitegemea kulingana na maslahi ya nchi zao, na si kwamba mmoja humwelekeza au kumdhibiti mwingine.

    "Sisi ni viongozi wa mataifa huru na yenye fahari. Wakati mwingine maoni yetu hutofautiana. Kila mmoja wetu anasimamia maslahi ya nchi yake. Mimi ninasimamia maslahi na usalama wa Israel."

    Netanyahu aliendelea kusema:

    "Mara nyingi mawazo yetu yanaendana. Lakini wakati mwingine hayaendani. Tunaheshimu mamlaka ya kila mmoja, uongozi wa kila mmoja, na dhamira ya kila mmoja kwa wananchi wake."

    Kauli hiyo ya Benjamin Netanyahu ilikuwa ikisisitiza kwamba licha ya uhusiano wa karibu kati ya Israel na Marekani, yeye na Rais wa Marekani, Donald Trump, hawakubaliani katika kila jambo na kila mmoja hufanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya taifa lake.

    Unaweza kusoma;

  12. Polisi wa Australia wakamata tani 2.7 za kokeni iliyofichwa kwenye maghala ya siri

    Kokeni

    Chanzo cha picha, Australian Federal Police

    Polisi wa Australia wamekamata tani 2.7 za kokeni, kiwango kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa nchini humo.

    Dawa hizo za kulevya, zenye thamani inayokadiriwa kufikia dola za Australia milioni 816 (takriban pauni milioni 433), ziligunduliwa Ijumaa katika vyumba vya siri vilivyofichwa chini ya sakafu bandia ndani ya makontena matatu ya usafirishaji kwenye eneo la Londonderry, magharibi mwa mji wa Sydney.

    Wanaume wawili wenye umri wa miaka 21 na 25 walikamatwa eneo la tukio baada ya kudaiwa kujaribu kuwatoroka polisi. Wameshtakiwa kwa kumiliki kiasi kikubwa cha dawa za kulevya zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria.

    Polisi wanasema kokeni hiyo ilisafirishwa kwa magendo kuingia Australia kupitia mji mdogo wa Midge Point, ulioko Kaskazini mwa jimbo la Queensland, kwa maagizo ya kundi la uhalifu uliopangwa.

    Wanaume hao wawili waliwekwa rumande baada ya kufikishwa mahakamani Jumamosi, na wanaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha gerezani iwapo watapatikana na hatia.

    Polisi walisema uvamizi huo ulikuwa sehemu ya operesheni iliyopewa jina la Operation Minjiang, ambayo ilianzishwa mwezi Mei baada ya kilo 40 za kokeni kupatikana zikielea majini karibu na sehemu ya kushushia boti katika Midge Point.

    Wiki iliyopita, watu wengine sita katika majimbo ya Queensland na New South Wales walikamatwa na kushtakiwa kutokana na uchunguzi ulioanzishwa kufuatia ugunduzi huo.

    Aidha, chombo kikubwa cha majini kinachoshukiwa kuwa sehemu ya mtandao wa usafirishaji wa dawa hizo kwa magendo kimezuiliwa katika visiwa vya Solomon.

  13. Trump: Lazima Iran isitishe vikosi washirika vyake nchini Lebanon

    Trump

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mara tu baada ya matamshi ya J. D. Vance kabla ya mkutano wa pande nne uliofanyika nchini Switzerland, Rais wa Marekani, Donald Trump, aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social:

    "Iran lazima mara moja izuie makundi yake washirika nchini Lebanon, ambayo yamekuwa yakifadhiliwa kwa kiasi kikubwa, kuendelea kusababisha matatizo. Ikiwa Iran haitafanya hivyo, tutaishambulia tena kwa nguvu zaidi kuliko tulivyofanya wiki iliyopita."

    Mazungumzo kati ya Iran na Marekani yanaendelea nchini Uswisi, yakihusisha pia uwepo wa wawakilishi kutoka Qatar na Pakistan.

    Lengo la mazungumzo hayo ni kutafuta makubaliano ya mwisho yatakayosaidia kupunguza mvutano wa kikanda, kusitisha mapigano yanayohusisha washirika wa Iran katika eneo hilo, na kujadili masuala ya usalama pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran.

    Unaweza kusoma;

  14. Starmer anatafakari mustakabali wake wa kisiasa huku shinikizo la kumtaka ajiuzulu likiongezeka

    Starmer

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, anaripotiwa kutafakari mustakabali wake wa kisiasa wakati kukiwa na shinikizo la kutaka atangaze kujiuzulu.

    Hali hiyo imekuja baada ya mshirika wake wa karibu katika Baraza la Mawaziri, Peter Kyle, kusema kuwa Waziri Mkuu alikuwa akizingatia "uhalisia wa kisiasa" kufuatia ushindi wa Andy Burnham katika uchaguzi mdogo wa Makerfield wiki iliyopita, ambao umefungua njia kwake kuwania uongozi wa Chama cha Labour.

    Baada ya matokeo hayo, Starmer amekabiliwa na wito mpya kutoka kwa baadhi ya mawaziri waandamizi wakimtaka kuweka wazi ratiba ya kuondoka kwake madarakani ili kumpisha Burnham.

    Katika pigo jingine kwa kiongozi huyo wa Labour, Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema kuwa Starmer "atajiuzulu kama Waziri Mkuu", huku akikosoa utendaji wake akiwa madarakani.

    Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema Starmer "ameshindwa vibaya" katika sera za uhamiaji na nishati, na akasisitiza tena wito wake wa kufunguliwa zaidi kwa uchimbaji wa mafuta katika Bahari ya Kaskazini.

    Trump aliongeza:

    "Namtakia kila la heri!"

    Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza iliiambia BBC kwamba viongozi hao wawili, ambao walikutana mara ya mwisho katika mkutano wa viongozi wa G7 nchini Ufaransa wiki iliyopita, hawakuwa wamezungumza mwishoni mwa wiki.

    Mara baada ya ushindi wa Burnham, Starmer aliendelea kusisitiza kwamba angepambana na jaribio lolote rasmi la kuondolewa kwenye uongozi wa chama.

    Hii ina maana kuwa kama kutakuwa na changamoto ya uongozi, uchaguzi wa ndani wa Labour utahitajika, ambapo wanachama wa chama pamoja na wafuasi wa vyama vya wafanyakazi vinavyoshirikiana na Labour wataamua mustakabali wa chama hicho.

    Unaweza kusoma;

  15. Kiongozi wa Hezbollah: Haiwezekani kwa majeshi ya Israel kuendelea kubaki nchini Lebanon

    Naim Qassem

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Kiongozi wa Hezbollah, Naim Qassem, alijibu kauli za Waziri Mkuu wa Israel siku ya Jumapili kuhusu majeshi ya Israel kuendelea kubaki katika eneo la usalama kusini mwa Lebanon, akisema:

    "Haiwezekani kwa majeshi ya Israel kubaki nchini Lebanon."

    Aliongeza:

    "Hakuna eneo la usalama kwa Israel. Tuna jeshi la taifa ambalo lina jukumu la kulinda nchi, na sisi tunashirikiana nalo."

    Kiongozi huyo wa Hezbollah alisema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni kwamba Israel ni "nchi adui" na kwamba "lazima iondoke nchini Lebanon."

    Pia alilaumu Marekani kwa kuendelea kuwepo kwa majeshi ya Israel nchini Lebanon, akisema kuwa Marekani inabeba jukumu la hali hiyo kuendelea.

    Unaweza kusoma;

  16. Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran inatarajiwa kuendelea usiku kucha

    Mohammad Bagher Ghalibaf alipuuza tishio la Donald Trump la kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya Iran.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mazungumzo kati ya Marekani na Iran ya kufikia makubaliano ya mwisho ya kumaliza vita yanatarajiwa kuendelea usiku kucha nchini Uswisi, afisa mwandamizi wa Marekani anayeshiriki katika mazungumzo hayo amesema.

    Mazungumzo hayo yalianza Jumapili, kufuatia makubaliano ya wiki iliyopita ya kufikia suluhu ndani ya siku 60.

    Jumapili usiku, mwanadiplomasia huyo wa Marekani alisema kwamba majadiliano yalikuwa yakijikita katika kufafanua baadhi ya ujumbe zilizokuwa hazieleweki kutoka Iran kuhusu kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, utekelezaji wa usitishaji mapigano kusini mwa Lebanon, pamoja na baadhi ya vipengele vya makubaliano ya nyuklia.

    Mapema, Rais wa Marekani, Donald Trump, alikuwa ametishia kuishambulia Iran ikiwa haitaisimamisha Hezbollah huku mapigano kati ya kundi hilo na Israel yakiendelea nchini Lebanon. Iran ilipuuzilia mbali onyo hilo, ikisema iko tayari kupigana.

    Afisa huyo alisema ujumbe wa pande zote mbili, ambao unakutana katika mji wa Lucerne nchini Switzerland, utatumia matokeo ya mazungumzo ya leo kama msingi wa mazungumzo ya kiufundi yatakayoendelea.

    Makubaliano ya awali ya wiki iliyopita yanajumuisha ahadi ya kufikia makubaliano ya mwisho ndani ya siku 60, pamoja na kusitishwa kwa mapigano katika maeneo yote ya mzozo, ikiwemo Lebanon, na kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

    Hata hivyo, tangu wakati huo kumeshuhudiwa kuongezeka kwa mapigano kati ya Hezbollah na majeshi ya Israel kusini mwa Lebanon, pamoja na mashambulizi ya anga ya Israel ambayo wizara ya afya ya Lebanon imesema yamesababisha vifo vya raia kadhaa, wakiwemo wanawake na watoto.

    Kuongezeka huko kwa mzozo kuliipelekea Marekani kutangaza usitishaji mpya wa mapigano kati ya Israel na Hezbollah siku ya Ijumaa.

    Lakini mapigano na mashambulizi ya anga yaliyoendelea yaliifanya Iran kutangaza Jumamosi kwamba imeufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, ingawa takwimu za ufuatiliaji wa meli zinaonesha kuwa vyombo vya majini vimeendelea kupita katika njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.

    Unaweza kusoma;

  17. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu hii leo.