Kenya yakosoa Saudi Arabia kwa kuweka vikwazo vya viza dhidi ya Wakenya
Serikali ya Kenya imekosoa uamuzi wa Saudi Arabia kuweka vikwazo vya usafiri dhidi ya Kenya, ikiwemo kusitisha utoaji wa visa kwa wasafiri kutoka nchini humo, ikisema hatua hizo ni kali kupita kiasi na haziendani na hali halisi ya mlipuko wa Ebola nchini Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo, na Wizara ya Afya ya Kenya imesema vikwazo hivyo havina msingi katika hali ya sasa ya mlipuko wa ugonjwa huo, ikisisitiza kuwa maambukizi ya Ebola yamedhibitiwa.
Wizara hiyo imesema mgonjwa wa kwanza aliyegunduliwa kuwa na Ebola, alikuwa ameambukizwa nje ya Kenya na kwamba mamlaka za afya zilifanikiwa kubaini na kufuatilia watu wote 135 waliokuwa wamekutana naye. Watu 118 waliwekwa karantini kwa ufuatiliaji.
Kulingana na Wizara ya Afya ya Kenya, visa vyote nane vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa vilihusishwa moja kwa moja na mgonjwa wa kwanza. Visa hivyo vinajumuisha wahudumu wanne wa afya na wanafamilia wanne wa karibu na mgonjwa wa kwanza.
Wizara hiyo imesisitiza kuwa hakuna maambukizi yaliyotokea nje ya kundi hilo na kwamba hakuna ushahidi wa ugonjwa huo kusambaa katika jamii. Kenya pia haijaripoti kisa kipya cha Ebola tangu Oktoba 19, 2026.
Soma pia: