Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe amemlaani Seneta wa Paraguay kama
"mtu asiye na maana" na asiyestahili wadhifa wake baada ya kutoa
matamshi kadhaa ya kibaguzi akidhihaki asili na elimu yake.
Celeste Amarilla, wa Chama cha Liberal Radical Party cha Paraguay,
alichapisha maoni kwenye X baada ya nchi yake kushindwa na Ufaransa katika
hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.
Mbappe alimjibu, "Madam Celeste Amarilla, wewe ni
mwanamke usiya na maana na usiyestahili wadhifa wako."
"Huiwakilishi Paraguay, nchi ambayo ni nzuri na ya heshima katika
mashindano yote."
"Kupitia uzembe wako na ubaguzi wako wa rangi, dunia nzima tayari
imesahau safari na juhudi za kihistoria ambazo wachezaji wako walifanya wakati
wa Kombe la Dunia, na kumpa nafasi mwanamke asiye na uwezo ambaye anatoa
taswira mbaya zaidi ya nchi yake."
"Sitawaruhusu watu kama yeye kueneza chuki na ubaguzi wa rangi
duniani kote."
Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) limetangaza mipango ya kuwasilisha
mashtaka ya jinai, likielezea matamshi ya Amarilla kama "ya kuchukiza
kabisa na yasiyokubalika".
Katika taarifa, FFF imesema: "Matamshi haya ni ya jinai na yana
hatia. Lazima yashtakiwe hapa kama mahali pengine popote. FFF inaripoti suala
hilo kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwa lengo la kesi za kisheria.
Serikali ya Paraguay imesema "inalaani na kukataa kauli"
zilizotolewa na Amarilla, ikisema "zinapingana na maadili na kanuni
zinazohimiza kuishi kwa amani na heshima."
Mbappe alifunga penalti ya ushindi katika kipindi cha
pili cha mchezo wa Jumamosi, na hivyo kufanikiwa kwenda robo fainali dhidi ya
Morocco jiji Boston siku ya Alhamisi.
Akiwa na mabao saba, Mbappe ndiye mfungaji bora wa pamoja katika
mashindano ya mwaka huu, sawa na Lionel Messi wa Argentina na Erling Haaland wa
Norway.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliandika: "Goli jingine kwa
Kylian Mbappe. Dhidi ya ubaguzi wa rangi wakati huu. Namuunga mkono kwa kila
kitu."
Matamshi ya Amarilla yamekuja baada ya yale ya kipa wa zamani wa
Paraguay Jose Luis Chilavert, ambaye alisema kuelekea mechi hiyo kwamba timu
yake ya taifa itacheza na "kikosi kutoka Afrika".
Matamshi hayo pia yalisababisha jibu kutoka kwa rais wa FFF Philippe
Diallo, ambaye alisema Chilavert "anatia aibu".
"Ninalaani kwa nguvu zote matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Jose
Luis Chilavert dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa, ambayo yanadhoofisha maadili
na heshima, udugu, na utofauti katika soka letu," Diallo alisema.
"Kama alikuwa kipa mzuri hapo awali, mtu huyu sasa amegeuka kuwa
fedheha."