Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Arsenal yamtaka mchezaji wa DRC Congo Aaron Wan Bissaka
Arsenal imemwongeza beki wa kulia wa West Ham na DR Congo Aaron Wan-Bissaka, 28, kwenye orodha yao ya wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya Ben White, iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ataondoka msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Tottenham itajaribu kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth na Ufaransa Eli Junior Kroupi kwa dau la pauni milioni 85 , licha ya Cherries kusisitiza kwamba mchezaji huyo wa miaka 20 hauzwi. (Talksport)
Atletico Madrid itatafuta kujaza nafasi ya Antoine Griezmann na nyota wa zamani wa Liverpool Mohammed Salah, 33, ambaye kwa sasa yuko kwenye Kombe la Dunia na Misri. (Fichajes - In Spanish )
Liverpool wamejiunga na Chelsea na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa West Ham, Mholanzi, Crysencio Summerville, 24. (Caught Offside)
Moja ya kazi za awali za Andoni Iraola kama kocha wa Liverpool itakuwa ni kusimamisha nia ya kutaka kusajiliwa na Old Trafford na Ulaya ili kumsajili kiungo wa kimataifa wa Mexico mwenye umri wa miaka 17, Gilberto Mora, ambaye anacheza soka lake la ndani kwa Klabu ya Tijuana. (Teamtalk)
Chelsea itampa mkataba mpya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 19, Jesse Derry, 19, ili kusimamisha nia ya kusajiliwa na Bayern Munich. (Football Insider,)
Wolves wana nia ya kumsajili kiungo wa kati Niko Sigur, 22, kutoka Hadjuk Split baada ya kuchezea Kombe la Dunia kwa Kroatia. (Sky Sports,)
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Dani Carvajal, 34, anaweza kujiunga na Deportivo La Coruna aliyepanda daraja hivi karibuni baada ya kuondoka Real Madrid. (Fichajes - In Spanish)