- “Patrice Lumumba” – shabiki wa DRC alisimama kama sanamu kushabikia ‘Leopards’
Mechi 104
zinatarajiwa kukamilika usiku wa Jumapili Julai 19 ambapo mbivu na mbichi
itajulikana wazi kuhusu ni nani Bingwa wa Kombe la Dunia katika Soka mwaka huu
wa 2026.
Na huku
Lamine Yamal wa Uhispania akijiandaa kukabiliana na mmoja wa wachezaji bora
duniani Lionel Messi, wengi watakumbuka mengi yaliyotokea kwenye maeneo ya
mashabiki kuketi, au hata nje ya uwanja lakini yalikuwa na uhusiano mkubwa na
kabumbu iliyokuwa ikisakatwa.
Haya hapa
matukio yaliyowavutia wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii:
“Patrice Lumumba”, Shabiki wa Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo Michel Kuka Mbolandinga anayefahamika kama ‘Lumumba Vea
– au sanamu iliyohai,’ alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliokuwa uwanjani
na hata waliomtazama kwenye mitandao ya kijamii hasa wakati ambapo timu ya
taifa ya DRC ilipokuwa ikicheza mechi zao za makundi, awali kwenye michuano ya
mwaka huu.
Alipigwa
picha akiwa amesimama bila kusonga kwa muda wote ambao mechi zilikuwa
zikichezwa, akiwa ameinuwa mkono wake wa kulia na akiwa amevalia suti yenye
rangi za bendera ya taifa hilo.
Hatua hiyo
inafanana na sanamu ya kumuenzi aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Patrice
Lumumba ambayo ipo katika mji mkuu Kinshasa.
2: Ndugu mdogo wa Lamine Yamal avutia wengi
Mtangazaji
wa soka wa BBC Kelly Cates alimtaja kijana huyo mdogo kama mtoto mrembo
aliyewavutia wengi kwa uzuri wake. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu –
Keyne – ni kaka yake mdogo mshambulizi wa Uhispania Lamine Yamal – mwenye umri
wa miaka 19.
Na japo
ndugu yake mkubwa ni mchezaji maarufu wa Klabu ya Barcelona nchini Uhispania,
Keyne amejipatia umaarufu wa aina yake aliporekodiwa akijaribu kucheza mchezo
wa gofu, na kukerwa na kutokuwa na uwezo wa kuupiga mpira vyema miongoni mwa
mambo mengine.
Katika mechi
kati ya Ubelgiji na Uhispania, kijana huyo mdogo alipigwa picha ya video akiwa
amepakatwa huku akitabasamu kwa kuwa Uhispania ilikuwa imefuzu kuendelea mbele
baada ya kuicharaza Ubelgiji.
3. Haaland na
Bellingham wakijitokeza kama marafiki
Licha ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England kwa misimu kadhaa, Erling Haaland anaonekana hakuwa amepata umaarufu mkubwa nchini Marekani na Canada hadi sasa.
Hata hivyo, mambo yalibadilika kabisa msimu huu wa kiangazi baada ya mitandao ya kijamii kumuenzi mshambuliaji huyo wa Norway na Manchester City kupitia wimbi la 'meme' zilizotawala TikTok na Instagram, na kumjengea kile kilichoonekana kama ulimwengu wa kipekee mtandaoni.
Kulikuwa na mengi ya kuvutia mashabiki, huku Haaland akionekana pamoja na mwigizaji Channing Tatum. Baadaye akafunga mabao saba, akapata maelfu ya wafuasi wapya kwenye mitandao ya kijamii.
Erling
Haaland na Jude Bellingham wakikumbatiana baada ya England kuibuka na ushindi
dhidi ya Norway mjini Miami.
Mwanamitandao
maarufu IShowSpeed, anayejulikana kwa kuruka sarakasi za nyuma (backflips),
kubweka kwa utani na kuvaa jezi zilizogawanywa rangi mbili, atatumbuiza kwa
wimbo wake wa (World Cup) Champions katika sherehe ya kufunga mashindano kabla
ya fainali ya Jumapili.
Mshawishi
huyo wa mitandao ya kijamii ambaye pia hurusha matangazo yake moja kwa moja amekuwa
mmoja wa watu walionufaika zaidi na Kombe la Dunia la mwaka huu, akiongoza
vipindi vya kutazama mechi mubashara mtandaoni akiwa ndani ya viwanja wakati wa
michezo.