Mapigano makali Yemen: Pakistan yasema "itafanya kila iwezalo" kuilinda Saudi Arabia

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Msemaji wa jeshi la Pakistan amesema nchi yake "itafanya kila iwezalo" kuilinda Saudi Arabia, wakati ufalme huo ukikabiliwa na ongezeko la mashambulizi kutoka kwa kundi la Ansar Allah la Houthi nchini Yemen.
Houthi wamesema wiki hii kwamba maeneo wanayodhibiti nchini Yemen yameshambuliwa tena kwa ndege za kivita za Saudi Arabia, huku Riyadh ikiwatuhumu kwa kujaribu kulenga mji mtakatifu wa Mecca kwa kutumia droni.
Msemaji wa jeshi la Pakistan, Ahmed Sharif Chaudhry, alisema katika mahojiano na Arab News yaliyochapishwa Alhamisi: "Tutakwenda mbali zaidi katika kuhakikisha usalama wa Misikiti Miwili Mitakatifu na Ufalme wa Saudi Arabia."
Chaudhry aliongeza: "Pakistan iko imara upande wa Saudi Arabia, kidiplomasia na kijeshi."
Mwezi uliopita, Pakistan, Saudi Arabia na Uturuki zilitia saini makubaliano yanayojulikana kama "Mkataba wa Mecca wa Ulinzi wa Pamoja", ambao unazitaka nchi hizo tatu kuzingatia kanuni ya ulinzi wa pamoja endapo moja kati yao itashambuliwa.
Hata hivyo, makubaliano hayo hayamaanishi kwamba nchi yoyote kati ya hizo tatu itaingia moja kwa moja katika vita vyovyote vitakavyoanzishwa na mojawapo ya nchi wanachama.
Unaweza kusoma;














