Moja kwa moja, Urusi yashambulia treni ya Ukraine muda mfupi baada ya Boris Johnson na maafisa wakuu wa Ulaya kuondoka kituoni

Droni ya Urusi imegonga treni karibu na mpaka wa Ukraine na Poland muda mfupi baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, na maafisa wakuu wa usalama wa Ulaya kupita eneo hilo.

Muhtasari

  • Bayern Munich wamnyatia Florian Wirtz wa Liverpool
  • Urusi yashambulia treni ya Ukraine muda mfupi baada ya Boris Johnson na maafisa wakuu wa Ulaya kuondoka kituoni

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Saudi Arabia yaonya raia wake katika maeneo mawili yanayopakana na Yemen

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Wahouthi

    Shirika la Ulinzi wa Raia la Saudi Arabia lilitoa maonyo siku ya Jumapili kuhusu mashambulizi yanayowezekana katika maeneo mawili yanayopakana na Yemen.

    Maonyo haya, yaliyotolewa kwa ajili ya mji wa Abha na eneo linalozunguka mji wa Khamis Mushait, yalifutwa haraka.

    Maonyo hayo yalitolewa muda mfupi baada ya vyombo vya habari vya Houthi kuripoti mashambulizi ya Saudi Arabia kaskazini mwa Yemen, karibu na mpaka.

    Mgogoro kati ya Houthi wanaoungwa mkono na Iran na vikosi vya serikali ya Yemen vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia umeongezeka tangu wiki iliyopita.

    Baada ya Houthi kutangaza kizuizi cha majini mnamo Julai 20 kujibu kizuizi cha Saudi Arabia, mgogoro wao na vikosi vya serikali ya Yemen umeongezeka.

    Wiki iliyopita, Houthi walichukua udhibiti kamili wa pwani ya magharibi ya Bahari Nyekundu na Mlango-Bab al-Mandab katika shambulio kubwa, na kuwafukuza wanajeshi wa serikali.

  2. Bayern Munich wamnyatia Florian Wirtz wa Liverpool

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bayern Munich wanafuatilia kwa karibu kiungo wa Ujerumani Florian Wirtz, mwenye umri wa miaka 23, katika klabu ya Liverpool. (Teamtalk)

    Liverpool inaweza kuvunja rekodi yake ya usajili kwa kumsajili mshambuliaji wa Brazil wa Bournemouth, Rayan, mwenye umri wa miaka 20, msimu ujao. Timu hiyo italazimika kulipa pauni milioni 130 iwapo itaamua kutumia kipengele cha mkataba kinachomruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa kiasi hicho. Kifungu hicho kitaanza kutumika mwaka 2027. (Football Insider)

    Liverpool wana kipengele cha kulipa euro milioni 55 (£47.2m) ili kumsajili moja kwa moja beki wa Uruguay Ronald Araujo, mwenye umri wa miaka 27, baada ya kumchukua kwa mkopo kutoka Barcelona. (Fabrizio Romano via Caught Offside)

    Juventus haiko tayari kumuuza Pierre Kalulu katika dirisha la usajili la Januari, licha ya Manchester United na Liverpool kuhusishwa na uwezekano wa kumsajili beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26. (Manchester Evening News)

    Kocha wa Borussia Dortmund, Niko Kovac, ameondoa uwezekano wa klabu hiyo kumsajili tena winga wa zamani wa Manchester United, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa hana klabu. (Mirror)

    Wakala wa Sancho amefanya mazungumzo na klabu kadhaa za Ligi Kuu England kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na moja ya klabu hizo. (Football Insider),

    Borussia Dortmund imeungana na Manchester United kuonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Leicester City, Louis Page, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiwa imetuma maskauti kumfuatilia Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 18. (Teamtalk),

    Klabu za Championship pamoja na Celtic zinafikiria kumsajili beki wa Liverpool na timu ya taifa ya vijana ya England, Luke Chambers, mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

    Aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan, Piero Ausilio, anatarajiwa kujiunga na Tottenham, ambayo imempa Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 54 nafasi ya kazi kuanzia dirisha la usajili la Januari. (Gazzetta)

    Pia unaweza kusoma:

  3. Urusi yashambulia treni ya Ukraine muda mfupi baada ya Boris Johnson na maafisa wakuu wa Ulaya kuondoka kituoni

    .

    Droni ya Urusi imegonga treni karibu na mpaka wa Ukraine na Poland muda mfupi baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, na maafisa wakuu wa usalama wa Ulaya kupita hapo.

    Hakuna majeruhi walioripotiwa kufuatia shambulio hilo huko Yahodyn, ambalo lililenga injini ya treni hiyo. Abiria wote walikuwa wameshaondolewa, kulingana na maafisa wa Ukraine.

    Johnson na washauri wengine wa usalama wa kitaifa wa Ulaya, akiwemo Jonathan Powell wa Uingereza, walikuwa wamepita kwenye njia hiyo hiyo kwa treni tofauti walipokuwa wakirejea kutoka kwenye mkutano mjini Kyiv.

    Urusi ilisema ilishambulia "miundombinu ya reli" magharibi mwa Ukraine, lakini kampuni ya reli ya serikali ya Ukraine, Ukrzaliznytsia, ilisema kuwa "kuna uwezekano mkubwa kuwa lengo la droni hiyo lilikuwa treni ya kidiplomasia".

    Katika taarifa, ilisema treni hiyo "ilikuwa imeondoka kituoni mapema kuliko ilivyotarajiwa kutokana na mabadiliko ya ratiba... kufuatia vitisho vya mara kwa mara vya mashambulizi ya Urusi".

    Pia ilisema agizo la kuwaondoa abiria kwenye treni iliyoshambuliwa lilitolewa "dakika 15 tu" kabla ya shambulio hilo lililofanywa na droni ya Urusi inayotumia injini ya ndege.

    Mamlaka ya reli pia ilisema kuwa aliyekuwa mkuu wa CIA, David Petraeus, alikuwa ndani ya treni nyingine katika kituo cha Yahodyn wakati wa shambulio hilo la droni.

    Maafisa wa Ukraine na Poland walisema droni hiyo ya Urusi ilishambulia eneo lililoko umbali wa kilomita 2 kutoka mpaka wa Poland.

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

  4. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja