Bernie Sanders kumpigia kura Clinton

Sanders na Clinton
Maelezo ya picha, Sanders na Clinton
Iliyochapishwa

Seneta wa Marekani Bernie Sanders amesema kuwa atampigia kura mpinzani wake katika chama cha Democrats Hillary Clinton katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.

Wawili hao walipigania uteuzi wa chama cha Democrats ambao aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton alishinda.

Kufikia sasa Seneta huyo wa Vermont ameapa kuendelea na kampeni yake katika katika mkutano mkuu wa chama hicho na amekataa kusitisha kampeni yake.

Bi Clinton atakabiliana na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi huo.