Iraq yaanzisha operesheni ya kukabiliana na vikosi vilivyohusika kuisaidia Marekani na Israel kushambulia Iran

.

Chanzo cha picha, Hayat al-Hashd al-Shaabi

    • Author, Haider Ahmad
    • Nafasi, BBC Arabic
    • Akiripoti kutoka, Baghdad
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mzozo umezuka tena nchini Iraq kufuatia operesheni za kijeshi ambazo serikali inadai imefanywa na ''vikosi ambavyo havijaidhinishwa.'' Operesheni hizo zilifanyika katika maeneo ya jangwani kusini magharibi mwa Iraq mwezi Machi mwaka jana, na kusababisha kuuawa kwa mwanajeshi wa Iraq wakati makabiliano na "kikosi cha kijeshi kisichojulikana."

Suala hilo liliibuka baada ya Jarida la Wall Street kuripoti tarehe 9 Mei, likinukuu vyanzo ambavyo havikufichulia, wakiwemo maafisa wa Marekani, kwamba Israel imeanzisha kisiri kambi ya kijeshi katika eneo la jangwani la Iraq ili kusaidia operesheni zake za kijeshi dhidi ya Iran. Hata hivyo Kamandi ya Usalama wa Iraqkimesisitiza kuwa hakuna wanajeshi wa kigeni waliopatikana katika eneo hilo.

Kamandi hiyo ilitangaza kuwa operesheni ya ukaguzi ilifanywa katika eneo ambalo baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilidai kuwa vilianzisha kambi ya kijeshi ya Israel katika miezi ya hivi karibuni, lakini hakuna dalili zozote zinazoashiria uwepo wa vikosi vya kigeni mahali hapo.

Mkuu wa kituo hicho Saad Maan, ameeleza kuwa operesheni hiyo ya ukaguzi ilifanywa kufuatia tukio la Machi 5, ambapo jeshi la Iraq ilipambana na kile alichokiita "vikosi visivyojulikana na ambavyo havijaidhinishwa" katika eneo la jangwani karibu na mji wa Karbala. Katika makabiliano hayo, mwanajeshi mmoja wa Iraq aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa.

Bw. Maan aliongeza kuwa vikosi vya Iraq "havikupata ishara yoyote inayothibitisha, uwepo wa vikosi vya kigeni, au silaha zozote wakati shughuli za ukaguzi zilipofanywa."

Mamlaka za usalama za Iraqi zilitangaza tukio hilo siku sita baada ya kuanza kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya ya Iran.

Jarida la Wall Street, likinukuu vyanzo vyake liliripoti kuwa vikosi vya Israel vilianzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Iraq ambavyo vilikuwa karibu kugundua eneo hilo baada ya mlinzi kuripoti shughuli isiyo ya kawaida katika eneo hilo.

Kulingana na Jarida hilo la Marekani, Israel ilikuwa imeanzisha kituo hicho, ambacho kilijumuisha vikosi maalum na kilitumika kama kituo cha vifaa cha Jeshi la Wanahewa la Israeli kabla ya vita, na Marekani ilikuwa na habari kuhusiana na hilo.

Kamandi ya operesheni ya pamoja: Hakuna kambi yoyote

.

Chanzo cha picha, Hayat al-Hashd al-Shaabi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kamandi ya Operesheni ya Pamoja ya Iraq imekanusha kuwepo kwa kambi au kikosi chochote kisichoruhusiwa katika ardhi ya Iraq hususan katika jangwa la Karbala magharibi mwa mikoa ya Naqeeb na Najaf na kusema kuwa operesheni na ukaguzi wa usalama katika maeneo ya jangwa na mipakani unaendelea.

Katika taarifa yake kamandi hiyo ilisema kikosi cha usalama cha Iraq kilicho na ufungamano na Kamandi ya Operesheni ya Karbala na Najaf kilipambana na "makundi haramu" yaliyokuwa yakipewa ulinzi wa anagani mnamo Machi 5.

Kamandi ya Operesheni ya Pamoja ilishutumu baadhi ya wanasiasa kwa kujaribu "kutumia tukio hili kwa maslahi ya kisiasa," na kuongeza kuwa "kauli zisizo na msingi" zinazotolewa "zinaharibu uaminifu wa Iraq na asasi zake za usalama."

Shirika hilo pia lilitishia kuchukua "hatua za kisheria" dhidi ya wale wanaoeneza "taarifa za kupotosha" ambazo zinatilia shaka mamlaka ya Iraq na hadhi ya taasisi zake za usalama.

Vyombo vya habari vya Iraq na ripoti za ndani pia zilimnukuu Mbunge wa Iraq Muhammad Khafaji akisema tarehe 4 Machi kwamba kuna "kikosi kimetua katika eneo la jangwani takriban kilomita 250 magharibi mwa mkoa wa Karbala, hasa kilomita 50 kutoka mji wa Nakhaib kuelekea jangwa la Najaf, na bado kipo katika eneo hilo hadi wa leo."

Aliongeza kuwa "asubuhi ya leo, kikosi cha jeshi la Iraq kulielekea eneo hilo kwenye magari 30 yaliyokuwa na bendera ya taifa kwenda kutathmini hali lakini kilikabiliwa katika mashambulizi ya anga. Mwanajeshi mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhi katika tukio hilo."

Mohammad Khafaji pia alisema "taarifa ya kamandi ya opresheni ya pamoja haikuwa na maelezo yoyote ya msingi."

Alisistiza "kinachoonekana sasa bila shaka ni kwamba kikosi hiki ni cha Marekani na kina helikopta na vikosi vya kijeshi," na kutoa wito kwa Kamandi ya Operesheni ya Pamoja huko Baghdad "kuchukulia suala hili kwa uzito, kwa sababu ni suala la hatari na sio dogo."

Kwa upande wake, Mbunge wa Irak Abu Turab Tamimi alisema katika taarifa kwamba kuzungumzia kuwepo kwa kambi ya kijeshi ya Israel katika Jangwa la Magharibi mwa Iraq, ndani ya eneo la mpaka wa Kamanda wa Polisi wa Mpaka wa Tano, ni "kashfa hatari ya kiusalama" na kutaka uchunguzi wa haraka wa tukio hilo ufanyike.

Bwana Tamimi alisema kuwa kuingia kwa "majeshi ya adui" ndani ya ardhi ya Iraq bila jibu kutoka kwa taasisi za usalama zinazohusika kunazua "maswali makubwa" kuhusu utendakazi wa taasisi zinazohusika katika ulinzi wa mipaka na uhuru wa Iraq.

Aliongeza kuwa kupuuza masuala hayo kutawafanya makamanda wa usalama kuwa "wajibu wa moja kwa moja, kitaifa na kisheria," na wakati huo huo kutaka kuundwa kwa kamati ya ngazi ya juu ya kuwawajibisha "watu wasio na hatia na wazembe".

Amesisitiza kuwa, mamlaka ya kujitawala ya Iraq na usalama wa mipaka yake si suala linaloweza kuchukuliwa kirahisi au kufumbiwa macho kwa maslahi ya mikataba na misingi ya kisiasa.

Vikosi vya Iraq vyaanza operesheni

Vikosi maalum vya usalama nchini Iraq vilitangaza Jumanne, Mei 12, kwamba vimeanzisha operesheni kubwa katika majangwa ya Najaf na Karbala katikati mwa Iraq. Operesheni hiyo inalenga kulinda maeneo ya jangwa na kuimarisha udhibiti wa usalama, utata ukiendelea kuhusu madai ya kuwepo kwa kambi kijeshi ya kisiri katika eneo hilo.

Sajjad Asadi, mkuu wa Makao Makuu ya Operesheni ya Euphrates alisema kuwa vikosi vya usalama vimeanza kusonga mbele kutoka kituo cha ukaguzi cha Faj kuelekea jangwa la Najaf ambako kuna kambi kadhaa za kimkakati. Alibainisha kuwa operesheni hilo inalenga kuimarisha usalama katika eneo hilo lenye urefu wa kilomita 120.

Afisa huyo aidha ameongeza kuwa operesheni ya ukaguzi inaendelezwa kutoka kiwanda cha saruji kuelekea mji wa Nakhaib na hadi kivuko cha mpaka cha Arar kwenye mpaka wa Saudi Arabia.

Ali Hamdani, kamanda wa Operesheni maalumu ya Middle Euphrates katika Vikosi vya Uhamasishaj, pia alitangaza kwamba "Operesheni ya Utawala" katika majangwa ya Najaf na Karbala imeanza kwa shoka nne, na lengo ni kulinda barabara kati ya Karbala na Nakhaib.

Bwana Hamdani alieleza kuwa operesheni hii inafanywa kwa amri ya Amiri Jeshi Mkuu na chini ya uangalizi wa Mkuu wa Majeshi, na kwamba vikosi kadhaa za kijeshi zinashiriki.

Huku mzozo wa kikanda ukiendelea kufukuta, vikosi vya usalama vya Iraq vinajaribu kuimarisha udhibiti wake ili kuzuia unyonyaji wowote unaotokana na mapungufu ya kijiografia.