Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Tottenham wana imani ya kumsajili winga wa Man City Savinho

.

Chanzo cha picha, GETTY

Maelezo ya picha, Savinho
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Tottenham wanaendelea kuwa na imani ya kumsajili winga wa Brazili mwenye umri wa miaka 22 wa Manchester City, Savinho. (Fabrizio Romano)

Real Madrid hawana mpango wa kumsajili kiungo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 30 wa Manchester City, Rodri, katika dirisha hili la usajili la majira ya joto. (Athletic - inahitaji usajili)

AC Milan wanamfuatilia kiungo wa Uingereza na Manchester City mwenye umri wa miaka 26, Phil Foden. (Tuttosport)

Hata hivyo, dili lolote kumhusu Foden litawezekana tu ikiwa AC Milan watafanikiwa kumuuza mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 27, Rafael Leao. (Tuttosport)

Beki wa Leicester City, Ben Nelson, ameueleza uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka, huku Manchester United na West Ham zikionyesha nia ya kumsajili Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

.

Chanzo cha picha, GETTY

Maelezo ya picha, Joao Palhinha

Arsenal wanatarajiwa kumsajili beki wa Uingereza, Elijah Upson, baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 kukataa mkataba mpya na Tottenham. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa Ureno, Joao Palhinha, anatarajiwa kurejea Bayern Munich kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya, huku taarifa zinazodai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anakaribia kujiunga na Aston Villa zikiwa si za kweli. (Sky Germany)

Liverpool wanatarajiwa kumsajili kiungo wa Colombia mwenye umri wa miaka 17, Samuel Martinez, kutoka Atletico Nacional kwa ada ya takriban pauni 750,000. (Athletic - Subscription Required)

Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid wanaonyesha nia ya kumsajili beki wa Tottenham na Argentina mwenye umri wa miaka 28, Cristian Romero. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Balogun

Juventus wako mbele ya Borussia Dortmund na Sunderland katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Marekani mwenye umri wa miaka 25, Folarin Balogun, kutoka Monaco. (Mundo Deportivo)

Chelsea bado wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, Maxence Lacroix, lakini bei inayotakiwa na Crystal Palace ya takriban pauni milioni 70 inakwamisha dili hilo. (Caught Offside)

Juventus wanaendelea kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil wa Tottenham mwenye umri wa miaka 29, Richarlison. (Gazzetta dello Sport - In Itali),

Everton ndio wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kumsajili winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, Jaden Philogene, kutoka Ipswich. (Football Insider)