Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Siku ya Mwisho ya Dirisha la Uhamisho: Fahamu wachezaji wote waliosajiliwa
01:05 Dario Osario ajiunga na Crystal Palace akitokea FC Midtjylland kwa mkopo.
Dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya Primia na English Football League (EFL) lilifungwa jana Jumanne saa 23:00 BST.
Tukufahamishe kwa kifupi mikataba yote iliyothibitishwa rasmi katika siku ya mwisho ya usajili, huku ukiendelea kufuatilia habari na tetesi za usajili zinazoendelea kujitokeza.
Pia kumbuka kuwa dirisha la usajili kwa klabu za Scottish Premiership litafungwa Alhamisi saa 17:00 BST, wakati klabu za Women's Super League (WSL) zitakuwa na muda hadi 23:00 BST siku hiyo hiyo kukamilisha usajili wao.
Usajili wa Ligi ya Premier – Septemba Mosi
01:01 Juan Riquelme Angulo amekamilisha uhamisho wake kwenda Sunderland akitokea Independiente del Valle kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
00:45 Jean-Matteo Bahoya amehamia Leeds United kutoka Eintracht Frankfurt kwa mkopo.
00:45 Quinten Timber amejiunga na Crystal Palace akitokea Marseille kwa ada ambayo haijatangazwa.
00:15 David Affengruber amesajiliwa na Fulham kutoka Elche kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
00:10 Ben Chilwell amejiunga na Crystal Palace akitokea RC Strasbourg kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
00:00 Ainsley Maitland-Niles amehama kutoka Olympique Lyon kwenda Everton huku kima chake kikiwa hakijawekwa wazi
23:50 Enzo Fernandez ameondoka Chelsea na kujiunga na Manchester City kwa dau la pauni milioni 125, moja ya uhamisho mkubwa kabisa wa dirisha hili.
23:45 Christos Mouzakitis amehamia Hull City kutoka Olympiakos kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi
23:41 Chema Andres amejiunga na Brighton & Hove Albion akitokea VfB Stuttgart kwa ada ya pauni milioni 15.5.
23:30 Sorba Thomas: Amehama kutoka Stoke City kwenda Hull City kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
23:30 Zian Flemming: Amejiunga na Ipswich Town akitokea Burnley kwa dau linaloripotiwa kufikia pauni milioni 20.
23:15 Tosin Adarabioyo: Ameondoka Chelsea na kuhamia Tottenham Hotspur kwa ada ambayo haijatangazwa rasmi.
22:50 Jack Grealish: Amejiunga na Everton kwa mkopo akitokea Manchester City hadi mwisho wa msimu.
22:45 Melvin Bard: Amehamia Leeds United kutoka Nice kwa mkataba wa mkopo.
22:31 Robinio Vaz: Amejiunga na Hull City kwa mkopo akitokea AS Roma.
22:30 Manuel Angel: Amehama kutoka Real Madrid kwenda Fulham kwa ada ya takribani pauni milioni 3.
22:30 Hugo Larsson: Amejiunga na Fulham kwa mkopo akitokea Eintracht Frankfurt.
22:15 Brooke Norton-Cuffey: Amehamia Hull City kutoka Genoa kwa dau la pauni milioni 12.
22:05 Tim Iroegbunam: Ameondoka Everton na kujiunga na Hull City kwa ada ya pauni milioni 22.
22:00 Mykhailo Mudryk amejiunga na Tottenham Hotspur akitokea Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
21:00 Iliman Ndiaye amehamia Manchester City akitokea Everton kwa ada inayoripotiwa kufikia pauni milioni 65 (£65m).
20:00 Kevin Danso ameondoka Tottenham Hotspur na kujiunga na Sunderland kwa mkopo.
19:00 Lucca Brughmans amejiunga na Liverpool akitokea Genk kwa ada ya uhamisho ya takribani pauni milioni 30 (£30m).
15:00 Matias Fernandez-Pardo amekamilisha uhamisho wake kwenda Newcastle United akitokea Lille kwa ada ya karibu pauni milioni 51.4 (£51.4m).
13:20 Honest Ahanor amehamia Crystal Palace kutoka Atalanta kwa mkataba wa mkopo.
12:30 Taylor Harwood-Bellis amejiunga na Aston Villa akitokea Southampton kwa ada ya takribani pauni milioni 29 (£29m).
11:30 Ibrahim Mbaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Paris Saint-Germain (PSG) kwenda Aston Villa kwa dau la pauni milioni 47 (£47m).
10:30 Ilyas Ansah amehamia Hull City akitokea Union Berlin kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
Kimataifa
22:20 Cody Drameh ameondoka Hull City na kujiunga na AS Roma kwa ada ya takribani pauni milioni 3.4.
20:12 Nathan Patterson amehamia Torino kutoka Everton kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
20:00 Wilfried Gnonto amejiunga na Fiorentina kwa mkopo akitokea Leeds United.
20:00 Robert Sanchez amehamia Como kwa mkopo kutoka Chelsea.
19:30 Dario Essugo amejiunga na Strasbourg kwa mkopo akitokea Chelsea.