Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Jaribio la Liverpool kumsajili Gusto lagonga mwamba
Liverpool ilijaribu kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa Malo Gusto, 23, katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili, lakini mpango wa mkopo ulivunjika baada ya Chelsea kutaka kumuuza mchezaji huyo kwa mkataba wa kudumu. (Fabrice Hawkins)
Chelsea ilifanya jaribio la mwisho kumsajili kiungo wa Bournemouth Alex Scott, 23, kama mbadala wa Enzo Fernandez, lakini Bournemouth haikuwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa timu ya England chini ya miaka 21 msimu huu wa joto. (Mirror)
Arsenal ilikataa ombi la Chelsea la kumtaka kiungo wa Hispania Martin Zubimendi, 27. Chelsea ilikuwa ikimwona Zubimendi kama chaguo la kuziba pengo lililoachwa na Enzo Fernandez. (The Sun)
Arsenal imekataa ombi la Chelsea la kutaka kumsajili kiungo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27, Martin Zubimendi. (Sun)
Manchester United inapanga kuongeza mabeki watatu dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwakani, huku mustakabali wa baadhi ya mabeki wake wakuu akiwemo Luke Shaw, Harry Maguire, Lisandro Martinez na Matthijs de Ligt ukitarajiwa kutathminiwa msimu huu. (Sun)
Mshambuliaji wa Manchester United, Chido Obi mwenye umri wa miaka 18, anataka kuondoka kwa mkopo kwenda Uholanzi au Denmark, huku Feyenoord ikiwa miongoni mwa klabu zinazovutiwa naye. Dirisha la usajili katika nchi hizo linafungwa Jumatano. (Mirror)
Everton ilikuwa na nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Monaco, Jordan Teze, 26, lakini viongozi wa klabu hiyo ya Ligue 1 walimkatalia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Nice-Matin)
Beki wa England Fikayo Tomori, 28, atarejeshwa kwenye kikosi cha AC Milan chini ya kocha Ruben Amorim baada ya kukataa kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A wakati wa dirisha la usajili. (Di Marzio)
Mshambuliaji wa Liverpool Cody Gakpo, 27, amefanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo baada ya Liverpool kukataa kuidhinisha uhamisho wake kwenda Manchester City. (ED)
Wrexham inaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huru Jamie Vardy, 39, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka klabu ya Sao Paulo ya Brazil na Sheffield Wednesday katika mbio za kumsaka nyota huyo wa zamani wa England. (TalkSport)
Klabu za Al-Ittihad imejiunga na Diriyah, zinazoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia, zinammnyatia winga wa Aston Villa na Jamaica, Leon Bailey, 29. (The Athletic)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi