Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei yuko wapi?
Mojtaba Khamenei, ambaye alitangazwa kuteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, ndani ya wiki moja tangu kuuawa kwa baba yake, bado hajaonekana hadharani.
Hakukosa tu kuhudhuria mazishi ya baba yake, Ayatollah Ali Khamenei, bali pia hakutoa hata ujumbe wowote, jambo lililozua maswali kuhusu mipango yake kwa Iran wakati ambapo nchi hiyo inakabiliwa na misukosuko.
Maafisa wa ngazi ya juu walisema kuwa Mojtaba, ambaye anasemekana kuingia madarakani kwa msaada wa jeshi la Iran (IRGC), alipata majeraha makubwa usoni na sehemu nyingine za mwili katika shambulio hilo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ingawa kiongozi huyo mpya bado anafanya maamuzi muhimu, hali yake ya afya bado haimruhusu kujitokeza hadharani.
Sasa, baada ya Iran kulipiza kisasi dhidi ya Marekani wiki hii, nafasi na hali ya afya ya Mojtaba zimeibua mjadala mkubwa.
"Ninaelewa kuwa kwa sababu za kiusalama hapaswi kujitokeza hadharani, ila nchi inapitia kipindi kigumu sana," alisema Taghi, mfanyabiashara kutoka Isfahan ambaye hakutaka jina lake kamili kujulikana.
"Si lazima Kiongozi Mkuu ajitokeze mara kwa mara. Lakini hata kama amejeruhiwa, watu wanataka kuona kwamba kiongozi wao yuko hai na bado anaiongoza nchi."
Je, jamaa na familia ya Mojtaba walimwakilisha katika mazishi ya babake?
Kamati ya mazishi ya babake ilisema siku ya Alhamisi kwamba mazishi yaliongozwa na wasomi wa kidini, huku sala ya mwisho ya mazishi ya Khamenei ikiongozwa na wanawe watatu, ambayo ilifanyika katika msikiti mkubwa na mtakatifu zaidi wa Iran.
Hii kwa mara nyingine inadhihirisha umuhimu wa familia hii katika uongozi wa Iran.
Ndugu watatu wa Mojtaba Khamenei hawaonekani kuwa na ushawishi mkubwa katika uongozi wa kisiasa wa Iran, na inaaminika kwamba hawatakuwa na nafasi kubwa katika siku za mbeleni.
Hata hivyo, wote wana hadhi ya juu ya kidini.
Wakati huo huo, Ali Khamenei, aliyetajwa kuwa mmoja wa watu muhimu sana katika mapinduzi ya Irani ya 1979, alisemekana kuzungumza kwa niaba ya Mojtaba katika maombolezo ya Ijumaa.
Hivyo, alijaribu kutumia uhusiano wa kifamilia ili kuonyesha mwendelezo wa mfumo wa kikasisi unaotawala.
Ingawa Mojtaba Khamenei hatimaye hakuonekana moja kwa moja kwenye mazishi ya babake, kulikuwa na uvumi kwamba angetoa ujumbe wa video uliorekodiwa awali au picha mpya.
."Uongozi thabiti unawezaje kuwepo ikiwa hakuna mtu wa kuchukua nafasi yake?"
"Hii bila shaka itakuwa na athari katika siku zijazo, hata kama itachukua muda. Mfumo huu jinsi ulivyo hauwezi kudumu kwa muda mrefu," alisema Ali Ansari, profesa wa historia ya kisasa katika Chuo Kikuu cha St Andrews Scotland.
Wana uhusiano na uongozi wa vikosi vya Mapinduzi
Zaidi ya watu 20 waliohojiwa na shirika la habari la Reuters walisema kuwa kutokuwepo kwa uongozi wakati wa mzozo ni suala linalozua wasiwasi mkubwa katika siasa za Iran.
"Kutokuonekana kwake hadharani, hasa baada ya kumalizika kwa vita na mazishi ya kiongozi wa nchi, kunaweza kuzua mashaka makubwa na kuzidisha migawanyiko," alisema Mohammad Reza, mwenye umri wa miaka 51 kutoka Tehran.
Nafasi ya Kiongozi Mkuu nchini Iran ni tofauti na nafasi za uongozi katika nchi nyingine, kwani itikadi ya Jamhuri ya Kiislamu inamtazama kiongozi huyo kama mwakilishi wa kidunia wa Imamu wa 12 wa Kishia, ambaye inaaminika alitoweka katika karne ya tisa.
Bado haijulikani wazi jinsi Mojtaba Khamenei atakavyoimarisha nafasi hiyo.
Kiongozi wa kwanza wa Iran, Ayatollah Ruhollah Khomeini, alikuwa baba wa Mapinduzi ya Iran na kiongozi aliyeheshimika sana pamoja na kuwa msomi mashuhuri wa kidini, ambaye maneno na mafunzo yake yaliheshimika sana.
Mrithi wake, Ali Khamenei, alikuwa rais wakati alipoteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu, na hakuchukuliwa kuwa msomi wa kidini wa kiwango cha juu au mwenye mamlaka ya kidini sawa na Khomeini.
Katika kipindi chake cha miaka 37 madarakani, Ali Khamenei amejiimarisha mwamuuzi mkuu wa kisiasa nchini humo, akiwapiku wapinzani wake kimkakati na kuwa na uungaji mkono kutoka kwa jeshi.
Mojtaba, kama ilivyoelezwa, hana elimu ya kidini inayolingana na ya baba yake, wala sifa ya misimamo binafsi ya kisiasa.
Hata hivyo, aliwahi kusimamia ofisi kubwa ya baba yake na ana uhusiano wa karibu na taasisi za serikali, jeshi la Iran IRGC.
Mtazamo, nguvu, na mtindo wake wa uongozi bado havijajulikana wazi, ila inaaminika kuwa jeshi litaendelea kuwa na nafasi muhimu katika uongozi wake.
Wakati Iran ikikabiliwa na vita, uchumi wake ukiharibiwa na vikwazo, na wananchi wake wakikabiliana na changamoto nyingi, ripoti zinaonyesha kuwa kutokuwepo kwa kiongozi huyo au kutojitokeza kwake hadharani kumezua wasiwasi.