Tetesi za soka: Vigogo wanne wa Ligi Kuu England 'watoana roho' kwa Alex Scott

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kiungo wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 22, Alex Scott, anawaniwa na vigogo vinne vya Ligi Kuu England, ambao ni Arsenal, Manchester United, Manchester City na Chelsea.(Talksport)

Arsenal imekubali kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji, Leandro Trossard, mwenye umri wa miaka 31, kwenda Besiktas ya Uturuki kwa euro milioni 20, sawa na pauni milioni 17.(Athletic - subscription required)

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 21, bado yupo kwenye rada za Real Madrid huku miamba hiyo ya Hispania ikitafuta kuimarisha safu yao ya kiungo. (Fichajes - in Spanish)

Manchester City imeziambia klabu zinazomtaka beki wa Ureno, Ruben Dias, mwenye umri wa miaka 29, ikiwemo Real Madrid, kwamba mchezaji huyo hauzwi katika dirisha hili la usajili.(Teamtalk)

Como ya Italia inaandaa ofa ya takribani pauni milioni 30 kwa ajili ya beki wa Chelsea na England, Trevoh Chalobah, mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports)

Roma iko tayari kuongeza kasi ya kumsajili mshambuliaji wa Marseille, Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 24, kwa ada ya euro milioni 45, sawa na pauni milioni 38.5.(Corriere dello Sport - in Italian)

Paris Saint Germain inafahamu italazimika kuweka mezani ada ya kihistoria ili kumng'oa mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Atletico Madrid.(Fichajes - in Spanish)

Atletico Madrid inaandaa ofa mpya kwa nahodha wa Sporting Lisbon, Morten Hjulmand, baada ya ofa yao ya euro milioni 35 kwa kiungo huyo wa Denmark kukataliwa.(A Bola - in Portuguese)

West Ham ina nia ya kumsajili winga wa Everton, Dwight McNeil, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha hili la usajili. (Sky Sports)

Beki wa zamani wa Uholanzi, Daley Blind, mwenye umri wa miaka 36, yuko karibu kurejea Ajax baada ya kuondoka Girona ya Hispania.(Algemeen Dagblad - in Dutch)

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid