Nini huzuia wanawake wengi kutofika kileleni?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mwanamke mmoja kati ya wawili hufika kileleni mara nyingi wakiwa pekee yao ikilinganishwa wakiwa na wenza wao wakati wa tendo la ndoa, hii ni kulingana na utafiti kuhusu raha anayopata mwanamke wakati anashiriki ngono, iliyochapishwa katika jarida la Archives of Sexual Behaviour.

Wanasayansi walipitia majibu kutoka kwa wanawake zaidi ya elfu 28,000 na kugundua kuwa tatizo si anatomia ya mtu bali uhusiano wake na mwenza wake.

Kufika kileleni bila mwenza

Kulingana na utafiti 47% ya wanawake wengi walisema walifika kileleni haraka na kushuhudia raha ya kujamiiana wakati wakijipiga punyeto.

Walipoulizwa na watafiti mbona hali iko hivyo, wanawake waliohojiwa walitoa majibu tofauti

Zaidi ya nusu ya wanawake wanaojifikisha kileleni pekee yao walisema ni kutokana na kukosa msisimuko wa kutosha kutoka kwa wenza wao.

Hii inaweza kujumuisha kubembelezana, kutiana nyege kwa muda kabla ya kushiriki ngono.

Wanawake wanaofika kileleni kwa urahisi wanapokuwa na wenzi wao, zaidi ya theluthi mbili walisema kwamba wenzi wao wanajua hasa ni aina gani ya msisimko wa kingono wanaouhitaji.

Kulingna na Karen Blair uwezo wa mwanamke kufika kileleni haitegemei maumbile ya kimwili pekee, bali ubora wa mawasiliano na mwingiliano wa kingono kati ya watu wawili.

Tatizo si anatomia

Waandishi wa utafiti huo wanaeleza kwamba, licha ya miaka mingi ya mjadala kuhusu umuhimu wa kisimi katika kufikia kileleni, kupenya ukeni wakati wa kujamiiana na mwenzi wako bado ndicho kitendo cha ngono kinachofanyika mara nyingi.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa msisimko wa kisimi una uwezekano mkubwa zaidi wa kumsaidia mwanamke kufikia kileleni kuliko kupenya tu ukeni.

Karen Blair pia anasema tafiti za awali za kisayansi pia zina wazo sawia na hilo.

Ngono inayofanyika kwa njia ya kupenya ukeni kwa kawaida huwapa wanaume raha zaidi, ilhali kwa wanawake wengi, msisimko wa kisimi hubaki kuwa njia yenye uhakika zaidi ya kufikia kileleni ikiambatana na mwanaume kupenya uken

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hoja si teknolojia pekee.

Sababu ya pili iliyotajwa mara nyingi na wanawake kuhusu kwa nini wao hufikia kileleni mara nyingi zaidi wanapojipiga punyeto , ni kutokuwepo na shinikizo la "kulazimika kuonyesha matokeo" ya kushiriki.

Wanawake wanapokuwa pekee yao, hawahisi shinikizo, hawahangaiki kuhusu kulazimika kufikia kileleni, huwa hawana aibu sana kuhusu miili yao, na huwa rahisi zaidi kupumzika wakichoka.

Sababu nyingine inayochochea wanawake kutofika kileleni wanapokuwa na wenzi wao ni ugumu wa kuzungumza na uwazi kuhusu wanachokipenda wakati wanashiriki ngono.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Fumbo

Ingawa kujipiga punyeto mara nyingi huongeza uwezekano wa kufikia kileleni kwa haraka, wanawake wengi ambao hufika kileleni wakiwa na wenzi wao, kwa ujumla wameridhika na Maisha yao ya ngono.

Waandishi wa utafiti huu wanaelezea hali hii kwa kusema kwamba aina hizi mbili za kingono hutimiza majukumu tofauti.

Kujipiga punyeto humpa mtu hisia ya kuwa na udhibiti, kuzingatia kikamilifu hisia zake mwenyewe, na kutokuwa na hofu ya kuhukumiwa.

Kwa upande mwingine, kufanya ngono na mwenzi kunahusishwa na kuwa na ukaribu wa kihisia na kuaminiana.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mara ambazo mwanamke hufikia kileleni huelezea takriban 11% pekee ya tofauti zinazojitokeza katika kiwango cha kuridhika kwa wanawake na maisha yao ya ngono.

Kufikia kileleni pekee hakuhakikishii mtu atakuwa na maisha ya ngono yanayoridhisha. Hata miongoni mwa wanawake ambao hawakuridhika na maisha yao ya ngono, wengi walikuwa wakifikia kileleni mara kwa mara.

Wakati huohuo, baadhi ya wanawake waliosema maisha yao ya ngono ni mazuri hawakuwa wakifikia kileleni kila walipofanya ngono.

Huenda ufunguo wa jambo hili upo ndani ya mwanamke mwenyewe.