Nani aliyejenga Al-Kaaba?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kaaba, iliyoko katikati ya Msikiti Mkuu katika mji wa Makka, ni sehemu takatifu zaidi kwa Waislamu na ndiyo eneo ambalo Waislamu huelekea wanaposwali.
Kuzuru Al-Kaaba angalau mara moja katika maisha ya Muislamu ni moja ya nguzo tano za Uislamu, sababu nyingine inayowafanya wafanye juhudi za kuhiji.
Takwimu zinaonyesha kuwa takriban watu milioni 13 hadi 15 hutembelea makaburi hayo kila mwaka, wakiwemo zaidi ya milioni 11 wanaofanya Umra na milioni 2 hadi 3 wanaohiji kila mwaka.
Mamilioni ya mahujaji kutoka kote ulimwenguni tayari wameanza kusafiri kuelekea eneo hilo Takatifu kutekeleza ibada ya Hija ya 2026.
Ili kufahamu zaidi kuhusu chimbuko na ujenzi wa Kaaba, BBC iliwasiliana na Dk.Ibrahim Disina, mwanazuoni wa Kiislamu wa Nigeria aliyesomea masuala ya dini nchini Saudi Arabia, ambako Kaaba ipo.
Msomi huyo alimpa mwandishi ukurasa maalum juu ya historia ya jengo takatifu ili kuandika makala hii.
"Habari hizi zote ni za kweli na za uhakika, ni tovuti ya wasomi wetu kutoka Qatar, Kuwait na Saudi Arabia," alisema Sheikh Disina.
Kaaba miaka 2000 kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu
Katika Uislamu, Mwenyezi Mungu anaelezea mahali pale kama 'Nyumba ya Kwanza' ya ibada duniani kama ilivyoelezwa katika kitabu kikuu, Quran.
"Hakika Nyumba ya kwanza (ya ibada) iliyoanzishwa kwa watu ni ile iliyoko Bakka iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu." (Al-Imran 3:96).
Wanazuoni wengi wa Kiislamu kama vile Imam Baghwi wanaelewa kuwa Al-Kaaba ni jengo la kwanza, kwamba ni jengo ambalo liliibuka kwa mara ya kwanza kutoka kwenye maji wakati mbingu na ardhi zilipoumbwa miaka 2000 kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Hata hivyo, baadhi ya wanachuoni wanapendelea kuamini kwamba Al-Kaaba lilikuwa jengo la kwanza la ibada duniani, lililojengwa na Nabii Adam.
Zaidi ya hayo, wapo wanaoamini kuwa Al-Kaaba ilijengwa na Malaika muda mrefu kabla ya Mungu kumuumba Nabii Adam.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nabii Ibrahim (AS)
Wanazuoni wa Kiislamu wanakubali kwamba moja ya sababu kwa nini Mungu alimuongoza Nabii Ibrahim hadi Makka ilikuwa ni kuirejesha Al-Kaaba, ambayo alikuwa ameijenga kuizunguka.
Nabii Ibraahiym na mwanawe Ismaili walichukua jukumu la kuijenga upya Al-Kaaba, huku Ismaili akitoa mawe na Nabii Ibrahim akijenga jengo hilo, na walilijenga kwa urefu usioweza kufikiwa kwa mikono.
Hapo ndipo Nabii Ibrahimu alipomtaka Ismaili ampe jiwe ambalo angeweza kulikanyaga ili kulikamilisha jengo hilo - jiwe ambalo leo linajulikana kwa jina la 'Maqama Ibrahim', lililoko karibu na Al-Kaaba.
Watu wa kabila la Quraish
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kulikuwa na makabila na jumuiya nyingi zilizoitunza Al-Kaaba, wakiwemo Waamaleki, Jurhum, Khuza'a, na Waquraishi, ambao walichagua kuchukua jukumu la kutunza mahali hapa patakatifu.
Kabila la Waarabu la Quraishi liliamua kuijenga upya Al-Kaaba ili maji yasiharibu tena msingi wa jengo hilo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Maquraishi walitumia miaka mitano kujenga jengo hilo kabla ya kumtuma Mtume Muhammad (SAW) mwaka 605, wakiongeza urefu wa jengo hilo kwa orofa 9, na kulifanya liwe na urefu wa orofa 18. Pia walizuia mlango wa magharibi wa jengo hilo, wakiacha ule wa mashariki tu, kuzuia kuingia.
Ilikuwa ni wakati wa utawala wa Maquraishi ambapo jengo hilo liliezekwa paa kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa rasilimali, ilibidi waondoke sehemu ya muundo wa awali, ambao sasa unaitwa 'Hijr Isma'il', nje ya Ka'ba.
Hadithi nyingi zinaonyesha jinsi Mtume Muhammad (SAW) alivyogawanya makabila ya Waarabu kuhusu ujenzi wa Al-Kaaba.
Abdullah bin Zubair 64 AH
Mnamo mwaka wa 64 Hijria, miaka 31 baada ya kifo cha Mtume Muhammad (saww), Abdullah ibn Zubair aliibomoa Al-Kaaba hadi ardhini na kuijenga upya baada ya kuchomwa moto wakati wa shambulio la Mecca na Yazid ibn Mu'awiyah.
Hapo ndipo alipoijenga na kuongeza nafasi ambayo Maquraishi hawakuiongeza, yaani 'Hijr Isma'il'.
Pia akaongeza kimo chake kwa mikono 10 na kuongeza milango yake miwili kutoka mashariki na magharibi chini ya jengo hilo.
Abdulmalik bin Marwan 73 BH
Baada ya Abdul Malik bin Marwan kumuua Abdullah bin Zubair na kuiteka Makkah, aliamuru Al-Kaaba ijengwe upya kama ilivyokuwa kabla ya Abdullah bin Zubair kuitengeneza.
Hili lilipelekea kubomolewa kwa lango la Magharibi la Ka'ba, na 'Hijr Isma'il' kutolewa nje, na kusalia na lango moja tu, ambalo liliinuliwa juu.
Hata hivyo, urefu wa jengo uliachwa vile ulivyokuwa, kwani Abdullah bin Zubair alikuwa ameupanua kwa dhiraa 10.
Wanahistoria wanasema kwamba Nyumba ya Mwenyezi Mungu ilibakia kama alivyoiacha Abdulmalik bin Marwan hadi mwaka 1039 Hijiria.
Sultan Murad Khan - 1039 AH
Wanahistoria wanasema kwamba Al-Kaaba ilipata mafuriko ambayo yaliharibu sehemu za jengo hilo mnamo tarehe 19 Sha'ban, 1039 Hijria, baada ya mafuriko hayo kuharibu Msikiti Mkuu wa Makka na ndani ya Kaaba.
Maji yaliingia ndani ya chumba na kuharibu kuta za kaskazini, mashariki, na magharibi pamoja na ngazi zinazoelekea kwenye paa la chumba.
Hii ilipelekea watoa fatwa wakati huo kukubali kubomoa sehemu zilizoharibika ili kuzijenga upya, jambo ambalo lilikamilishwa na Sultan Murad Khan, Sultani wa Dola ya Ottoman, mnamo tarehe 2 Dhul-Hijjah katika mwaka wa 1040 Hijria.
Muhammad Ali Pasha - 1239 AH
Mwishoni mwa 1939 baada ya Hijra, gavana wa Misri, Muhammad Ali Pasha, aliamuru kusafishwa kwa eneo la karibu na Ka'ba ili kuondoa matope na mchanga wote ambao ulikuwa umerundikana kutokana na mafuriko yaliyotokea wakati huo.
Baada ya hayo, jengo hilo lilifanyiwa ukarabati mdogo ambao uliongeza thamani yake.
Abdulaziz bin Abdul Rahman Al Saud - 1924
Mfalme wa kwanza wa Saudia, Abdul'aziz bin Abdul Rahman Al Saud, ndiye aliyeipamba upya Kaaba, ikiwa ni pamoja na kufungua tena milango ya jengo hilo baada ya kuingia ndani ya chumba hicho.
Na hii inachukuliwa kuwa kazi kubwa zaidi ya kisasa iliyofanywa kwenye Msikiti wa Mecca na Kaaba tangu kuanzishwa kwa Ufalme wa Saudi mnamo 1924.
Wakati huo, sehemu ya juu na ya chini ya Ka'bah ilirekebishwa. Kuta zote za chumba pia zilirekebishwa na dari na sakafu zilipambwa.
Mfalme Fahad - 1997
Wakati wa utawala wa Mfalme wa Saudi Fahd, Kaaba ilifanyiwa ukarabati ambao bado unaonekana hadi leo, ikiwa ni pamoja na paa, nguzo zake tatu, milango ya ndani, sakafu, na msingi wa jukwaa.
Matengenezo mengine ni pamoja na kuongezwa kwa ukuta wa Hijr Isma'il.















