Tetesi 5 kubwa za Soka Ulaya

Chanzo cha picha, Getty Image
Liverpool iko njia panda kumuuza Mo Salah ama la, baada ya kupokea dau nono kutoka Uarabuni. Gwiji wa zamani wa klabu hiyo, Jamie Carragher amesema Liverpool haipaswi kukataa dau la £200m kutoka Al-Ittihad kwa ajili ya Mo Salah (The Mirror).

Chanzo cha picha, getty Image
Al Duhail inakaribia kumnasa Philippe Coutinho ! Makubaliana tayari na Aston Villa ambapo atatua kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Qatari akizikataa Besiktas na Betis (Romano).

Chanzo cha picha, getty Image
Rais wa PSG Al Khelaifi amejitokeza kuzungumzia uhusiano wake na nyota wa klabu hiyo Kylian Mbappe: “Mbappé ni mchezaji bora na mtu mzuri, naweza kuthibitisha hilo. Tunauhusiani mzuri. Niamini — PSG, nje na ndani ya uwanja, sasa tuna muunganiko mzuri kuliko wakati wote” (Romano).

Chanzo cha picha, Getty Image
Mikel Arteta amemwambia Nicolas Pepe kwamba hatachezea tena Arsenal huku vigogo wa klabu hiyo wakipambana kumuuza Mu-Ivory cost huyo (The Sun)

Chanzo cha picha, Getty Image
Wolves inapambana na West Ham kunasa saini ya Jesse Lingard, kwa mujibu wa Sky Sports. Lingard yuko huru baada ya kuachwa na Nottingham Forest.



























